MAMA SALMA KIKWETE AHUDHURIA MKUTANO WA 9 WA WAKE WA MARAIS KUHUSU KANSA HUKO NAIROBI
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akielekea kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa
wa Jomo Kenyetta huko Nairobi kuhudhuria mkutano wa 9 wa Wake wa
Marais wa Nchi za Afrika unaozungumzia magonjwa ya saratani ya matiti,
shingo ya kizazi na tezi dume tarehe 20.7.2015.
PICHA ZOTE NA JOHN LUKUWI
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete na Mke wa Rais wa Niger Madame Dkt. Lalla Malika
Issofou Mahammadou wakiwa kwenye sherehe za ufunguzi wa mkutano wa 9 wa
Wake wa Marais wa nchi za Afrika. Mkutano huo ulifunguliwa rasmi na
Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyetta (hayupo pichani) tarehe
20.7.2015.
Rais
Uhuru Kenyatta wa Kenya na wake wa Marais kutoka nchi mbalimbali barani
Afrika wamesimama wakati wimbo waTaifa wa Kenya ukiimbwa.
Rais
Uhuru Kenyatta wa Kenya akiwa amesimama na baadhi ya wake wa Marais wa
Afrika wakati wimbo wa Mataifa ya Afrika ukiimbwa. Kushoto kwa Rais
Kenyatta ni Mkewe Mama Margret Kenyatta akifuatiwa na Mke wa Rais wa
Namibia Mama Monica Geingos, Mama Salma Kikwete na mwisho ni Mama Dkt.
Lalla Malika Issofou Mahammadou wa Niger.
Baadhi ya
Wake wa Marais wa Nchi za Afrika wakishiriki kumvisha mkanda maalum kwa
kuteuliwa kwake kuwa Balozi wa Hiari kwenye Masuala ya Afya ya Mama na
Mtoto Barani Afrika. Wanaomvisha mkanda huo kwa niaba ya wake wa Marais
ni (kutoka kushoto kwenda kulia) Princess Nikky Onyeri, Mwanzilishi na
Mkurugenzi Mkuu wa ‘Forum of African First Ladies against Cervical,
Breast and Prostate Cancer, Mama Dkt. Lalla Mahammadou wa Niger, Mama
Monica Geingos wa Namibia, Mama Mary Ayen Mayardit wa Sudan Kusini. Mama
Salma Kikwete na Mwisho ni Mama Mathato Mosisili wa Lesotho.
Baadhi ya
wajumbe kutoka Tanzania wanaoshiriki kwenye mkutano wa 9 wa Wake wa
Marais wa Afrika wakifuatilia kwa makini sherehe za ufunguzi.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akiteta jambo na Princess Nikky Onyeri,
Mwanzilishi wa Forum of African First Ladies Against Cervical, Breast
and Prostate cancer mara baada ya viongozi hao kutembelea Hospitali ya
HH Aga Khan jijini Nairobi tarehe 20.7.2015.
Comments
Post a Comment