TAKUKURU YAMKINGIA KIFUA MKURUGENZI WA MANISPAA YA TABORA MBELE YA BARAZA LA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA
Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora, Sipora Liana. Mkurugenzi wa Manispaa ya Tabora, Sipora Liana, akijieleza mbele ya Baraza la Maadili kwa Viongozi wa Umma Dar es Salaam leo, alipofikishwa kwa tuhuma za kukiuka maadili ya viongozi wa umma alipokuwa Halmshauri ya Manispaa ya Mkuranga mkoani Pwani kabla ya kuhamishiwa Tabora. Jaji Msumi (katikati), akiwa na wenzake akisikiliza shauri hilo. Na Dotto Mwaibale KAMANDA wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Wilaya ya Mkuranga, Damas Pasalau, amemkingia kifua aliyekuwa Mkurugenzi wa Halamashauri ya Manispaa ya Mkuranga Sipora Liana kwa tuhuma zinazomkabili katika Baraza la Maadili ya Utumishi wa Umma. Kwa mujibu wa hati ya mashitaka iliyosomwa katika vikao vya baraza a maadili vilivyoanza jana jijini Dar es Salaam, Sipora ambaye kwa sasa Mkurugenzi wa Manispaa ya Arusha anakabiliwa na tuhuma za kukiuka maadili. Inadaiwa kuwa mnamo mwaka 2009/2010 Sipora alimchukulia hatua za kinidh