MWANZA NA ARUSHA YAONGOZA WATUMISHI HEWA.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora , Aggrey Mwanri akikabidhi majina ya watumishi hewa kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene leo jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Lindi ,Godfrey Zambi akikabidhi majina ya watumishi hewa kwa Waziri wa nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George Simbachawene leo jijini Dar es Salaam.
Wakuu
wa Mikoa na Watendaji wa TAMISEMI wakimsikiliza Waziri wa nchi Ofisi ya
Rais-TAMISEMI, George Simbachawene leo jijini Dar es Salaam. Picha na
Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.
MKOA Mwanza waongoza kuwa na watumishi hewa 334 ukifuatiwa na Mkoa wa Arusha kwa kuwa na watumishi hewa 270 ikiwa nchi nzima na watumishi hewa 2,702.
Hata hivyo Shinyanga na Songwe ni mikoa isiyo kuwa na watumishi hewa kukosekana
kwa watumishi hewa katika mkoa wa shinyanya imetokana na mikakati ya
mikoa hiyo kila idara kupeleka majina ya watu wanaostahili kulipwa
mishahara kila mwezi.
Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga, Anne Killango kuwa viongozi walioanza katika
mikoa huo walijipanga katika kuondokana na watumishi hewa.
Mkoa wa Songwe kukosekana kwa watumishi hewa kunatokana na upya wake na mkuu wake mkoa ameapishwa wiki moja iliyopita.
Akizungumza
na Wakuu wa Mikoa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George
Simbachawene aliwataka wakuu wa mikoa wafanye kazi ikiwemo ubunifu wa
miradi ya kuongeza mapato.
Simbachawene amewataka wakuu wa mikoa kuondokana na matumizi yasio na ulazima ili fedha hizo zitumike katika matumizi ya msingi.
Amesema
kuwa zoezi hilo liweze kuwa endelevu ikiwa ni pamoja na kushughulika na
watoro ambao wanalipwa fedha wakati hawafanyi kazi,
Mkuu
wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri amesema wote ambao wamehusika na
hujuma za mishahara wafikishwe katika vyombo vya dola na mkoa wake
umeanza kutekeleza
Comments
Post a Comment