Kwani ni lazima uolewe???
HAKIKA sifa na utukufu zimuendee yeye Jalali ambaye ametupa nafasi ya kuweza kukutana tena siku ya leo hii.Moja ya kitu kinachonishangaza kwa wanawake wengi ni kuwa na ndoto zaidi ya kuolewa kuliko kufikia ndoto zao halisi kwa maana ya maono ambayo wamekuwa wakiyawaza kwa muda mrefu. Tabia hii ya wanawake wengi ya kutaka au kukimbilia kuolewa si jambo baya, kama ikitokea ukapata bahati hiyo ya kuolewa lakini kama haitatokea sio ishu sana bali kumbuka kuwa kuna maisha nje ya kuolewa nayo si mengine ni maisha ya kufikia ndoto zako.
Kama haujaolewa
Ni kweli Mungu alituumba na kutuweka duniani ili tuujaze ulimwengu
lakini hata hilo la upande wa pili nalo ni la kushukuru pindi
linapokukuta, linauma ila kupunguza maumivu yake ni kulikuba li na
kujifunza vitu vingine vingi ili uweze kuendelea na maisha mengine.
Hulka ya wanawake
kuolewa imekuwa ni sehemu ya wengi wao, utamsikia binti wa miaka 16
amemaliza darasa la saba anataka kuolewa eti kisa amefeli mtihani wa
mwisho, wewe nani kakuambia ukifeli mtihani wa drasani ndiyo umefeli
maisha? Umefeli kutimiza ndoto zako?
Kukosa bahati
Kuna wakati naamini wanawake wanakosa fursa au bahati ya kusaidiwa vitu
f’lani na mwanaume anayekuwa naye, kwa kuhofia ataambiwa kuoa wakati huo
pengine yeye hana uwezo huo.
Nje ya ndoa Lengo
langu si kukufanya wewe mwanamke usiolewe bali ni kukukumbusha kuwa kuna
mambo mengine zaidi ya hilo. Kuolewa sio ndoto ni wajibu ambao Mungu
ameuweka kwa wanadamu pindi watakapoafikiana ila kila mtu ana ndoto
zake.
Usisahau ndoto zako
Wanawake wengi wamekuwa wakilisahau hilo la ndoto, wamesahau pindi
walipokuwa wanasoma na walipoulizwa kuwa wakikuwa wanapenda kuwa akina
nani? Najua wewe unayesoma mada hii ulisema unataka kuwa mtetezi wa
wanawake, kuna mwingine alisema anataka kuwa mwanasheria, rais, mwalimu,
mwanasayansi, rubani na kadhalika, sasa nashangaa leo ndoto zako zote
zimeyeyuka kinyemela hivyo?
Acha mawazo mgando
Funguka kama ikitokea hujabahatika kutokuolewa usijilaumu na kujiona
kama una mkosi vile, lahasha! bado unaweza kutimiza ndoto zako, ndoto
zinapiganiwa, ndoa ni maridhiano na makubaliano.Mada hii haihalalishi nwanaume kuendekeza tabia ya kutaka kukutana faragha mwenza wake bila kufikia malengo ya kuoana kwani ni tendo lenye baraka na ni muhimu sana kama utafanikiwa ila kutimiza ndoto yako au zako ni kubwa pia.
ss.GP
TUPE MAONI YAKO NA USISAHAU KULIKE PAGE YETU KWA HABARI NA MAKALA ZAIDI
Comments
Post a Comment