EDWARD LOWASSA AUNGA MKONO MAAMUZI YA CUF KUTOSHIRIKI UCHAGUZI ZANZIBAR
Aliyekuwa
mgombea wa nafasi ya urais akiungwa mkono na vyama vinavyounda umoja wa
katiba ya wananch UKAWA, Mh. Edwrad Lowassa amesema ni vema serikali
ikahakikisha inapata suluhu ya mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar
kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa marudio machi 20 mwaka huu.
Mh.
Edward Lowassa amesema hayo ofisini kwake Mikocheni jijini Dar es
Salaam wakati wa kikao chake na wazee kutoka chama cha Chadema ambapo
amesema anaunga mkono uongozi wa CUF kutokushiriki uchaguzi huo huku
akisisitiza endapo serikali ikishindwa kumaliza mgogoro huo kabla ya
mach 20 huenda hali ya kisiasa Zanzibar ikabadilika.
Aidha
amewahakikishia wazee hao kuwa yeye na uongozi mzima wa UKAWA wako
imara katika kuhakikisha wanatetea maslahi ya watanaznia ambapo pia
amemshukuru waziri mkuu kwa kuruhusu mikutano suala ambalo linawapa
fursa ya kujipanga ili kuwashukuru watanzania waliojitokeza kupiga kura
mapema 25.
Kwa
mujibu wa risala ya wazee hao iliyosomwa na mzee Enec
Ngombare,wamempongeza Mh. Lowassa kwa uvumilivu wake baada ya uchaguzi
ambapo pia wamemhakikishia kuwa wako pamoja nae katika safari ya
kuelekea mwaka 2020.
Katika
mkutano huo ambao uliohudhuliwa na kada wa siku nyingi Kingune Ngombare
Mwiru, Mh Lowassa amewataka wazanzibar na watanzania kwa ujumla kuwa
watulivu na kuhakikisha wanadumisha amani ya nchi hasa katika kipindi
hiki ambacho viongozi wanaendelea na juhudi za kutafuta suluhu ya
kisiasa visiwani Zanzibar.
Comments
Post a Comment