Trump Kusitisha Uagizwaji wa Ndege Mpya za Air Force One
Rais Mteule wa Marekani, Donald Trump amesema anataka kufuta ombi la ununuzi wa ndege mpya za Air Force One ambazo hutumiwa na marais wa Marekani.
Wiki sita kabla ya kuchaguliwa,
aliandika kwenye akaunti yake ya Twitter kuwa: “Boeing wanaunda ndege
mpya aina ya 747 Air Force One za kutumiwa na marais siku zijazo, lakini
gharama yake imezidi, zaidi ya $4 billion. Futa oda hiyo!”
Serikali ya Marekani iliingia kwenye
mkataba na kampuni ya Boeing ili kutengenezwa kwa ndege hizo mbili au
zaidi za kuwabeba marais.
Ndege hizo zilitarajiwa kukamilika na kuanza kutumiwa mwaka 2024.
Hisa za kampuni ya ndege ya Boeing
zilishuka kwa zaidi ya 1% baada ya ujumbe huo wa Trumpp kwenye Twitter,
ingawa zilijikwamua baadaye.
Trump hatarajiwi kutumia ndege hizo mpya, iwapo hatashinda uchaguzi wa muhula wa pili wa mwaka 2020.
Comments
Post a Comment