Njombe kidedea Kampeni ya Usafi, yatwaa Toyota Land Cruiser
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akiwakabidhi cheti baadhi ya wawakilishi kutoka halmashauri zao.
HALMASHAURI ya Mkoa wa Njombe
leo imeimbuka kidedea na kutwaa gari aina ya ‘Toyota Land Cruiser’ na
pikipiki baada ya kutangazwa mshindi katika Kampeni ya Kitaifa ya Usafi
wa Mazingira ulioanza mwaka jana.
Halmashauri hiyo imeibuka kidedea leo
katika hafla fupi iliyofanyika Katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu
Julius Nyerere jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri
wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt.
Mpoki Ulisubisya ambao walikabidhi zawadi za medali na vyeti vya
ushindi.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mwalimu
amesema kuwa tangu kampeni hiyo ya kufanya usafi kuzinduliwa na Rais
John Pombe Magufuli, wananchi kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa kuwa
mabalozi wazuri katika kuhakikisha mazingira wanayoishi yapo safi na
kuhimizana kuendelea na usafi wa mazingira kuepukana na ugonjwa wa
kipindupindu na kuishi kwenye mazingira ya kuvutia.
Aidha aliziasa halmshauri zote nchini
kuhakikisha zinaiga mfano kutoka Halmashauri ya Njombe iliyoibuka
kidedea ili ziweze kuwa miongoni mwa washindi wa zawadi nyingine.
Halmashauri ya Njombe iliibuka kidedea
katika nyanja mbalimbali za vigezo vilivyokuwa vikizingatiwa ikiwemo
mitaa zao za mkoa huo.
Kwa upande wa halmashauri za miji
zilizoibuka kidedea ni Halmashauri ya Mbeya na ya Kinondoni huku kwa
upande wa manispaa ni Iringa, Moshi na Mpanda.
NA DENIS MTIMA/GPL
Comments
Post a Comment