RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA MAAFISA WA JESHI LA POLISI WALIOPANDISHWA VYEO IKULU JIJINI DAR ES SALAAM,AWATAKA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA WANAOLETA MATATIZO
Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Ahmada Abdalla Khamis akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kula kiapo cha ahadi ya uadilifu Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Jeshi la Polisi waliopandishwa vyeo vya Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) na Naibu Kamishna wa Polisi DCP mara baada ya kula kiapo cha ahadi ya uadilifu Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Jeshi la Polisi waliopandishwa cheo cha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) mara baada ya kula kiapo cha Maadili ya Watumishi wa umma Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwagaia vitafunwa wageni mbalimbali waliofika Ikulu kwa ajili ya kushuhudia Maafisa wa Polisi walipondishwa vyeo wakati wakila kiapo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwagaia vitafunwa baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria tukio hilo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaagiza
viongozi wa Jeshi la Polisi Tanzania kuwaondoa watumishi wote wasiokuwa
askari polisi na ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya ukiukwaji
wa taratibu na ufujaji wa fedha za umma ili kulinda heshima, nidhamu na
uadilifu ndani ya jeshi hilo.
Rais
Magufuli ametoa maelekezo hayo leo tarehe 18 Julai, 2016 muda mfupi
baada ya Naibu Makamishna wa Polisi 25 na Makamishna Wasaidizi
Waandamizi wa Polisi 35 kula kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma,
Ikulu Jijini Dar es salaam.
Pamoja na kutoa agizo la kutaka
wasio askari polisi kuondolewa katika utumishi wa jeshi la polisi, Rais
Magufuli pia ameagiza jeshi hilo lichukue hatua dhidi ya wote
wanaokabiliwa na tuhuma za wizi wa fedha wakiwemo wanaodaiwa kuiba
mabilioni ya shilingi zilizotolewa kwa ajili ya ununuzi wa sare za
askari mwaka jana 2015.
"Mnajua kupeleleza, mna vyombo vyote, ofisi ya IGP (Inspekta Jenerali wa Polisi)ipo palepale, ofisi ya DCI (Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai) ipo palepale, Makamishna wote mnazunguka mnakwenda palepale, mwizi mnae palepale, mnashindwa kumshika.
"Kama mnafikiri kuwa na raia
katika jeshi la polisi wanawaharibia kazi zenu hamisheni raia wote na
wapelekeni utumishi, kwani hakuna mhasibu ambaye ni askari polisi?
hakuna mhandisi ambaye ni askari polisi? hakuna afisa tawala ambaye ni
askari polisi? Mimi nafikiri kama matatizo ya wizi na wafanyakazi hewa
yanaletwa na raia waliomo ndani ya jeshi la polisi na majeshi yetu
mengine, IGP kaorodheshe raia wote wanafanya kazi Jeshi la Polisi ili
waondolewe na tuwapangie kazi nyingine uraiani" Amesema Rais Magufuli.
Hata hivyo Rais Magufuli
amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kazi nzuri linayofanya iliyoliwezesha
kujenga imani kubwa kwa watanzania na ametaka viongozi wa Jeshi hilo
wawaongoze askari walio chini yao vizuri, wawatie moyo na waache vitendo
vya kuwakatisha tamaa kwa kuwaadhibu ama kuwatisha pale wanapochukua
hatua stahiki dhidi watu wanaovunja sheria.
"Sasa mimi niwaombe nyinyi,
wale wadogo mnaowaongoza mkawape mamlaka ya kutimiza wajibu wao, hata
kama ameshika gari la IGP liache lishikwe IGP atakwenda kujieleza
mwenyewe, hata akishika gari la RPC afanye hivyohivyo, hata akishika
gari la Waziri au gari la Rais mwacheni atekeleze wajibu wake, sheria ni
msumeno, tunawanyima nguvu hawa wa chini wanapotimiza wajibu wao kwa
mujibu wa sheria halafu unamwambia liachie, ukifanya hivyo aliyeshikwa
anatoka pale akiwa anatamba kwelikweli na yule askari unamvunja nguvu ya
kufanya kazi"Amesisitiza Rais Magufuli.
Rais Magufuli pia amelitaka jeshi
hilo kuungana na vyombo vingine vya serikali katika kutekeleza shughuli
zake zikiwemo kusimamia ukusanyaji wa mapato ya serikali bandarini,
katika sekta ya utalii na maeneo mengine, kukabiliana na vitendo vya
rushwa na kuondoa watumishi hewa.
Tukio hili la Naibu Makamishna wa
Polisi na Makamishna Wasaidizi Waandamizi wa Polisi kula kiapo cha
uadilifu kwa viongozi wa umma limeongozwa na Kamishna wa Maadili Jaji
Mstaafu Salome Kaganda na limehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba, Waziri wa
Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Anjellah Kairuki, Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Hamad Yusuf Masauni, Mwanasheria
Mkuu wa Serikali Mhe. George Mcheche Masaju, Makatibu Wakuu na Viongozi
wa vyombo vya Ulinzi na Usalama.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
18 Julai, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Maafisa wa Jeshi la polisi aliowapandisha vyeo vya Naibu Kamishna wa Polisi DCP na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ikulu jijini Dar es Salaam.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Kedmon Andrew Mnubi akila kiapo cha Ahadi ya uadilifu pamoja na Maafisa wengine wa Jeshi la Polisi Ikulu jijini Dar es Salaam.
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Mwamini Marco Rwantale akila kiapo cha Ahadi ya uadilifu pamoja na Maafisa wengine wa Jeshi la Polisi Ikulu jijini Dar es Salaam.
Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Ahmada Abdalla Khamis akisaini hati ya kiapo cha Ahadi ya Uadilifu Ikulu jijini Dar es Salaam.
Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Frasser Rweyemamu Kashai akisaini hati hati ya kiapo cha Ahadi ya Uadilifu Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwagaia vitafunwa baadhi ya Maafisa mbalimbali wa Polisi waliokula kiapo cha Maadili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mwigulu Nchemba akizungumza jambo na Naibu wake Hamadi Masauni mara baada ya Maafisa wa Jeshi la Polisi waliopandishwa vyeo kula Kiapo ahadi ya uadilifu Ikulu jijini Dar es Salaam.PICHA NA IKULU.
Comments
Post a Comment