Diamond na Zari Wamepata Mtoto wa Kiume Leo Des. 6, Bofya Hapa Kuona Pichaz



diamond-na-zari
chibu-jr-1
Pretoria, Afrika Kusini: TAARIFA njema kwa mashabiki wa msanii wa Bongo Fleva hapa nchini, Nasbu Abdul “Diamond Platnumz” ambaye leo leo Desemba 6, 2016, mpenzi wake Zarina Hassan “Zari The Boss Lady” amejifungua mtoto wa kiume katika Hospitali ya Netcare iliyopo mjini Pretoria nchini Afrika Kusini. Mtoto aliyekuwa akisubiliwa kwa hamu kubwa.zari-na-mond-kid
k
chibu-jr-1
Kwa mujibu wa taarifa aliyoitoa Diamond kupitia ujumbe aliouandika kwenye akaunti yake ya Instagram ameeleza kuwa mtoto wao huyo amezaliwa majira ya saa 8:35 usiku kwa saa za Afrika kusini ambazo ni sawa na saa 10:35 alfajiri kwa saa za Afrika Mashariki.
Mbali na Diamond kuposti picha zikionesha miguu ya mtoto huku akieleza kuwa mpaka sasa bado hawajapata jina la kumuita mtoto wao, mpenzi wake, Zari ameposti picha ikionesha mikono ya kichanga chao na kuwashukuru wale wote waliokuwa wakimuombea kwa Mungu ili ajifungue salama.

Mtoto huyo anakuwa ni wa pili kwa Diamond kuzaa na mpenzi wake Zari baada ya mtoto wao Tiffah aliyezaliwa August 6, 2015. Kwa zari ni mtoto wa tano huku wengine wakubwa watatu aliyozaa na aliyekuwa mumewe, Ivan nchini Uganda.

Comments

Popular posts from this blog