Serikali Kuanzisha Tuzo za Mitandao ya Kijamii kwa Wanahabari
Mwandishi wa habari wa mtandao huu,
Denis Mtima (kushoto) akikabidhiwa kadi ya kujiunga na mfuko wa hiari wa
mwanachama wa PSPF na Waziri Nape Nnauye.
Nape akimkabidhi mwanadada mwandishi wa habari, kadi ya ATM ya NMB.
…Akisisitiza jambo fulani kwa wanahabari.
…Akizungumza jambo.
Mwakilishi wa wadhamini wa semina
hiyo ambaye ni Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Vicky Bishubo,
akizungumza jambo kwenye hafla hiyo.
Mkurugenzi wa mfuko wa hiari wa mwanachama wa PSPf, Adam Mayingu ambao nao walikuwa wadhamini wa semina hiyo, akizungumza jambo.
Vicky Bishubo akimkabidhi Nape zawadi iliyokuwa imeandaliwa kutoka NMB.
Taswira ilivyoonekana katika semina hiyo.
WAZIRI wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, amesema serikali inatarajia kuanzisha
Tuzo za Umahiri kwa waandishi wa habari wa mitandao ya kijamii (blogs na
website) kuanzia mwakani 2017.
Hayo ameyasema jana wakati akifunga
semina kwa mtandao wa wamiliki wa mitandao ya kijamii na wanahabari
nchini Tanzania maarufu kama Tanzania Bloggers Network (TBN).
Wakati huohuo alikabidhi kadi za ATM za
NMB za kutolea fedha kwa wanahabari waliofungua akaunti zao za ‘Chap
Chap Account’ na za kujiunga na mfuko wa hiari wa pensheni wa mwanachama
(PSPF) jijini Dar es Salaam.
Semina hiyo ilikuwa ya siku mbili ambayo
ililenga juu ya uendeshaji mitandao ya kijamii, namna ya kuzingatia
maadili na namna ya kunufaika na mitandao hiyo kwa waendeshaji.
Akizungumza katika hafla hiyo, Nape
alisema serikali inaitambua mitandao ya kijamii (blogs na website) kuwa
vyombo vya habari nchini kwani vina nguvu kubwa katika kupasha habari
kwa jamii hata kuliko magazeti.
Alisema katika uchaguzi mkuu wa urais wa
2015 mitandao ya kijamii ndiyo iliyokuwa ikitumiwa kwani iliaminika
kuwa ndiyo ingeweza kufikisha taarifa za matukio kwa urahisi na
ilisaidia kwa kiasi kikubwa hata kupatikana kwa viongozi.
Na Denis Mtima/GPL
Comments
Post a Comment