
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limelaani hatua ya Korea Kaskazini kulipua Kombora la masafa marefu.
Katika taarifa iliyotolewa baada kikao cha dharura mjini New York
imesema baraza limekubaliana kuiwekea nchini hiyo vikwazo vya kiuchumi
mapema iwezekanavyo,lakini pia baraza hilo limeilaumu Korea Kaskazini
kwa kukiuka maazimio ikiwa ni pamoja na hatua yake ya kulipua bomu la
nyuklia mwezi January.

Kauli
hizo za kuilaani hatua hiyo Korea Kaskazini zimetowa maeneo mbali mbali
duniani pamoja na kulaumiwa na dunia Korea Kaskani yenyewe imesema
imelipua kombora hilo ili kutuma mitambo ya satellite angani,jambo
linalopingwa na mahasimu wake kuwa hiyo ni danganya toto kwani ina nia
ya kujaribu kombora angani.

Akitoa
taarifa ya kulaani hatua hiyo Rais wa Baraza la Usalama la Umoja wa
mataifa ambaye pia ni Balozi wa Venezuela Rafael Ramirez Carreno amesema
wanachama wamekubaliana kulaani kile alichosema ukiukwaji Korea
Kaskazini wa azimio la Umoja wa Mataifa.

Rafael
Ramirez Carreno,amesema ”Wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa
Mataifa kwa kauli wamelaani vikali hatua hii ya kulipua kombora hilo,
wanachama wa Baraza la usalama la umoja wa mataifa wamesisitiza kuwa
jaribio hilo na mengine ya ulipuaji yaliyofanywa na Korea Kaskazini
ambayo yanatumia teknologia ya angani hata kama yana tabia kama ya
ulipuaji mitambo inayofanana na ya satellite, yanachangia mfumo wa Korea
Kaskani wa kulipua silaha za nyuklia ambayo ni hatari na inayokiuka
azimio la Umoja wa Mataifa.

Kwa
upande wake balozi wa Marekani ndani ya Umoja wa Mataifa Samantha Power
amesema hakuna mtu anayeweza kufanywa mjinga na Korea Kaskazini kwamba
inalipua kombora kwa ajili ya mipango ya satellite na shughuli za anga.
Samantha Power, amesema kwamba “Ambacho Korea Kaskani imefanya kwa
tukio hili, tukio ambalo ni kinyume cha sheria, katika matukio yote ya
ulipuaji , ni ulipuaji wenye kuendeleza mipango ya Korea Kaskanini
kuongeza uwezo wake wa kuendeleza utengenezaji wa silaha za nyuklia.
Hatua hiyo ya Korea Kaskazini imeelezwa kuwa sio tu ukaidi kwa moja
ya matukio hayo, nchi hiyo inasonga mbele hatua moja katika kudhihirisha
azma yake ya kuendeleza nyuklia yenye uwezo wa kuingia bara nyingine
kwa kombora la angani, hili hatutalikubali wala hatutaruhusu hili
kutokea.
Chanzo: BBC
Comments
Post a Comment