MAAJABU MAZISHI YA KOMBA-TINGATINGA LATUMIKA KUMZIKA
Ndugu na jamaa wakisaidiwa na kijiko cha tingatinga kushusha mfuniko wa zege kwenye kaburi la Mbunge wa Mbinga Magharibi, John Komba aliyezikwa katika Kijiji cha LItuhi, wilayani Nyasa, Ruvuma jana. Picha na Emmanuel Herman Na Joyce Joliga na Ibrahimu Yamola, Mwananchi Nyasa. Safari ya mwisho ya mbunge wa Mbinga Magharibi jana ilihitimishwa saa 9.25 alasiri wakati mwili wake ulipofunikwa na mfuniko mkubwa wa zege uliobebwa na gari maarufu kwa jina la “kijiko”.Haikuwa kitu cha kawaida wakati gari hilo kubwa likishusha mfuniko huo wa zege kwenye kaburi la mwimbaji huyo maarufu wa nyimbo za uhamasishaji za CCM na kiongozi wa kundi la Tanzania One Theatre (TOT), lakini majonzi yaliwafanya waombolezaji kulichukulia tukio hilo kuwa la kawaida.Safari ya Komba, iliyoanza miaka 61 iliyopita kwenye kijiji cha Lituhi ambako aliazikwa jana, ilikamilishwa kwa salamu mbalimbali ambazo zilielezea ushupavu wa kapteni huyo mstaafu wa jeshi. Mazishi hayo yaliyohudhuriwa na