SABABU ZA UKAWA KUSUSIA KAMATI ZA BUNGE NA KUMGOMEA SPIKA NDUGAI
Wakati vikao vya Kamati za Kudumu za Bunge vikitarajiwa kuanza leo kwa uteuzi wa wajumbe, wabunge wa upinzani tayari wameanza kwa kumtikisa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Job Ndugai, baada ya kususia uchaguzi wa wenyeviti wa kamati hizo. Dalili za mgawanyiko kwenye kamati hizo zilianza kuonekana juzi, baada ya wabunge hao wa Kambi ya Upinzani kufanya kikao na kuweka msimamo wa kutaka kushirikishwa kwenye uteuzi wa wajumbe. Kambi ya Upinzani ilisema inataka kushirikishwa katika hatua hiyo ikidai kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM), imekuwa ikiwapangia watu wa kuongoza kamati zinazosimamia mapato ya serikali ambazo kikanuni zipo chini yao. Aidha, jana hali ilikuwa ngumu ndani ya kambi ya CCM ambao walifanya vikao tangu asubuhi mpaka jioni kujadili kamati hizo. SABABU ZA UPINZANI KUSUSA Viongozi hao wa kambi ya upinzani walidai kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakipangiwa watu wa kuongoza Kamati ya Hesabu za Serikali za (PAC) na ile ya Hesabu za Serikali za Mitaa