JE,NI KWELI WEWE HUJITAMBUI? NA KWANINI UNATAKIWA KUJITAMBUA?
- Get link
- X
- Other Apps
Kujitambua
ni uwezo na uelewa wa kujua wewe ni nani, una kusudi gani, wapi na watu
gani kwa muda upi. Ni uwezo wa kujua wapi ulikotoka na wapi unaelekea
na unatakiwa uwe kwenye eneo gani. Je unajitambua?
Asili yako ni nini?
Katika
harakati za kujitambua unaanzia kwenye asili yako, asili yako ni utu
wako, kusudi lako na mpango mzima wa maisha yako. Kama umeelewa asili
yako vizuri ni rahisi kujua wewe unapaswa kufanya nini wapi na watu
gani, ingawa tumekuwa na tatizo la kutokujua wapi tunatoka na tuelewe
wapi tunakwenda na watu gani? Bila kujua tumepoteza mwelekeo wa kile
ambacho tunapaswa kufanya kila siku kufikia kule tunanatakiwa kufika
katika maisha yetu.
Je Utu wako ni nini na unajengwa na nini?
Vijana
wengi tumejikuta tukipoteza dira na maisha wakati mwingine kwa sababu
utu wetu tumewauzia watu wengine kwa kubadilishana na fedha au umaarufu.
Baada ya kuuza utu wetu tumelazimika kufanya mambo ambayo
yatamfurahisha mtu fulani au au watu fulani lakini wakati huo huo
tukiharibikiwa na hatuna mipaka ya namna tunavyoishi. Tumeingia kwenye
mkumbo kwa kuwa hatujui utu wetu umejengwa na nini? Je ni fedha, maadili
ya dini, umaarufu au marafiki zetu?
Je kila unachokifanya kila siku kinaleta msukumo kutoka wapi na kwa kusudi gani?
Msingi wa hicho unachofanya uko wapi?
Haya
ni mambo ambayo hatutafundishwa shule au vyuoni unatakiwa utafute
sehemu nyingine. Ukijifanya ni kipofu na ni upuuzi kuna siku vitu
vinakutokea puani na hujui unaanzia wapi kutatua tatizo. Je malengo ya
maisha yako unayatambua au unaendeshwa na malengo ya watu wengine?
Msingi wako uko wapi?
Kujitambua
ni mwanzo wa wewe kuweza kufikia malengo na kutokuingilia maisha kwa
pupa au kufuata mkumbo. Roma haikujengwa kwa siku moja, hivyo hata
maisha tunayoyatafuta hayatajengwa kwa siku moja ukienda kwa pupa lazima
utapotea bila watu kujua. Tafakari na chukua hatua!
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment