Trich; hushambulia sehemu nyeti za mwanamke
Ugonjwa wa Trich ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea vya jamii ya Protozoan na huathiri mrija wa kupitisha mkojo unaojulikana kama Urethra na tupu ya mwanamke Vagina . Ugonjwa huu huweza kuwapata wanaume lakini huwapata na kuonekana zaidi kwa wanawake na daktari anaweza kumuambia mgonjwa anayeugua maradhi haya kuwa ana Trichomonas Vaginalis. UNAAMBUKIZWAJE? Mwanamke au hata mwanaume anaweza kukumbwa na ugonjwa huu akifanya tendo la ndoa na mtu mwenye maambukizi bila kutumia kinga. Kwa kawaida vimelea vya Trichomonas Vaginalis ni vidogo mno ni sawa na chembechembe moja ya damu nyeupe kwa upana (10 μm) ingawa wakati mwingine ukubwa waweza kutofautiana kulingana na mazingira.Wengine huuita ugonjwa huu Trichomoniasis. Watu walio na ugonjwa wa Trich wana hatari ya kupata ugonjwa wa Ukimwi (HIV) au magonjwa mengine ya zinaa kwa sababu bakteria hawa huharibu seli aina ya Epithelium na kusababisha vidonda Microulcerations katika tishu zilizo ndani ya utupu wa mwakamke. DALILI K