MWANASAIKOLOJIA ANT SADAKA AONGEA NA WANAWAKE WA DODOMA KWENYE MAFUNZO YA WAJASIRIAMALI YANAYOENDESHWA NA TAASISI YA MANJANO FOUNDATION
Mwanasaikolojia
Anti Sadaka akitoa Mada kwenye Mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake wa
Mkoa wa Dodoma yanayoendesha na Taasisi ya Manjano Foundation
yanaoendelea kwenye ukumbi wa LAPF House.
Mwanasaikolojia
Anti Sadaka amewafunda wanawake waDodomawanaoshiriki mafunzo ya
ujasiriamali ya kujikita katika biashara ya Vipodozi vya LuvTouch
Manjano. Mafunzo hayo yanaendeshwa na wataalamu kutoka taasisi ya
Manjano Foundation na mkufunzi wa maswala ya Biashara mjini Dodoma
yanayoendelea kwa wiki nzima.
Washiki Kutoka Mkoani Dodoma na Maeneo Jirani wakiliskiliza kwa Makini Wakati wa Mafunzo hayo Leo.
Anti
Sadaka amewataka wanawake hao kujitambua kwa lengo la kufikia malengo
yao waliojiwekea. Akieleza zaidi katika semina hiyo amewataka wanawake
hao kujitambua wao ni nani, wajiamini, watambue vyeo vyao katika
familia, wana nafasi gani kwenye jamii inayowazunguka, kufanya kazi kwa
bidii na kudumisha nidhamu yao kwa kila wakifanyacho kwa lengo la
kufikia malengo yao.
Pia amewaasa wanawake walioshiriki mafunzo hayo mjini Dodoma kuchangamkia FURSA zinazowazunguka. Semina
hiyo inawanufaisha wanawake wa Dodoma kwa lengo la kuwaongezea kipato
na pia kuweza kujiajiri ili kujikwamua na tatizo la ukosefu wa ajira.
Picha ya Pamoja Washiriki hao kutoka Mkoani Dodoma wakiwa na Mwanasaikolojia
Anti Sadaka Pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear Illusions africa na
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Manjano Foundation Mama Shekha
Nasser.
Anti Sadaka
amewashauri wanawake wasiache kujifunza na waache kujibweteka baada ya
mafunzo haya kuisha isipokuwa wawe makini kutafuta elimu zaidi ya
kujiongezea ujuzi katika kazi zao.
Comments
Post a Comment