RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. DKT. JOHN POMBE MAGUFULI MGENI RASMI SIKU YA SHERIA NCHINI, ASISITIZA UFANISI WA MAHAKAMA NA UTOAJI WA HAKI KWA WAKATI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
akipokewa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman leo jijini
Dar es salaam wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini. Rais,
Dkt. John Magufuli alikua mgeni rasmi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
(katikati) akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria
leo jijini Dar es salaam.
Wimbo
wa Taifa ukipigwa wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Sheria. Kulia ni
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (Kulia) akiwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman
Baadhi
ya Viongozi waliohudhuria Maadhimisho ya Siku ya Sheria wakiwa
wamesimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa. Kutoka kulia ni Jaji Mkuu wa
Kenya Dkt. Willy Mutunga, Jaji Kiongozi wa Tanzania Mhe. Shaaban Lila
(katikati) na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Said Mecki Sadiki.
Baadhi
ya Viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini na wadau muhimu wa
Mahakama waliohudhuria Maadhimisho ya Siku ya Sheria wakitoa heshima zao
wakati wimbo wa Taifa ukipigwa.
Rais
wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Charles Rwechungura akitoa
salam na ujumbe wa Chama hicho wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria
leo jijini Dar es salaam.
Katibu
Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (kulia) akifuatilia hotuba
zilizokuwa zikitolewa na viongozi mbalimbali wakati wa maadhimisho ya
Siku ya Sheria. Kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama Bw. Hussein
Katanga.
Jaji
Mkuu wa Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akiwahutubia
viongozi, mabalozi na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi
waliohudhuria maadhimisho ya Siku ya Sheria.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
akisisitiza jambo kuhusu utendaji wa Mahakama na Utoaji wa Haki kwa
wananchi kwa wakati kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria. Mhe. Rais
alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo yaliyohudhuriwa na viongozi
na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
katika picha ya pamoja na Majaji wa Mahakama ya Tanzania leo wakati wa
kilele cha Siku ya Sheria nchini.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
katika picha ya pamoja na viongozi wa dini na baadhi ya wakuu wa vyombo
vya ulinzi na Usalama na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania
wakati wa kilele cha Siku ya Sheria.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mawakili.
Jaji
Mkuu wa Kenya Dkt. Willy Mutunga (kulia) akimkabidhi zawadi ya
kumbukumbu kutoka nchini Kenya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli leo jijini Dar es salaam. Jaji Mkuu wa Kenya
alikua miongoni mwa wageni mashuhuri walioalikwa na Mahakama ya Tanzania
kuhudhuria maadhimisho ya Siku ya Sheria.
Wageni
mbalimbali waliohudhuria maadhimisho ya Siku ya Sheria wakifurahia
Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe
Magufuli aliyokua akiitoa leo jijini Dar es salaam.
……………………………………………………………………….
(Na. Jacquiline Mrisho/Aron Msigwa – Dar es salaam)
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka
Mahakimu na Majaji wa Mahakama ya Tanzania kufanya kazi kwa kuzingatia
weledi wa taaluma ya Sheria katika kushughulikia mashauri yanayopelekwa
Mahakamani.
Aidha amewataka Majaji na Mahakimu kutoa hukumu za mashauri yanayowasilishwa Mahakamani kwa haraka ili kuwasidia wananchi wanaotafuta haki.
Akizungumza
na mamia ya wageni kutoka ndani na nje ya nchi waliohudhuria
Maadhimisho ya Siku ya sheria, Dkt. Magufuli amewataka Majaji na
Mahakimu hao kutanguliza Uzalendo na maslahi ya taifa mbele pindi
wanapotoa maamuzi ya mashauri yaliyoko Mahakamani.
Mhe. Rais
amemtaka Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman kuchukua
hatua kwa watendaji wa Mahakama wanaokiuka maadili kwa kufanya vitendo
vinavyochafua taswira ya Mahakama mbele ya macho ya jamii.
Aidha,
Katika hotuba yake Mhe. Rais amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano
itaendelea kuijengea uwezo wa kifedha Mahakama ili iweze kutekeleza
majukumu yake ipasavyo.
Comments
Post a Comment