WATANZANIA KUNUFAIKA NA BIMA YA ELIMU KUTOKA SANLAM LIFE INSURANCE TANZANIA

Meneja Mkuu wa Bima ya Maisha, Wilson Mnzava (wapili kulia), wakati wa uzinduzi wa bima hiyo.Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam Life Insurance, Julius Magabe na kulia ni Mchambuzi wa Mahesabu ya Bima wa kampuni hiyo, Kyenekiki Kyando. 
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam Life Insurance, Julius Magabe, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bima ya Elimu ya 'Sanlam Education Care,Kulia ni Meneja Mkuu wa Bima ya Maisha, Wilson Mnzava.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam Life Insurance, Julius Magabe (wapili kushoto), akimkabidhi Hati ya Bima ya Elimu wa 'Sanlam Education Care', Meneja Mkuu wa Bima ya Maisha, Wilson Mnzava (wapili kulia), wakati wa uzinduzi wa bima hiyo, Dar es Salaam leo. Kulia ni Mchambuzi wa mahesabu ya Bima wa kampuni hiyo, Kyenekiki Kyando na kushoto ni Meneja Mkuu wa Uhusiano wa Biashara, Nura Masood.

Kampuni inayoongoza kwa utoaji wa bima za maisha TanzaniaSanlam Life Insurance, leo, imezindua bima ya elimu ya kipekee inayolenga kukupa uhakika wa elimu ya mwanao.
'Bima hiyo inayoitwa “Sanlam Education Care', inawapa wazazi mpango wa akiba wa kila mwezi pamoja na faida ya bima ya maisha ambayo inalinda uwekezaji wako katika tukio la kifo au ulemavu wa kudumu. 
Afisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam Life Insurance  amesema,"kuwekeza katika elimu ya mtoto wako ni moja ya zawadi bora ambayo wazazi wanaweza kuwapatia watoto wao”. Elimu imeanza kuwa huduma ghali katika maisha ya siku hizi, kwahiyo wazazi wanashauriwa kufanya maamuzi ya busara ya uwekezaji pale linapokuja suala la ustawi wa maisha ya baadaye ya watoto wao. Sanlam Education Care ni suluhisho kamili, kwani imebuniwa kama mpango wa akiba unaowawezesha wazazi kuwa na utaratibu mahususi wa kuweka akiba ambao unazingatia kupanda kwa gharama za elimu."Hakuna huduma nyingine ya bima ya maisha inayokidhi haja ya kulinda elimu ya mtoto kama 
huduma hii ya Sanlam Education Care. ‘Kuongezeka kwa huduma ya Sanlam Education Care kwenye orodha ya bidhaa zetu' inatilia mkazo dhamira yetu ya kupanua wigo wa huduma zenye ubunifu na zinazokidhi mahitaji ya wateja wetu pamoja na kuboresha na kulinda ukwasi wao"

Comments

Popular posts from this blog