Umuhimu wa maziwa mwilini
Unywaji wa maziwa unaopendekezwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) ni mtu mmoja kunywa lita 200 kwa mwaka. Tovuti za Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB) zinaonesha kuwa Mtanzania hunywa wastani wa lita 47 tu kwa mwaka. Wakati unywaji huo wa maziwa si wa kuridhisha, kiwango cha watoto wetu kudumaa bado ni kikubwa ambapo asilimia 35 hudumaa. Sababu kubwa inayofanya watoto hao kudumaa ni ukosefu wa vyakula vyenye virutubisho mwilini. Maziwa yana virutubisho vyote muhimu kwa ujenzi wa afya ya binadamu kwani yana protini ya daraja la kwanza, mafuta, madini, vitamin na sukari ya asili ya lactose na maji. Maziwa hutupatia takriban vitamini zote ambazo huyeyuka kwenye mafuta. Nazo ni vitamini A, D, E na K. Vitamini A huhusika na shughuli mbalimbali mwilini. Mfano afya bora ya ngozi zetu kuwa nyororo na ng’avu na pia kuwa na uwezo wa kuzuia wadudu wasiingie mwilini. Vile vile vitamini A hutumika pia kuyapatia macho uimara wa kuona. Na hasa kuona usiku au kwenye mwanga hafifu. Ukosefu wake hud