Posts

Kwani ni lazima uolewe???

Image
HAKIKA sifa na utukufu zimuendee yeye Jalali ambaye ametupa nafasi ya kuweza kukutana tena siku ya leo hii.Moja ya kitu kinachonishangaza kwa wanawake wengi ni kuwa na ndoto zaidi ya kuolewa kuliko kufikia ndoto zao halisi kwa maana ya maono ambayo wamekuwa wakiyawaza kwa muda mrefu. Tabia hii ya wanawake wengi ya kutaka au kukimbilia kuolewa si jambo baya, kama ikitokea ukapata bahati hiyo ya kuolewa lakini kama haitatokea sio ishu sana bali kumbuka kuwa kuna maisha nje ya kuolewa nayo si mengine ni maisha ya kufikia ndoto zako. Kama haujaolewa Ni kweli Mungu alituumba na kutuweka duniani ili tuujaze ulimwengu lakini hata hilo la upande wa pili nalo ni la kushukuru pindi linapokukuta, linauma ila kupunguza maumivu yake ni kulikuba li na kujifunza vitu vingine vingi ili uweze kuendelea na maisha mengine. Hulka ya wanawake kuolewa imekuwa ni sehemu ya wengi wao, utamsikia binti wa miaka 16 amemaliza darasa la saba anataka kuolewa eti kisa amefeli mtihani wa mwisho,

Mafuta ya Wizi ya Diesel Yakamatwa Bandari ya Dar

Image
Jeshi la Polisi kitengo cha majini limekamata tani zipatazo 20 za mafuta ya dizeli yaliyokuwa katika Jahazi lililokuwa kando ya bandari ya Dar es Salaam likijiandaa kwa safari ya kwenda Zanzibar. Mkuu wa Kitengo hicho cha Polisi cha Wanamaji, Bw. Mboje John Kanga amesema watu watano wanashikiliwa kuhusiana na tukio hilo na uchunguzi zaidi unaendelea.

ALIKIBA NA WILDAID WATOA WIMBO KUPINGA UJANGILI WA TEMBO.

Image
 Video ya wimbo huo imerekodiwa jijini Los Angeles Marekani ambapo Alikiba alikuwa mgeni rasmi kweye hafla maalum iliyoandaliwa na shirika la uhifadhi wanyamapori la kimataifa la WildAid. Chini ya kauli mbiu “Ujangili Unatuumiza Sote”, Alikiba amefanya kazi na WildAid kuongeza uelewa wa Watanzania kuhusu tatizo la ujangili wa tembo ambao wamechinjwa kwa maelfu miaka ya hivi karibuni kwa ajili ya meno yao. Hatimaye Alikiba ametoa wimbo wake “Lupela” uliokuwa ukisubiriwa na mashabiki wake Afrika Mashariki kwa wiki kadhaa sasa. Wimbo huo ni sehemu ya kampeni ya “Ujangili Unatuumiza Sote” iliyozinduliwa mwaka jana na WildAid na African Wildlife Foundation mashirikia yanayofanya kazi pamoja barani Afrika na Asia kupunguza mahitaji ya bidhaa zitokanazo na wanyamapori na kuongeza uelewa wa janga la ujangili linaloikabili Afrika. Katika uzinduzi uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye hoteli ya Slipway jijini Dar es salaam, wageni mbalimbali na waandishi wa habari walipata

ASILIMIA 10 YA WATANZANIA WANAMILIKI UCHUMI WA NCHI’

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua  Mkutano wa Wadau wa Uwezeshaji  Wananchi Kiuchumi kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua  Mkutano wa Wadau wa Uwezeshaji  Wananchi Kiuchumi kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kaipata maelezo kutoka kwa Bi Fatuma Kango kuhusu Msimbomilia  au Barcode baada ya kufungua Mkutano wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es slaam Februari 9, 216. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafisi nchini, Reginald Mengi baada ya kufungua mkutano wa  Wadau wa Uwezeshaji Wananchi  Kiuchumi kwenye

Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda Apata Ajali Mbaya ya Gari

Image
Mtu mmoja amefariki dunia na wengine wanne wamejeruhiwa akiwemo mke wa waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda Mama Tunu Pinda baada ya gari walilokuwa wakisafiria kumgonga mwendesha pikipiki wakati akikatisha barabara katika eneo la Mkundi barabara ya Morogoro Dodoma manispaa ya Morogoro. Ajali hiyo imetokea majira ya saa nane mchana katika eneo la Mkundi ikihusisha gari lenye namba za usajili STK 9242 gari la mke wa waziri mstaafu Mizengo Pinda likitokea Dodoma kwenda jijini Dar-es-Salaam  na pikipiki Majeruhi wengine wa ajali hiyo ni dereva wa gari hilo Bw Anjelo Mwisa, mlinzi wa mke wa waziri mkuu mstaafu Gaudensi Tembo na kijana wa familia ya Mama Tunu Pinda Bwana Gilbert Sampa. Kwa upande wake mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa mkoa wa Morogoro Dr Rita Liamuya amesema hali ya mke wa waziri mkuu mstaafu na majeruhi wengine zinaendelea vizuri na kueleza kuwa  majeruhi hao wanatarajia kuhamishiwa jijini Dar-es-Salaam kwa matibabu zaidi TOA MAONI YAKO

Breaking News.....Watuhumiwa 9 walio tungua HELKOPTA wamekamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Simiyu wakiwa na bunduki 27

Image
Watuhumiwa 9 wamekamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Simiyu wakiwa na bunduki 32 pamoja na meno matatu ya Tembo. .. Watuhumiwa walihusika kumuua Rubani wa Helicopter ya Mwiba. ... Mmoja alikamatwa akafanikisha wengine 8

UN Yalaani Korea Kaskazini Kurusha Kombora la Masafa Marefu

Image
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limelaani hatua ya Korea Kaskazini kulipua Kombora la masafa marefu. Katika taarifa iliyotolewa baada kikao cha dharura mjini New York imesema baraza limekubaliana kuiwekea nchini hiyo vikwazo vya kiuchumi mapema iwezekanavyo,lakini pia baraza hilo limeilaumu Korea Kaskazini kwa kukiuka maazimio ikiwa ni pamoja na hatua yake ya kulipua bomu la nyuklia mwezi January. Kauli hizo za kuilaani hatua hiyo Korea Kaskazini zimetowa maeneo mbali mbali duniani pamoja na kulaumiwa na dunia Korea Kaskani yenyewe imesema imelipua kombora hilo ili kutuma mitambo ya satellite angani,jambo linalopingwa na mahasimu wake kuwa hiyo ni danganya toto kwani ina nia ya kujaribu kombora angani. Akitoa taarifa ya kulaani hatua hiyo Rais wa Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa ambaye pia ni Balozi wa Venezuela Rafael Ramirez Carreno amesema wanachama wamekubaliana kulaani kile alichosema ukiukwaji Korea Kaskazini wa azimio la Umoja wa Mataifa. Rafael Ra

Ni vitu vidogo lakini ukivizingatika kila asubuhi utakuwa na furaha siku nzima

Image
Wimbo wa Happy wa Pharrell Williams ulikuwa moja ya nyimbo ninazosikiliza kila ninapo amka asubuhi, kwanini sababu ni siku mpya na nilitaka kuanza na furaha kama jina la nyimbo. Je, wewe unafanya nini cha kwanza unapoamka asubuhi.? Kuna vitu vidogo sana unaweza ukawa unafanya kila siku na ukajisikia mwenye furaha na ukaanza siku yako vizuri Usizime Alarm (kengere). Kuna wakati unahitaji kitu cha kukufanya uamke muda unaopanga wewe asubuhi. Kengere ya simu au saa ya mezani, inapoita wengi wetu sababu ya usingizi mwingi tunaizima na kuendelea na usingizi,  kwa dakika chache,  ila ni vizuri kama ulipanga kuamka muda huo basi na uamke . panga ratiba yako na uizoe. Tafuta Ujumbe wa kukupa moyo. Kuna wakati tunahitaji mtu wa kutuambia tunaweza,weka chumbani kwako ujumbe mzuri wa kukupa moyo kama “You’re the Best” au unaweza ukaingia Google na kutafuta “inspiration quotes” hizi ni nikuu za watu mbalimbali, ambazo unaweza kusoma kila unapo amka uanze na siku mpya

Utafiti umeonesha wanaume wenye vipara ni wanaume wenye mvuto zaidi kimapenzi!

Image
Kuna vitu vingi humvutia mtu inapokuja swala la kumchagua mpenzi, siwezi taja sifa zote, kila mtu anasifa zake na vigezo vyake, ila ngoja tuongelee mvuto wa kipekee unaopatikana kwa wanaume wenye vipara. Nikiongelea vipara naongelea wale walio na vipara asili, achilia mbali wale wanaopenda kunyoa vipara japokuwa kuna baadhi ya sifa hapa wanaweza wakawa nazo pia. Muonekano wa kiume: wanaume wenye vipara wengi huwa na muonekana wa kiume zaidi,muonekano nadhifu  sina maana kama wanaume wengine walio na nywele ndefu ama wastani hawana mvuto lah, nauongelea mvuto zaidi ama mvuto wa kipekee. Ujasiri: wanaume wa aina hii wengi huonekana ni wajasiri kwa muonekano wao tu, hii huwafanya kuwa kivutio kwa wanawake. Wana hisia kali za kimapenzi: daktari kutoka Chuo cha Yale Marekani , James B. Hamilton alisema katika utafiti wake wanaume wengi walio na vipara miili yao huwa inazalisha mbegu nyingi za kiume kuliko wanaume wenye nywele, japokuwa si kwa asilimia 100 alisema

INATIA HURUMA SANA....HUYU MTOTO KAOMBA KUONA NDEGE WAKATI AKISUBIRIA KUFA ...ANAUMWA KANSA NA ANASUBIRI KUFA TU

Image
A child in an ambulance is at kotoka airport , u know why,? He want to see an aeroplane before he dies, yes die , his parents couldn't afford treatment for canc er and he was kept at home till it got worse. Now there is nothing to do and he will die any moment from now but he begged the hospital to make him see a plane before he die. TOA MAONI YAKO HAPA CHINI

Simba hatari, yashinda mechi ya sita mfululizo.

Image
Wachezaji wa Simba wakishangilia goli. Johnson James, Shinyanga SIMBA ni hatari! wala huwezi kubisha kwa hilo baada ya kufanikiwa kuichapa Kagera Sugar bao 1-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliopigwa katika Uwanja wa Kambarage, jana. Simba sasa haijapoteza kwenye michezo yote ambayo imecheza chini ya kocha mpya wa timu hiyo, Jackson Mayanja, ukiwa ndiyo mchezo ambao uliaminika kuwa unaweza kuwa kizuizi kwa timu hiyo ya Msimbazi. Hii imeonyesha kuwa Simba ndiyo timu ambayo inaweza kuwa na nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa baada ya kucheza michezo sita (ukiwemo wa Kombe la FA) mfululizo na kufanikiwa kushinda yote. Ilianza kwa kuichapa Mtibwa 1-0, JKT Ruvu 2-0, Burkina Faso 3-0 (Kombe la FA), African Sports 4-0, Mgambo 5-1 na mchezo wa jana. Simba ambao awali chini ya kocha Dylan Kerr walionekana kuwa nyanya walijipatia bao lao kupitia kwa Ibrahim Ajib, ambaye alifunga bao safi akipata pasi kutoka kwa Hamis Kiiza. Hata hivyo, Simba walikuwa wanaweza kuibuka na us

BREAKING NEWS : FREEMAN MBOWE ATANGAZA BARAZA KIVULI LA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI,

Image
Freeman Mbowe na mawaziri Vivuli.  Ofis ya rais Tamisemi jafar maiko Utumishi Lucy molel Makam muungano Ali saleh A. Ali PM bunge kazi na ajira Esta bulaya Sera na mipango Halima mdee Naibu silinde Uchukuzi Injinia mbatia Will kambalo Nishat  Mnyika na heche Maambo ya nje Msigwa Kilimo Makdalena sakaya Ulinzi Juma hamad omar Waitara naibu Mambo ya ndani Lema Ardhi Wilfred lwakatare Maliasili Estamatiko na pareso Viwanda Kalist komu Elimu Suzan limo Afya Dk godwin molel Habar  Joseph mbiliny Minja devota Maji Hasan bobali Peter lijualikali Katiba na sheria Tundu lisu

Aliyedaiwa kumbaka shilole afunguka mazito!

Image
  Makala Elia Joseph. Makala: richard manyota -igunga KATIKA maho-jiano na Mwandishi nguli wa burudani nchini wa Gazeti la Ijumaa, Erick Evarist, Februari 2012, msanii Zuwena Mohammed ‘Shilole’ alinukuliwa akieleza kisa hiki: “Katika maisha yangu nimepitia mitihani mingi, mmoja wapo ni huu wa kulazimishwa kufanya mapenzi bila ridhaa yangu, kwa kifupi nilibakwa.” Kwa kuwa kisa hiki cha kusikitisha kimesemwa sana na Shilole katika mahojiano yake mengi na vyombo mbalimbali vya habari, Gazeti la Ijumaa lililazimika kufunga safari mpaka wilayani Igunga mkoani Tabora ili kumtafuta anayetuhumiwa kumbaka ambapo lilifanikiwa kufanya naye mahojiano. UTAMBULISHO WA JINA NA MAKAZI “Kwa jina naitwa Makala Elia Joseph. Nimezaliwa mwaka 1988 ni mtoto wa pili katika familia yetu. Naishi hapa Igunga, karibu na stendi ya mabasi yaendayo mikoani eneo la Barabara ya Singida. Mwandishi: Umejitambulisha vyema. Mimi ni Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Ijumaa, nimetoka Dar…(Kicheko kinakati

Mbunge adatishwa na penzi la Lungi

Image
Msanii maarufu wa filamu Bongo, Lungi Maulanga. Hamida Hassan na Gladness Mallya Taarifa ambayo gazeti hili linayo ni kuhusu mbunge moja machachari sana wa chama tawala (jina tunalihifadhi kwa sasa) ambaye kwa muda mrefu amekuwa akidaiwa kutoka kimapenzi kwa siri na msanii maarufu wa filamu Bongo, Lungi Maulanga. Chanzo makini ambacho kipo karibu na Lungi kimeeleza kuwa, Lungi na mheshimiwa huyo wamekuwa ‘lovers’ kiasi cha kufikia kila mmoja kufa na kuoza kwa mwenzake. Kisikie chanzo “Yaani suala la mheshimiwa (anataja jina la mbunge huyo) kutoka na Lungi siyo siri na wakati mwingine Lungi mwenyewe anajitapa kuwa sasa hivi ni matawi ya juu, nyie fuatilieni mtajua ukweli.” Ijumaa laingia mzigoni Kufuatia madai hayo, Ijumaa liliingia mzigoni kujaribu kuwafuatilia wawili hao hasa inapobainika mheshimiwa huyo yuko jijini Dar lakini hawakuweza kunaswa, hali iliyoonesha kuwa, huwa wanakutana kwa siri sana. Hata hivyo, rafiki huyo wa Lungi juzikati alimpigia simu mmoja wa

EDWARD LOWASSA AUNGA MKONO MAAMUZI YA CUF KUTOSHIRIKI UCHAGUZI ZANZIBAR

Image
Aliyekuwa mgombea wa nafasi ya urais akiungwa mkono na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananch UKAWA, Mh. Edwrad Lowassa amesema ni vema serikali ikahakikisha inapata suluhu ya mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa marudio machi 20 mwaka huu. Mh. Edward Lowassa amesema hayo ofisini kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam wakati wa kikao chake na wazee kutoka chama cha Chadema ambapo amesema  anaunga mkono uongozi wa CUF kutokushiriki uchaguzi huo huku akisisitiza endapo serikali ikishindwa kumaliza mgogoro huo kabla ya mach 20 huenda hali ya kisiasa Zanzibar ikabadilika. Aidha amewahakikishia wazee hao kuwa yeye na uongozi mzima wa UKAWA wako imara katika kuhakikisha wanatetea maslahi ya watanaznia ambapo pia amemshukuru waziri mkuu kwa kuruhusu mikutano suala ambalo linawapa fursa ya kujipanga ili kuwashukuru watanzania waliojitokeza kupiga kura mapema 25. Kwa mujibu wa risala ya wazee hao iliyosomwa na mzee Enec Ngomba

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. DKT. JOHN POMBE MAGUFULI MGENI RASMI SIKU YA SHERIA NCHINI, ASISITIZA UFANISI WA MAHAKAMA NA UTOAJI WA HAKI KWA WAKATI

Image
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipokewa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman leo jijini Dar es salaam wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini. Rais, Dkt. John Magufuli alikua mgeni rasmi.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (katikati) akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria leo jijini Dar es salaam.  Wimbo wa Taifa ukipigwa wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Sheria. Kulia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  (Kulia) akiwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman  Baadhi ya Viongozi waliohudhuria Maadhimisho ya Siku ya Sheria wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa. Kutoka kulia ni Jaji Mkuu wa Kenya Dkt. Willy Mutunga, Jaji Kiongozi wa Tanzania Mhe. Shaaban Lila (katikati) na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Sa