MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU KUMWAKILISHA RAIS MAGUFULI RWANDA KATIKA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI WANACHAMA WA UMOJA WA AFRIKA
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN ataondoka
nchini kesho jumamosi kwenda KIGALI nchini Rwanda kwa ajili ya
kuhudhuria Mkutano wa 27 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika
(AU).Makamu
wa Rais atamwakilisha Rais Dkt JOHN MAGUFULI katika Mkutano huo wa siku
MBILI ambao unatarajiwa kufanyika KIGALI – RWANDA kuanzia Julai 17-18
mwaka huu.Katika
Msafara wake, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA
SULUHU HASSAN atafuatana na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa
Afrika Mashariki,Kikanda na Kimataifa Balozi AUGUSTINE MAHIGA na Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais Zanzibar Issa Haji Ussi.
Mkutano
huo ambao utahudhuriwa na Makamu wa Rais utaanza kwa vikao vya ndani
ambapo viongozi watajikita katika kujadili masuala ya kimkakati ikiwemo
umuhimu wa kuliunganisha Bara la Afrika kibiashara kwa kuwa na soko la
biashara huria ifikapo mwaka 2017 pamoja na mageuzi katika Baraza la
Usalama la Umoja wa Mataifa.
Aidha
Wajumbe wa mkutano huo wa 27 wa AU pia watachagua Mwenyekiti wa
Kamisheni ya Umoja wa Afrika pamoja na Makamu wake, Makamishna WANANE wa
sekta mbalimbali na Majaji WANNE wa Mahakama ya Afrika ya Haki za
Binadamu pamoja na na kupitisha mapendekezo kuhusu gharama za uendeshaji
wa umoja huo na bajeti ya fedha ya mwaka 2017.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN na Ujumbe
wake wanatarajia kurejea nchini Julai 19 mwaka huu baada ya kumalizika
kwa Mkutano huo wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU)
KIGALI nchini RWANDA.
Comments
Post a Comment