Habari na Mwene Said wa Globu ya Jamii . Maofisa wanane wa Benki Kuu Tanzania (BOT) wamekutwa na kesi ya kujibu na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salam, dhidi ya mashitaka 14 ya kughushi na kuwasilisha vyeti vya kidato cha nne vilivyoghushiwa. Uamuzi huo ulitolewa na Hakimu Mkazi Nyigulila Mwaseba baada ya upande wa Jamhuri kufunga ushahidi wao, dhidi ya washtakiwa Justina Mungai, Christina Ntemi, Siamini Kombakono, Janeth Mahengena Beatha Masawe, Jacquiline Juma, Philimina Mutagurwa na Amina Mwinchumu. Hakimu Mwaseba alisema baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi wa Jamhuri bila kuacha shaka washtakiwa wana kesi ya kujibu na kwamba wanatakiwa kupanda kizimbani kujitetea dhidi ya mashitaka yao. Hakimu alisema kesi hiyo itaanza kusikilizwa utetezi wao Juni 16 hadi 17, mwaka huu. Watumishi hao wa Benki Kuu wanadaiwa kuwa katika kitengo cha kuhesabu fedha vya BoT. Mapema Septemba 19, mwaka 2008, upande wa Jamhuri uliwasomea washtakiwa ha