Posts

Wezi Watokomea na Mashine ya ATM Ikiwa na Pesa

Image
NAIROBI: Polisi jijini Nairobi nchini Kenya wamemkamata mlinzi wa Benki ya Equity kuhusiana na tukio la wizi lililotokea Jumamosi iliyopita ambapo watu wanaoaminika kuwa ni wezi waliiba mashine ya kielektroniki ya kutolea pesa, Automatic Teller Machine (ATM) pamoja na pesa taslim ambazo hazijafahamika kiasi chake. Wezi hao walichimba ukuta wa nyuma wa Benki hiyo na kutoweka na sanduku la uhifadhi wa pesa pamoja na mtambo wa ATM, pesa zikiwa ndani. Wakati wakitekeleza tukio hilo, washukiwa waliweza kuzima kamera za CCTV na pia kengele ya usalama kabla ya kutekeleza adhma yao ya kuiba mashine na pesa hizo. Akizungumza na wanahabari, Kamanda wa Polisi wa Jimbo la Nairobi, Japheth Koome amesema kwamba polisi waliweza kupata mitungi ya gesi na vifaa vingine ambavyo hutumuka kukata chuma. Alipoulizwa kama wezi siku hizi wamepata maarifa na mbinu nyingi kama wacheza filamu, alisema kwamba kwa siku za hivi karibuni matukio ya wizi kwenye mabenki yanazidi kuongezeka na

SAKATA LA DIVA NA JOKATE KIDOTI KWA ALI KIBA,MAPYA YAIBUKA,GIGY MONEY AFUNGUKA

Image
Mwanadada Diva aliweza ku tweet kuhusiana na uwezo wa alikiba katika kuimba na kumalizia kuwa “Girlfriend anakutia gundu” kitu ambacho wengi walijiuliza inamaana Jokate (Kama inavyo julikana kuwa ndiye wa Kiba) kuwa anamtia gundu? Leo Mrembo Gigy_Money amejitokeaza na kupost picha hii hapa chini na kuandika maneno ya kumtetea Jokate: "Honestly jojo wangu mtoto classic uyu 😍wache waseme unagundu ila mwisho wa siku watakuelewa tu kwa mafanikio yako hadi unafikia umri wao yani we utakua Michael Jackson wa kike unajituma mwaya #USIFORCETUFANANE #HATUFANANI" Gigy Mone y

Makonda Kujenga Vituo 20 Vya Kisasa Vya Polisi Dar

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na wananchi Kituo cha Polisi cha Tandika, Dar. ..Maongezi yakiendelea katika Kituo cha Polisi cha Tandika. Makonda akizungumza na mmoja wa mahabusu alipotembelea vituo vya polisi.   Kituo cha Polisi Kigogo, Dar. Muonekano wa Kituo cha Polisi Traffic Mwenge, Dar. Tangu kuteuliwa kwake kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekuwa akipokea malalamiko ya wananchi na taarifa za changamoto zifuatazo kuhusu hali ya huduma za kipolisi mkoani kwake;- 1. Wananchi kutokupatiwa huduma kwa saa 24 kutokana na vituo hivyo kufungwa usiku. 2. Mazingira mabovu na yasiyoridhisha ya vituo vya polisi. 3. Polisi kutofika kwenye matukio kwa wakati pindi wapigiwapo simu na wananchi. 4. Polisi kushindwa kutoa huduma kutokana na upungufu wa askari polisi. 5. Majambazi kuvamia vituo vya polisi wakiwa na lengo la kuchukua silaha. Changamoto hizi za msingi na ambazo zinahatarisha uhakika wa usalama wa raia wa Dar es

ALICHO ANDIKA MBUNGE TUNDU LISSU KUHUSU KIFO CHA SAMMUEL SITTA

Image

YANAYOENDELEA KUJIRI NYUMBANI KWA MAREHEMU SAMUEL SITTA

Image
 Mwenyekiti  wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida akisaini kitabu cha maombolezo, wakati alipofika nyumbani kwa Marehemu Mh. Samuel Sitta aliekuwa Spika wa Bunge na Waziri Mwandamizi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliefariki leo Novemba 7, 2016 huko nchini Ujerumani. Msiba upo Nyumbani kwa Marehemu, Masaki jijini Dar es salaam.  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda (wa pili kulia) akiwa katika mazungumzo na baadhi ya viongozi pamoja ndugu wa Marehemu Mh. Samuel Sitta aliekuwa Spika wa Bunge na Waziri Mwandamizi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliefariki leo Novemba 7, 2016 huko nchini Ujerumani. Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge akisaini kitabu cha Maombolezo cha aliekuwa Spika wa Bunge na Waziri Mwandamizi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliefariki leo Novemba 7, 2016 huko nchini Ujerumani. Sehemu ya ndugu wa Marehemu wakiwa nyumbani hapo.

Rais Magufuli Atuma Salamu za Rambirambi Kufuatia Kifo cha Samwel Sitta samwel-sittaaRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai kufuatia kifo cha Spika Mstaafu na Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Urambo lililopo Mkoani Tabora Mhe. Samwel Sitta. Mhe. Samwel Sitta amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Technical University of Munich nchini Ujerumani alikokuwa akipatiwa matibabu tangu mwezi uliopita. Katika salamu hizo, Rais Magufuli amesema amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mhe. Samwel Sitta na kwamba Taifa limempoteza mtu muhimu aliyetoa mchango mkubwa katika uongozi na maendeleo. “Nitamkumbuka Mzee Sitta kwa uchapakazi wake, uzalendo wake na tabia yake ya kusimamia ukweli katika kipindi chote alichokuwa kiongozi katika ngazi mbalimbali za siasa na Serikali. “Kupitia kwako Mhe. Spika naomba kutoa pole nyingi kwa Mke wa Marehemu Mhe. Magreth Sitta ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Urambo na familia nzima ya marehemu, Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wananchi wa Urambo Mkoani Tabora na watu wote walioguswa na msiba huu” amesema Rais Magufuli katika salamu hizo. Dkt. Magufuli amesema anaungana na wafiwa wote katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo na amewaombea moyo wa uvumilivu na ustahimilivu. “Namuomba Mwenyezi Mungu aiweke roho ya Marehemu mahali pema peponi, Ameni” Gerson Msigwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU Dar es Salaam 07 Novemba, 2016

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai kufuatia kifo cha Spika Mstaafu na Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Urambo lililopo Mkoani Tabora Mhe. Samwel Sitta.   Mhe. Samwel Sitta amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Technical University of Munich nchini Ujerumani alikokuwa akipatiwa matibabu tangu mwezi uliopita.   Katika salamu hizo, Rais Magufuli amesema amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mhe. Samwel Sitta na kwamba Taifa limempoteza mtu muhimu aliyetoa mchango mkubwa katika uongozi na maendeleo.   “Nitamkumbuka Mzee Sitta kwa uchapakazi wake, uzalendo wake na tabia yake ya kusimamia ukweli katika kipindi chote alichokuwa kiongozi katika ngazi mbalimbali za siasa na Serikali.   “Kupitia kwako Mhe. Spika naomba kutoa pole nyingi kwa Mke wa Marehemu Mhe. Magreth Sitta ambaye ni Mbunge wa Jimb

Tanzia: Spika Samwel Sitta Afariki Dunia

Image
  DAR ES SALAAM : Spika wa Bunge la Tisa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mstaafu, Samuel Sitta (74) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo wakati akipatiwa matibabu nchini Ujerumani. Mtoto wa marehemu, Benjamin Sitta amesema baba yake amefariki saa 10:00 usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Technical University of Munich nchini Ujerumani. ‘’Nikweli mzee amefariki nchini Ujerumani akiwa anapatiwa matibabu, alipelekwa Alhamisi iliyopita na alikuwa anasumbulia na saratani ya tezi dume ambayo ilisambaa na kuathiri miguu na mwili mzima. Benjamin amesema kuwa taarifa za mipango ya kusafirisha mwili zitatolewa baadaye. Sitta aliyezaliwa Desemba 18, 1942, alikuwa Spika wa Bunge tangu mwaka 2005 baada ya kustaafu kwa aliyekuwa spika wa Bunge hilo, Pius Msekwa, hadi mwaka 2010 na pia Mbunge wa Jimbo la Urambo Mashariki, Tabora. Mwaka 2010, aliteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki cheo alichokitumikia hadi hadi mwaka 201

Afrima Awards: Diamond Platnumz Anyakua Tuzo 3

Image
Lagos, Nigeria: Diamond Platnumz ameibuka na ushindi wa nguvu kwenye tuzo za Afrima 2016 zilizotolewa Jumapili hii jijini Lagos, Nigeria. Muimbaji huyo ameshinda tuzo tatu, Song of The Year – Utanipenda, Best Artist/Duo/Song Of The Year Utanipenda na Best Male Artist in Eastern Africa. Pamoja na ushindi huo, Diamond pia alitumbuiza wimbo alioimba na Papa Wemba, msanii aliyetunukiwa tuzo ya heshima. Wasanii wengine waliotumbuiza ni pamoja na Patoranking, P-Square, Falz, Eddy Kenzo, Avril, Simi, Darey, Phyno, Seyi Shay na wengine. Chini ni orodha ya washindi kwenye tuzo hizo pamoja na picha za ndani ya ukumbi na red carpet: Artist of the Year  Wizkid Song of The Year Utanipenda – Diamond Album of the Year Ahmed Soultan Revelation of the year Falz Video of the Year Dogo Yaro – Vvip Best African Collaboration Eddy Kenzo ft Niniola – Mbilo Mbilo (Remix) Best African Group VVip Best African Jazz Jimmy Dludlu Best Artist/Duo/Song Of The Year  Diamond –

Listi Ya Wasanii Watakao Kinukisha Jukwaa La Fiesta, Dar leo

Image
Staa kutoka Nigeria, Yemi Alade. Mkali wa ngoma ya Wash, Where, Dulo kutoka Nigeria, Tekno Miles. Staa wa Bongo Fleva, Ali Kiba. Msanii wa Bongo Fleva, Darassa. Maua Sama. Jux. Baraka The Prince . Shilole. Roma. Vanessa Mdee . Raymond. Sholo Mwamba . Snura . Man Fongo . Fiesta 2016 kwa kishindo cha Tigo leo viwanja vya Leaders manispaa ya kinondoni jijini Dar es salaam, jukwaa litashereheshwa na orodha ifuatayo kwa wasanii kutoka hapa nyumbani. Ni pamoja na Alikiba, Baraka The Prince, Barnaba, Bell 9, Billnas, Chege, Christian Bella, Darassa, Dogo Janja, Fid-Q, Hamadai, Jay Moe, Juma Nature, Jux, Lord Eyez, Man Fongo, Maua Sama, Mr Blue, Msami, Nandy, Raymond, Roma, Shilole, Sholo Mwamba, Snura, Stamina, Vanessa Mdee, Weusi na Young Dee. Jukwaa pia litashereheshwa na wasanii kutoka nje ya Tanzania, ni pamoja na Jose Chameleon kutoka Uganda, Tekno Miles na Yemi Alade kutoka Nigeria. Fiesta 2016 Imooooo! Kwa tiketi

MWANAMKE ALIYEKAA SIKU NZIMA KWENYE JENEZA ILI KUPATA UZOEFU WA KIFO

Image
Imetokea nchini Brazil na Mwanamke  anayeitwa Vera Lucia da Silva na umri wake ni miaka 44 ambapo aliamua kukaa kwenye jeneza siku nzima ili apate uzoefu wa mazingira ya kifo ili siku akifa asiwe mgeni na Jeneza. Vera aliamua kukaa kwenye jeneza huku familia yake ikifanya vitu vinayofanywa kwenye msiba ili aone inakuaje ambapo baada ya kutoka humo alisema ilikua siku nzuri zaidi kwenye maisha yake yote. Sherehe hiyo ya kujifunza maisha ya kwenye Jeneza ambayo ilifanyika Jumatano ya November 2 2016 ni sherehe ambayo ilifanyika kwenye eneo la makaburi.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AMEONGOZA MATEMBEZI YA HISANI KWA AJILI YA KUSOMESHA WAUGUZI WAKUNGA

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki mazoezi ya viungo kabla ya kuanza kwa Matembezi ya Hisani kwa ajili ya kuchangia fedha za Mafunzo ya Wauguzi Wakunga kwenye viwanja vya Green Ground ,Oysterbay jijini Dar es Salaam  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki mazoezi ya viungo pamoja na umati uliojitokeza kabla ya kuanza kwa Matembezi ya Hisani kwa ajili ya kuchangia fedha za Mafunzo ya Wauguzi Wakunga kwenye viwanja vya Green Ground ,Oysterbay jijini Dar es Salaam  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) akiongoza Matembezi ya Hisani kwa ajili ya kuchangia fedha za Mafunzo ya Wauguzi Wakunga ambapo alitembea kwa kilometa 4.3 kuanzia viwanja vya Green Ground na kupitia barabara ya Toure na kurejea na barabara ya Msasani ,Oysterbay jijini Dar es Salaam wengine pichani ni Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto Mhe. Umm

Polisi Dar Yaeleza kwa Nini Hawajamkamata Tundu Lissu

Image
DAR ES SALAAM: Jana, Novemba 4, 2016 iliripotiwa kwenye vyombo vya habari kwamba Mbunge na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu anatakiwa kukamatwa kwa amri ya Mahakama baada ya kutotimiza masharti ya Mahakama kwa kutohudhuria kwenye kesi yake inayomkabili Kisutu, Dar. Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kupitia kwa Kamishna wake Simon Sirro imesema sababu za kwanini Tundu Lissu hajakamatwa mpaka sasa ni kutokana na Polisi kutopokea hati yoyote kutoka Mahakamani Kisutu inayoagiza kukamatwa kwa Tundu Lissu lakini ikiwafikia tu watafanya hivyo.

Hatimaye Bunge Lapitisha Mswada Sheria ya Huduma za Habari

Image
Hatimaye mchana huu wabunge wamepitisha bungeni muswada wa sheria ya huduma za habari wa mwaka 2016 uliojadiliwa kwa siku mbili. Mswada huo uliwasilishwa bungeni jana mjini Dodoma na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kisha wabunge wakaanza kuujadili. Picha na Edwin Mjwahuzi

MWAKILISHI WA SHIRIKA LA MAENDELEO LA UMOJA WA MATAIFA (UNDP) ATEMBELEA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

Image
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva akimkabidhi Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka 2015, Kiongozi wa Timu ya Tathmini ya Mradi wa Ukuzaji wa Demokrasia wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Tanzania, Sue Nelson, wakati kiongozi huyo alipotembelea Ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Kamishna wa Tume Mhe. Jaji Mary Longway.  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mst. Damian Lubuva (kushoto katikati) akimueleza jambo mgeni wake ambaye ni Kiongozi wa Timu ya Tathmini ya Mradi wa Ukuzaji wa Demokrasia wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Tanzania, Sue Nelson (kulia) wakati mgeni huyo alipotembelea Ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Kamishna wa Tume Mhe. Jaji Mary Longway.  Kiongozi wa Timu ya Tathmini ya Mradi wa Ukuzaji wa Demokrasia wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Tanzania, Sue Nelson (kulia) akimueleza jambo Mwenyekiti wa Tume y