ASILIMIA 10 YA WATANZANIA WANAMILIKI UCHUMI WA NCHI’
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Mkutano wa Wadau wa Uwezeshaji
Wananchi Kiuchumi kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius
Nyerere jijini Dar es salaam Februari 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Mkutano wa Wadau wa Uwezeshaji
Wananchi Kiuchumi kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius
Nyerere jijini Dar es salaam Februari 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa kaipata maelezo kutoka kwa Bi Fatuma Kango kuhusu
Msimbomilia au Barcode baada ya kufungua Mkutano wa Uwezeshaji
Wananchi Kiuchumi kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu
Julius Nyerere jijini Dar es slaam Februari 9, 216. (Picha na ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya
IPP na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafisi nchini, Reginald Mengi
baada ya kufungua mkutano wa Wadau wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi
kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es
salaam Februari 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Rais wa VICOBA, Devota Likokola
(wapili kulia ) wakati alipotembelea banda la Benki ya Posta Tanzania
katika Mkutano wa Wadau wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi alioufungua
kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha walimu Julius Nyerere jijini
Dar es salaam Februari 9, 2016. (Picha na Ofisi yaWaziri Mkuu)
…………………………………………………………………………………………………………
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imebuni na kuanza kutekeleza Sera
ya Uwekezaji ili kufikia lengo la kuwawezesha wananchi kiuchumi.
“Taarifa
zilizopo zinaonyesha ni asilimia 10 tu ya Watanzania ndio wanaomiliki
uchumi wa nchi na sera hiyo ndiyo inatoa mwongozo wa jumla unaohakikisha
kwamba wananchi wanapata fursa mbalimbali za kiuchumi ambazo
zitawawezesha kujenga na kufaidika na uchumi wa mchi yao,” alisema.
Waziri
Mkuu amesema maeneo yanayolengwa na sera hiyo ni yale yenye kuleta
matokeo ya haraka na yanayogusa maisha ya wananchi hasa katika sekta za
kilimo, ufugaji, uvuvi, misitu, ujenzi, biashara, utalii, madini,
viwanda na usafirishaji.
Ametoa
kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Februari 7, 2016) wakati akizungumza na
washiriki wa Mkutano wa Kwanza wa Wadau wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi
nchini uliofanyika kwenye ukumbi wa kituo cha kimataifa cha mikutano
cha mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Alisema
Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 inalenga kuhakikisha kuwa sehemu kubwa
ya uchumi wa nchi yetu inamilikiwa na Watanzania wenyewe. Waziri Mkuu
pia alizindua Mwongozo wa Utekelezaji Mkakati wa Taifa wa Uwezeshaji
Wananchi Kiuchumi.
Mapema,
akimkaribisha Waziri Mkuu kufungua mkutano huo, Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Walemavu, Bibi Jenista Mhagama
alisema hadi sasa mikoa 20 imekwishatenga maeneo ya uwekezaji kwenye
halamhashauri zake na imeanza kuweka miundombinu ya kuvutia wawekezaji.
Naye
Mweyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Prof.
Omari Issa alisema katika dunia ya sasa imebainika kuwa haina maana
kumpatia mtu mkopo bila kumtafutia masoko au kumuunganisha wadau wa
masoko. Kwa hiyo wamejipanga kuwasaidia Watanzania kwa kuwaunganisha na
masoko.
Comments
Post a Comment