Posts

SIRI NZITO YAFICHUKA MTANZANIA ALIYEWEKWA REHANI PAKISTAN,MKE AHAMISHWA NA JUMA,APANGIWA NYUMBA

Image
NI mateso. Ndivyo unavyoweza kusema, hasa baada ya kundi la maharamia linalojishughulisha na bishara ya ‘unga’ nchini Pakistan kuelezwa kumtesa kijana Mtanzania, Adamu Akida. Kutokana na hali hiyo, timu ya MTANZANIA ilipiga kambi jana katika eneo la Magomeni, Mtaa wa Idrissa, ambako pamoja na mambo mengine, ilifanikiwa kuzungumza na kaka wa Adamu aliyejitambulisha kwa jina la Hemed Abdallah (si jina lake halisi). Akisimulia mkasa huo, alisema miezi minane iliyopita, Adamu alikwenda kwa kaka yake ambaye ni mtoto wa mama yake mdogo aliyetambulika kwa jina la Juma, na kuomba msaada wa mtaji kwani kazi yake ya kinyozi haikuwa ikilipa na hali ya maisha ilikuwa ngumu. Baada ya kueleza shida yake hiyo, kaka yake huyo (Juma) alimuhoji kama yupo tayari kwa ajili ya kutafuta maisha nje ya nchi, na Adamu alikubali kufanya kazi ya aina yoyote ili mradi aweze kupata pesa. “Adamu kwa sasa ameshikiliwa kwa muda wa miezi minane, hatujui kama alikuwa ameingia katika janga hili ha

Binti miaka 8 afanyiwa ukatili wa kutisha!

Image
Mtoto Mariam aliyezibwa uso. Na Issa Mnally, UWAZI DAR ES SALAAM: Mtoto aliyejulikana kwa jina moja la Mariam (10), mkazi wa Mavurunza ‘A’ Kimara King’ong’o, Dar yupo katika mateso makubwa kufuatia vitendo vya ukatili na unyanyasaji anavyofanyiwa na mwanamke anayedaiwa kuwa ni mama yake mzazi aitwaye Aisha.   Akionesha sehemu ya shingo alivyokwaruzwa kwa kucha. Kwa mujibu wa majirani, mtoto huyo ambaye hata mahudhurio yake shuleni si mazuri, amekuwa katika mateso hayo ya kupigwa mpaka kujeruhiwa kwa muda mrefu lakini majirani walikuwa wakishindwa jinsi ya kumnasua kuzingatia kuwa, anayedaiwa kufanya vitendo hivyo ni mama yake. Hivi karibuni, majirani wa eneo hilo wakishirikiana na Mjumbe wa Shina Namba 063, Mavurunza ‘A’ Kwa Kichwa, Janet Moshi waliamua kumwokoa mtoto huyo baada ya kufukuzwa nyumbani na mama yake huyo majira ya saa 4:30 usiku bila kuwa na sehemu ya kwenda. “Ilikuwa saa nne na nusu usiku, sisi tulikuwa tumekaa kule mbele tukipata moj

Wanafunzi 7,800 waliofukuzwa UDOM ni 382 tu wenye sifa – Prof. Ndalichako

Image
Serikali imetangaza orodha ya wanafunzi ambao watarejea kuendelea na masomo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) baada ya uchambuzi kumalizika na kupatikana idadi ya wanafunzi ambao wana sifa za kuendelea na masomo. Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako alisema kuwa kwa kipindi chote walikuwa wakifanya uchambuzi ili kuona ni wanafunzi gani walikuwa na sifa za kusoma kozi hiyo maalum ambayo ilianzishwa kutokana na tatizo la walimu wa Sayansi. Alisema kuwa programu hiyo ilikuwa inahitaji walimu ambao watakwenda kufundisha shule za sekondari lakini kulikuwa na wanafunzi 1,210 ambao walikuwa wanachukua stashahada ya ualimu wa shule za msingi ambao ni kinyume na malengo na 6,595 wakichukua stashahada ya kufundisha shule za sekondari. “Baada ya hatua ya kuwaondoa wanafunzi chuoni kuchukuliwa, serikali ilifanya uchambuzi wa wanafunzi hao kwa lengo la kujiridhisha na sifa zao. Sifa zilizotakiwa ni ufaulu wa daraja

RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA MAAFISA WA JESHI LA POLISI WALIOPANDISHWA VYEO IKULU JIJINI DAR ES SALAAM,AWATAKA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA WANAOLETA MATATIZO

Image
Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Ahmada Abdalla Khamis akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kula kiapo cha ahadi ya uadilifu Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Jeshi la Polisi waliopandishwa vyeo vya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) na Naibu Kamishna wa Polisi DCP mara baada ya kula kiapo cha ahadi ya uadilifu Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Jeshi la Polisi waliopandishwa cheo cha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) mara baada ya kula kiapo cha Maadili ya Watumishi wa umma Ikulu jijini Dar es Salaam Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwagaia vitafunwa wageni mbalimbali waliofika Ikulu kwa ajili ya kushuhudia Maafisa wa Polisi walipondishwa vyeo wakati wakil

'Ni vizuri mwanaume, amfiche mkewe vipato vyake’

Image
  Ukipata bahati ya kukaa kwenye vijiwe vingi vya wanaume, kauli za ‘mwanamke usimueleze kila kitu’ huwa zinatawala. Wanaambizana kwamba ili uhusiano udumu, usimueleze kila kitu mwanamke. Wanasema mfiche asijue kila kitu. Taswira hiyo imeanza kama utani lakini pengine kadiri siku zilivyokuwa zinazidi kusonga mbele, sasa inakuwa kama sheria. Wanaume wanasambaziana mbinu hiyo ili kukabiliana na wanawake zao. Wanaona ni bora kuwaficha baadhi mambo ili mambo yaende vizuri. Mwanaume anaamini akimficha baadhi ya vitu mkewe, inasaidia kumfanya aishi kwa amani. Hataki kumueleza kila kitu kinachomhusu kwani anaamini uwezo wake wa kukabiliana na mambo hauwezi kuwa sawa na yeye hivyo bora amfiche. Hali hiyo haikuja hivihivi, imetokana na visa mbalimbali wanavyokutana navyo katika uhusiano. Wanafikia hatua ya kuwafananisha wanawake na watoto. Kwamba hata kama mwanaume hana fedha, hapaswi kumueleza mwanamke kuwa hana fedha. Kwamba mwanamke usimueleze vyanzo vyote

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU KUMWAKILISHA RAIS MAGUFULI RWANDA KATIKA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI WANACHAMA WA UMOJA WA AFRIKA

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN ataondoka nchini kesho jumamosi kwenda KIGALI nchini Rwanda kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 27 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU). Makamu wa Rais atamwakilisha Rais Dkt JOHN MAGUFULI katika Mkutano huo wa siku MBILI ambao unatarajiwa kufanyika KIGALI – RWANDA kuanzia Julai 17-18 mwaka huu. Katika Msafara wake, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN atafuatana na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kikanda na Kimataifa Balozi AUGUSTINE MAHIGA na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Zanzibar Issa Haji Ussi. Mkutano huo ambao utahudhuriwa na Makamu wa Rais utaanza kwa vikao vya ndani ambapo viongozi watajikita katika kujadili masuala ya kimkakati ikiwemo umuhimu wa kuliunganisha Bara la Afrika kibiashara kwa kuwa na soko la biashara huria ifikapo mwaka 2017 pamoja na mageuzi katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Aidha Waju

TANZANIA YAFANYA UPASUAJI WA KIHISTORIA,YAWEKA BETRI KWENYE MOYO

Image
Na John Stephen, MNH Dar es Salaam, Tanzania.Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)-Muhimbili LEO imefanya upasuaji mkubwa wa moyo kwa mtoto, Happiness John Josephat ambaye amepandikizwa peacemaker (betri ya umeme wa moyo) kwenye mfumo wa moyo wake. Mmoja wa madaktari wa moyo walioshiriki kwenye upasuaji huo, Dk Godwin Sharau wa taasisi hiyo amesema upasuaji huo umechukua saa moja na kwamba mtoto anaendelea vuzuri. Dk Sharau amesema mtoto huyo amepandikizwa peacemaker (betri ya umeme wa moyo) ambayo itasaidia kuunganisha mishipa ya fahamu ya umeme wa moyo ambayo inaunganisha vyumba vya moyo vya juu na chini kwenye moyo wa binadamu. “Upasuaji huu ni wa kwanza kufanyika Tanzania. Upasuaji kama huu unafanyika kwa watu wazima, lakini watu wazima hawahitaji upasuaji wa moyo wa kupandikiza. Watoto wanahitaji upasuaji wa moyo wa kuipandikiza. “Tatizo la mtoto huyu ni la kuzaliwa. Na ni nadra kutokea. Inaweza kupita miaka mingi bila watoto kutokea tatizo kama hilo.

STEVE NYERERE AIZUNGUMZIA ISSUE YA KUKOSA U DC ,AELEZA MENGI

Image
Baada ya madai kuwa msanii wa filamu, Steve Nyerere alikuwa na matumaini ya kuteuliwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli katika uteuzi wa wakuu wa wilaya (ma-DC) wapya, staa huyo wa filamu amefunguka na kuzungumzia issue hiyo. Steve Nyerere Steve Nyerere amesema yeye ni mmoja kati ya watu ambao walikuwa wanasubiria uteuzi wa ma- DC na hajajisikia vibaya kukosa kwa kuwa ana imani bado Magufuli anamwangalia. “Mtu kama upo smart kwanini usisubirie nafasi kama hizo, mimi ni mtu safi na kazi naiweza,” alisema Steve. Aliongeza, “Uteuzi nimeusikia, tuombe mungu kama akinifikiria kwa awamu nyingine sio mbaya, tena ningependa Kinondoni, ni sehemu ambayo naona naweza kuifanyia kazi vizuri kwa sababu hata kwenye nafasi za ubunge nilishika nafasi yatatu, kwa hiyo kama ningepata Kinondoni ingekuwa poa zaidi” Mwigizaji huyo ni mmoka kati ya wasanii ambao walikuwa katika team ya kampeni ya Magufuli katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2016.

Njombe kidedea Kampeni ya Usafi, yatwaa Toyota Land Cruiser

Image
         Waziri wa afya, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akisoma hotuba katika hafla hiyo. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda,  akiwakabidhi cheti baadhi ya wawakilishi kutoka halmashauri zao. …Akiendelea kukabidhi vyeti vya ushindi. …Akikabidhi kombe kwa mmoja wa wakilishi wa halmashauri hizo. Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya akiwakabidhi kombe wawakilishi wa halmashauri zao. Baadhi ya wawakilishi kutoka mikoa mbalimbali wakipita mbele kupewa mkono wa hongera. Waziri Mwalimu (kushoto) akiwa na baadhi ya wawakilishi wa Halmashauri ya Mkoa wa Njombe. Baadhi ya pikipiki zilizotolewa kwa halmashauri zilizoibuka kidedea kwa usafi. Mwalimu (mwenye kilemba kichwani) akishuhudia gari la ushindi lililotolewa Njombe. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Njombe, Valentino Aidani,  akiwa ndani ya gari walilojishindia. Gari la ushindi wa Halimashauri ya Njombe. HALMASHAURI ya Mkoa wa Njombe leo imeimbuka kidedea na kutwaa gari aina ya  ‘Toyota La

Nafasi 500 za Udereva Kutoka UDA

Image
Uongozi wa UDA Management Agency Limited unatangaza kazi za Madereva 500 wenye leseni daraja “C” na uzoefu wa kuendesha mabasi ya abiria kwa miaka kuanzia 2 na kuendelea. Maombi yawasilishwe kwa Charles Nzilankoma -Operations Manager 0763 600 376 au kwa Cyprian Malekela 0754 266 029 kwa Usaili wa awali.

WAKURUGENZI WA HALMASHAURI ZA MAJIJI, MANISPAA,MIJI NA WILAYA WALA KIAPO CHA AHADI YA UADILIFU KWA VIONGOZI WA UMMA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa,Miji na Wilaya walioteuliwa hivi karibuni na kuwataka kuwatumikia wananchi ikiwemo kuondoa kero zinazowakili wananchi katika maeneo yao kama utitiri wa kodi hasa kwenye bidhaa wanazozalisha.Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mh. Angella Kairuku na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan. wakati wa hafla ya kula kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma kwa wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa,Miji na Wilaya walioteuliwa hivi karibuni.Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan akiongea na wakurugenzi wa Halmashauri za Majiji, Manispaa,Miji na Wilaya (Hawapo pichani) walioteuliwa hivi karibuni na kusisitiza kwenye matumizi ya Kanuni, Sheria na Taratibu katika kutimiza majukumu y