Wifi wa Zari adaiwa kutimuliwa kwa Diamond
Wifi nambari moja wa Zarinah Hassan ‘Zari’, Esma Platnumz. Stori: Musa Mateja, Ijumaa Hivi karibuni yalitua madai kwenye meza ya gazeti hili yakieleza kuwa, eti yule wifi nambari moja wa Zarinah Hassan ‘Zari’ anayefahamika kwa jina la Esma Platnumz (pichani) ametimuliwa pale nyumbani kwa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’, Madale jijini Dar na sasa anaishi Tandale. Chanzo chetu ambacho kiliomba jina lake lisiandikwe gazetini kilidai kuwa, baada ya Zari kutua Bongo kabla ya kwenda Ulaya, Esma alitakiwa kufungasha kila kilicho chake na kwenda kuishi kwenye ile nyumba ya familia iliyokuwa ikikarabatiwa pale Tandale. Diamond akiwa na waubani wake, Zari. “Nyie mbona mnapitwa na ubuyu? Esma katimuliwa pale kwa Diamond, sasa hivi anaishi kule Tandale kisa ni zile figisufigisu zilizokuwa zikitokea kati yake na Zari. “Diamond ameona ili mzazi mwenzake awe na amani, anayeweza kuondolewa kwenye ule mjengo aondolewe ili amani itawale na kusiwepo manenomaneno,” kilidai chanzo