TANZANIA YAFANYA UPASUAJI WA KIHISTORIA,YAWEKA BETRI KWENYE MOYO
Na John Stephen, MNH
Dar es
Salaam, Tanzania.Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)-Muhimbili LEO
imefanya upasuaji mkubwa wa moyo kwa mtoto, Happiness John Josephat
ambaye amepandikizwa peacemaker (betri ya umeme wa moyo) kwenye mfumo wa
moyo wake.Mmoja
wa madaktari wa moyo walioshiriki kwenye upasuaji huo, Dk Godwin Sharau
wa taasisi hiyo amesema upasuaji huo umechukua saa moja na kwamba mtoto
anaendelea vuzuri.Dk
Sharau amesema mtoto huyo amepandikizwa peacemaker (betri ya umeme wa
moyo) ambayo itasaidia kuunganisha mishipa ya fahamu ya umeme wa moyo
ambayo inaunganisha vyumba vya moyo vya juu na chini kwenye moyo wa
binadamu.
“Upasuaji
huu ni wa kwanza kufanyika Tanzania. Upasuaji kama huu unafanyika kwa
watu wazima, lakini watu wazima hawahitaji upasuaji wa moyo wa
kupandikiza. Watoto wanahitaji upasuaji wa moyo wa kuipandikiza.
“Tatizo
la mtoto huyu ni la kuzaliwa. Na ni nadra kutokea. Inaweza kupita miaka
mingi bila watoto kutokea tatizo kama hilo. Upasuaji umefanywa kwa
ushirikiano wa madaktari wa moyo na madaktari wa matibabu ya moyo
nikiwamo mimi (Dk. Godwin Sharau), Dk Michael Valentine kutoka
Marekani, Dk Kisenge na Dk Sulende Kubhoja, Dk wa usingizi, Dk Anjelan
Muhozya na madaktari wengine ambao wamesaidia katika upasuaji
huu,” amesema Dk Godwin Sharau.
Comments
Post a Comment