Pichaz: Muhammad Ali Alivyoagwa Kiislamu
Maombi ya Kiislamu ya kuswaliwa kwa jeneza la marehemu bondia mashuhuri duniani Mohammed Ali yamefanyika katika jimbo la Kentucky, Marekani. Ali alifariki wiki iliyopita akiwa na umri wa miaka 74.
Maelfu ya watu, wakiwemo Waislamu kutoka maeneo mengi duniani, wamehudhuria swala hiyo katika ukumbi wa Freedom Hall, mjini Louisville. Swala hiyo inapeperushwa moja kwa moja kupitia runinga na Waislamu wengi duniani wanatumai kwamba itaashiria mchango mzuri kwa dini ya Kiislamu nchini Marekani.
Muhammad Ali alisilimu akiwa kijana. Alikuwa kwanza mwanachama wa madhehebu ya Nation of Islam, kundi lililotetea haki za watu weusi, lakini baadaye akakumbatia imani ya kawaida ya Kiislamu. Mazishi yake yatafanyika leo Ijumaa
Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa championi wa ngumi za kulipwa duniani, Muhammad Ali ukiwasili kwa ajili ya mazishi katika taratibu za Kiislamu huko, Louisville, Kentucky, U.S. jana June 9, 2016.
Comments
Post a Comment