Bahati Bukuku Aishiwa Nguvu

MMG_2228Mwimba Injili mahiri Bongo, Bahati Bukuku akiwa na huzuni baada ya kufiwa na mama yake.
DAR ES SALAAM: Pole! Mwimba Injili mahiri Bongo, Bahati Bukuku hivi karibuni aliishiwa nguvu wakati akimzika mama yake mzazi, Enea Bukuku aliyefariki dunia Januari 12, mwaka huu jijini Mbeya kwa ugonjwa wa shinikizo la damu (presha).
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, Bahati alikumbwa na hali hiyo mara baada ya kuuaga mwili wa mama yake, tayari kwa safari ya kwenda kuupumzisha kwenye Makaburi ya Mlima James jijini humo.
IMG_8413
…..Akiweka shada la maua.
“Jamani kifo cha mama kinauma sana! Bahati amejikuta akiishiwa nguvu msibani. Nimemhurumia sana huyu dada, lakini naamini Mungu atamtia nguvu maana yeye ndiye aliyetoa na ndiye aliyetwaa, jina lake libarikiwe,” alisema shuhuda huyo.
Akaendelea: “Lakini nimeona waimba Injili wenzake, nilimwona Bonny Mwaitege naye kutoka Dar amekuja kumzika mama wa mwimba Injili mwenzake. Bahati anahitaji uangalizi kwa siku mbili hizi, kwani muda mwingi namwona ana simanzi tu.”
MMG_2271Bony Mwaitege akichukua matukio kwenye mazishi hayo.
Juzi, Amani lilimtafuta Bahati kwa njia ya simu yake ya mkononi na kumpa pole ambapo alisema anaendelea vizuri na Jumatatu ijayo, atarudi Dar.
“Asante. Tumeshamzika mama. Mimi naendelea vizuri, Mungu ni mwema. Jumatatu inayokuja nitarudi Dar,” alisema Bahati kwa majonzi.

Comments

Popular posts from this blog