Jaji Msumi (katikati), akiwa na wenzake akisikiliza shauri hilo.
Na Dotto Mwaibale
KAMANDA wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Wilaya
ya Mkuranga, Damas Pasalau, amemkingia kifua aliyekuwa Mkurugenzi wa
Halamashauri ya Manispaa ya Mkuranga Sipora Liana kwa tuhuma
zinazomkabili katika Baraza la Maadili ya Utumishi wa Umma.
Kwa
mujibu wa hati ya mashitaka iliyosomwa katika vikao vya baraza a
maadili vilivyoanza jana jijini Dar es Salaam, Sipora ambaye kwa sasa
Mkurugenzi wa Manispaa ya Arusha anakabiliwa na tuhuma za kukiuka
maadili.
Inadaiwa
kuwa mnamo mwaka 2009/2010 Sipora alimchukulia hatua za kinidhamu bila
sababu za msingi kwa kumsimamisha kazi aliyekuwa Ofisa Kilimo, Mifugo na
Ushirika Wilaya ya Mkuranga Dk. Fransis Mallya kinyume na sheria ya
maadili ya utumishi wa umma.
Pasalaus
alitoa utetezi kwa muda wa dakika 30 ambapo kati ya hizo 10 alizitumia
kutoa utetezi wakati akiulizwa maswali na Mwanasheria wa Serikali
Getrude Cyriacus.
Pasalau
ambaye mara kwa mara alibanwa na mwanasheria huyo kwaajiri ya kutoa
ushahidi sahihi aliendelea kumtetea huku akitoa mifano mbalimbali na
utendaji kazi wake uliofanyika katika Wilaya aliyotoka Sipora huku
akidai kuwa ni kitendo hichop ni chuki binafsi hivyo zisiruhusiwe
kushika nafasi kwenye mali za umma.
Wakati
akitoa ushahidi huo alimtaka Jaji Hamis Msumi kutenda haki na kudai
kuwa Mkurugenzi huyo hana kosa bali ni hujuma za baadhi ya watu ambao
walikuwa kwa maslahi yao binafsi katika ofisi za Manispaa hiyo.
Alisema
awali katika Manispaa hiyo kulikuwa na msuguano kati ya Madiwani,
watumishi wa umma na wakurugenzi jambo ambalo baada ya kufanyika kwa
uchunguzi na taasisi hiyo ilibainika uwepo wa ubadhilifu wa mali za
umma.
"Baada
ya Sipora kuwasili katika halmashauri hiyo ambapo katika utendaji kazi
wake mzuri watu wengi hawakumpenda kwani wengi wao walikuwa wakifanya
shughuli zao kwa maslahi binafsi," alisema.
Alidai
baada ya Mkurugenzi huyo kufika na kuonekana utendaji wake unawabana
baadhi ya watu akiwemo Mallya na wenzie waliunda kundi ambalo lilikuwa
ni kwaajili ya kupambana nae.
"Watu hawa walitumia vyombo vya udhibiti wa maadili kutunga hoja za uwongo ili kuweza kufanikisha malengo yao.
"
Ila kiukweli mwenyekiti huyu mama amethubutu na ameweza kulingana na
hali ya mazingira yaliyoko katika halmashauri ile kwatu watendaji wengi
hawakupenda watu wa aina hii," alisema.
Akifafanua
zaidi kuhusu tatizo lililotokea hadi hatua za kusimamishwa kazi
zilipotokea alidai kuwa baada ya Mkurugenzi huyo kuwasili katika
halmashauri hiyo alianza kufuatilia idara ya Mallya katika kukamilisha
miradi ya Mabwawa ya Mkwalia pamoja na ununuzi wa vitotozi
visivyofanyakazi na kuweka mashamba hewa ambapo hakuwa amefanya kazi
yeyote.
Hata
hivyo shauri hilo liliahirishwa kutokana na anaedaiwa kuwa ni
mlalamikiwa Sipora, kutofika na mashahidi wake kama alivyowasilisha
idadi yao katika baraza la hilo.
Akihairisha
kikao cha baraza hilo, Jaji Msumi alisema shauri hilo litasikilizwa
hadi pale itakapotolewa hati maalum ya wito kwa mashahidi wa Mkurugenzi
huyo.
(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
|
Comments
Post a Comment