RAIS DKT MAGUFULI AKIWASALIMIA WANANCHI JIJINI ARUSHA WAKATI AKIELEKEA WILAYANI MONDULI KIKAZI
Amiri
Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli akisalimiana na wananchi wa Arusha Mjini wakati akipita
Barabarani kuelekea Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli ambako
pamoja na mambo mengine kesho tarehe 23 Januari, anatarajiwa kutunuku
Kamisheni kwa Maafisa wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli
kundi la 57/15.
Amiri
Jeshi Mkuu,Rais Dkt Magufuli akiwasikiliza wananchi kwa makini
alipopita maeneno ya Sanawali kuwasalimia wakati akielekea Wilayani
Monduli.
Baadhi
ya Wananchi wa Maeneo ya Sanawali wakishangilia ujio wa Rais John Pombe
Joseph Magufuli,alipokuwa akielekea Wilayani Monduli mapema leo
asubuhi.
Rais
Magufuli akiwa amevalia sare za kijeshi amesimamishwa na kuwasalimu
wananchi katika maeneo ya SANAWALI, TEKNIKO, NGARENALO, MBAUDA, MAJENGO
na KISONGO
Comments
Post a Comment