Sentensi nyingine 22 za Faiza Ally kuhusu mavazi yake, mtoto, dini, umaarufu.. anajuta? (Audio & Pichaz)
Kama uko karibu na stori za TZ najua hautakuwa umesahau kuhusu ishu ya Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na mzazi mwenzake, Faiza Ally..
Mbunge huyo hakuridhishwa na mavazi ambayo mzazi mwenzake alionekana
nayo sehemu mbalimbali akaipeleka ishu Mahakamani kwamba kutokana na
mama wa mtoto anavyoonekana yeye haridhishwi mtoto kuendelea kulelewa na Faiza.
Chanzo cha yote ilikuwa ni aina ya mavazi, leo kwenye show ya #Nirvana @EATV Faiza alikuwa kwenye Interview na ishu kubwa ilikuwa kuhusu mavazi yake >>>>“Napenda
kuvaa vitu ninavyovaa, sina mavazi special naweza kuvaa vyovyote,
niliipenda idea ya kuvaa nepi (diapers) na sina tatizo nayo kabisa”
Faiza ni mama wa mtoto mmoja wa kike, kwenye upande wa malezi ikoje? >>> “Mimi
ni mama mzuri sana, ninamtazama mtoto wangu saa 24… mavazi yangu
hayaingiliani kabisa na malezi ya mtoto wangu… namlea kwa mazingira ya
heshima, heshima na nguo ni vitu tofauti… ninavaa mavazi ninayopenda na
bado nina heshima kwa watu. Sio lazima kila mtu akubali ninachofanya,
ninapofanya kitu kwa watu kukubali au kukataa ni matatizo yao” >>> Faiza Ally.
Kuna kitu chochote anachojutia kutokana na mavazi yake? >>> “Sina
ninachojuta, niko sawa… tukio ambalo sijafurahia ni moja la kupelekwa
Mahakamani na kunyang’anywa mtoto wangu kitu ambacho ninakifanyia kazi
na kinaenda vizuri.. sioni tukio baya zaidi ya watu kunitukana na ni
kawaida… ninaenjoy na ninapenda mavazi yangu” >>>>
Haya ndio maneno yake kuhusu nguo aliyoivaa kwenye KTMA 2015 >>> “Idea
ilikuwa ni nzuri mpaka pale ambapo nguo iliachana… lengo lilikuwa sio
kuacha makalio wazi, ile nguo baada ya kukaa kwenye gari ilishuka na
sehemu ya makalio ikabaki wazi… Wakati natoka nyumbani ilikuwa imekaa tu
vizuri, nilivyoshuka kwenye gari sikujiangalia, nilipofika red carpet
nikapigwa picha” >>>>
Anatoka kwenye familia inayofuata Dini? >>> “Baba
yangu sijawahi kumwona anakwenda Msikitini, sio kwamba naikana dini
lakini sijazaliwa kwenye familia ya kidini.. maisha yangu yako hivi
miaka yote na hakuna kilichobadilika kwenye maisha yangu… nafurahia
maisha yangu” >>>>
Huu ndio ushauri wake kwa wasichana kuhusu ishu ya fashion za mavazi >>>> “Wasichana
wajue kwamba kilicholeta gumzo ilikuwa bahati mbaya, ila wawe huru
wavae vitu wanavyovifurahia ila isitokee kama ile… kuna mavazi navaa na
kuna mavazi siwezi kuvaa” >>>>
Matukio ya mavazi yake yamempa umaarufu? Amepanga kufanya chochote? >>>> “Sijapanga
chochote, sikujua kama itakuwa ni umaarufu… mimi ni mwigizaji na
ninaandika kitabu, labda kwa kazi zangu hizo… kipande kilichoonekana sio
maisha yangu yote, ni sehemu ya mwili… Faiza ni mwanamke mzuri,
anayejielewa, mwenye akili timamu, mama bora, anayejipenda, mtu wa watu” >>>> Faiza Ally.
Kwenye Interview hiyo alikuwepo pia mwanamitindo Ally Rehmtullah, haya ndio maneno yake kuhusu nguo ya Faiza >>>> “Ubunifu
wake ulikuwa mzuri labda mawasiliano kati ya yeye na mbunifu wake
hayakuwa mazuri, vazi kama lile kwa utamaduni wetu lazima watu
watashtuka watakusema, ni muhimu kujua yeye mwenyewe Faiza alikuwa
anataka nini… Naamini ilikuwa bahati mbaya, ingekuwa ni mimi ile gauni
nisingevaa” >>>> Ally Rehmtullah.
Majibu ya Faiza Ally yako pia kwenye hii sauti niliyorekodi kipande cha Nirvana mtu wangu, unaweza kuplay kumsikiliza mwenyewe.
Comments
Post a Comment