Waziri wa Rwanda Afia Gerezani Burundi
Bujumbura, Burundi
WAZIRI
wa zamani wa Rwanda, Jacques Bihozagara amefariki katika gereza moja
nchini Burundi miezi minne baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kufanya
ujasusi.
Rwanda imesema marehemu Jacques alikuwa
ameshikiliwa kinyume cha sheria. Balozi wa Rwanda nchini Ubelgiji
ameandika na kusema kifo cha Jacques ni “mauaji”.
Wafungwa katika gereza alipokuwa
ameshikiliwa wanasema alionekana akiwa katika hali nzuri na kwamba
alifariki dakika chache baada ya kuchukuliwa kutoka gereza kupelekwa
hospitali baada ya kuugua.
Umoja wa Mataifa umekuwa ukiishutumu
Rwanda kwa kujaribu kuipindua serikali ya Rais wa Burundi Pierre
Nkurunziza, madai ambayo Rwanda imekuwa ikiyakanusha.
Comments
Post a Comment