SERIKALI YAKANUSHA UZUSHI UNAOENEZWA KATIKA MITANDAO YA KIJAMII KUMHUSU RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Kaimu
Mkurugenzi wa idara ya Habari MAELEZO Bi Zamaradi Kawawa akitoa
ufafanuzi juu ya taarifa za uzushi unaosambazwa katika mitandao ya
Kijamii ya ndani na nje ya nchi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimwa Dkt. John Pombe Magufuli amefukuza wageni kutoka nje
waliokuwa wanafanya biashara hapa nchini kwa kuwa Serikali yake
haitataki wageni wafanye bishara zao nchini ambapo ukweli ni kwamba
Serikali haijafukuza wageni wanaofanya biashara zao nchini na haina
mpango wa kufanya hivyo kwa wageni wanaoishi nchini kwa vibali
vilivyotolewa kisheria na Serikali.kushoto ni Naibu Kamishna na Msemaji
wa Idara ya Uhamiaji Bw. Abbas Irovya na mwisho kushoto ni Msemaji wa
Wizara ya Mambo ya Ndani Isaac Nantanga,Kulia ni Naibu Kamishna wa Idara
hiyo Bw.Wilson Bambaganya.
Naibu
Kamishna na Msemaji wa Idara ya Uhamiaji Bw. Abbas Irovya akitoa wito
kwa Watanzania kuwafichua wale wote wanaoingia na kuishi nchini kinyume
cha sheria ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa kwa mujibu wa Sheria na
kanuni na kusisitiza kuwa Ofisi yake itaendelea kufanya oparesheni ya
kuwakamata watu hao, kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa idara ya Habari
MAELEZO Bi Zamaradi Kawawa na Mwisho Naibu Kamishna wa Idara hiyo
Bw.Wilson Bambaganya.
Baadhi
ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano Idara ya Habari Maelezo kwa
kushirikiana na Idara ya Uhamiaji ukilenga kutoa ufafanuzi kuhusu
taarifa za upotoshaji zinasozambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa
Serikali imewafukuza wafanyabiashara wakigeni wanaofanya kazi zao hapa
nchini ,taarifa hizo si za kweli na zinalenga kuichafua Serikali ya Rais
Dkt. John Pombe Magufuli.
(Picha na Frank Mvungi-Maelezo)
………………………………………………………………………….
Hivi
karibuni kumejitokeza uzushi unaosambazwa katika mitandao ya kijamii ya
ndani ya nchi na nje ya nchi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli amefukuza wageni kutoka nje
waliokuwa wanafanyabiashara zao nchini kwa kuwa serikali yake haitaki
wageni kufanya biashara nchini.
Serikali
haijafukuza wageni kutoka nje ya nchi kufanya biashara nchini na haina
mpango wa kuwafukuza wageni wanaoishi nchini kwa vibali vilivyotolewa
kisheria na Idara ya Uhamiaji.
Uzushi
huo usiokuwa na ukweli umeenezwa kufuatia Idara ya Uhamiaji kutekeleza
jukumu lake la kufuatilia wageni wote wanaoishi nchini bila vibali
halali vya ukaazi ambapo kwa mwezi Novemba na Desemba mwaka 2015 wageni
372 walioondoshwa nchini.
Kazi
ya kufuatilia wageni wanaoishi nchini bila vibali halali vya kisheria
haijaanza katika Serikali ya Awamu ya Tano. Idara ya Uhamiaji nchini
tangu Januari hadi Desemba mwaka jana iliondosha nchini jumla ya wageni
1,642 waliokuwa wanaishi na kufanya shughuli zao nchini kinyume na
Sheria.
Uzushi
unaoenezwa hauna ukweli wowote na hauna nia njema na nchi yetu kwani
kati ya mwaka 2014 na 2016 Idara ya Uhamiaji imetoa vibali vya ukaazi
(Residence Permits) 40,765 kwa wageni wawekezaji na wafanyabiashara,
wageni wanaofanyakazi za kuajiriwa, wageni wanaokuja kwa ajili ya
Masomo, matibabu, dini, utafiti na wastaafu kuishi na kufanya shughuli
zao nchini.
Serikali inawakaribisha wageni kuja nchini kuwekeza na kufanya shughuli zao kwa kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu za nchi.
Aidha,
kuna uzushi unaenezwa kuwa Rais Dkt John Pombe Magufuli amepiga
marufuku wanawake kuvaa nguo fupi kama njia ya kupunguza kasi ya
maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI.
Mheshimiwa
Rais tangu aingie madarakani hajawahi kuagiza wala kutoa tamko
kuhusiana na uzushi wa kukataza uvaaji wa nguo fupi ili kupunguza
maambukizi ya Ukimwi kama inavyoenezwa katika mitandao ya ndani na Nje
ya Nchi ambayo inanukuu habari hiyo kuwa imeandikwa na Gazeti la Kenya
“The Standard”
Serikali
inapenda kuutangazia umma kuwa uzushi huo unaomhusu Mheshimiwa Rais
Magufuli umetungwa na watu wasioitakia mema nchi yetu kwa lengo la
kumdhalilisha Rais na hauna ukweli hivyo watu wasishiriki kuueneza kwa
njia yeyote ile.
Serikali
kupitia balozi zake za Kenya na Afrika Kusini zinafuatilia chanzo cha
uzushi huu kuhusu Rais Magufuli kwa kushirikiana na nchi husika na
watakaobainika kutunga na kueneza uzushi huu watachukuliwa hatua za
kisheria
Comments
Post a Comment