MUME ALIVYOMCHOMA KISU HAWARA,NAYE AJICHOMA UTUMBO WAMWAGIKA NJE,DAMU CHAPAPA
Hawara akipelekwa hospitali baada ya kuchomwa kisi.
Habari
zilizolitikisa Jiji la Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita ni
pamoja na ile ya mkazi wa Chamazi, Hussein Mfaume, kumchoma visu hawara
yake, Ester Thomas Ungele (30), naye kujichoma mpaka kujitoa utumbo,
Uwazi limeichimba kwa kina.
Mume akiwa taabani baada ya kujichoma kisu.
Habari
zilidai kuwa, kisa hasa cha mwanaume huyo kujichukulia uamuzi huo wa
kikatili ni madai ya mwanamke huyo kuwa na uhusiano wa kimapenzi na
mwanaume mwingine anayedaiwa kuwa ni dereva wa teksi.
Kwa
mujibu wa shuhuda wa tukio hilo ambaye ni mtoto wa Ester, Sarah siku
hiyo, yeye na mama yake walikuwa kwenye eneo lao la biashara ya Mama
Lishe, nje ya Ukumbi wa Vijana, Amana uliopo Ilala, Dar.
“Ghafla
nilimwona Hussein akija huku usoni akionekana mtu mwenye hasira.
Alimfuata mama alipokuwa na kumuuliza ni kwa nini anamfanyia dharauMALUMBANO YAANZA, WAKIMBIZANA
Sarah
anaendelea: “Niliona kama malumbano ya kawaida nikawa nawaangalia lakini
nikashangaa kumuona Hussein akimsogelea mama na kutoa kisu.“Mama
alianza kukimbia naye Hussein akamkimbiza huku bado ameshika kisu
mkononi. Niliogopa sana, nikatetemeka. Nilipiga mayowe kumuombea msaada
mama.
“Mama
alikimbia uelekeo wa kuingia kwenye Ukumbi wa Vijana lakini kabla
hajafika, Hussein alimchota mtama mama akaanguka. Ndipo Hussein
alipoanza kumchoma visu mama sehemu mbalimbali za mwili na kisha kumkita
nacho kichwani.”
KISU MWILINI MWAKE
Sarah
tena: “Baada ya kumchoma mama visu hivyo, nilishangaa kumuona Hussein na
yeye akijichoma visu sehemu mbalimbali za mwili wake lakini mwisho
alijikita nacho tumboni na kuanza kukitikisa kama vile alikuwa
anauchanachana utumbo wake, akaishiwa nguvu na kuanguka. Ndipo wasamaria
wema wakaanza kuwasogelea.”
Sarah
alisema hata yeye alisogea eneo hilo na kuwakuta wote wamepoteza fahamu
huku utumbo wa mwanume ukiwa nje na damu chapachapa ikiwa imetapakaa
mwilini. Wakachukuliwa na kukimbizwa Hospitali ya Mkoa wa Ilala, Amana,
Dar ambapo ni mita chache tu kutoka eneo la tukio.
MKE WA HUSSEIN SASA
Naye mke
wa mtuhumiwa huyo aliyejitambulisha kwa jina la Zubeda Abeid alipopata
nafasi ya kuzungumza na Uwazi alikuwa na ya kusema:“Ukweli taarifa hizi
nimezipata kwa mshtuko mkubwa sana hali iliyonifanya nipoteze fahamu.
Hussein ni mume wangu wa ndoa, alinioa mwaka 1997 kijijini kwetu,
Likombora mkoani Lindi. Tuna watoto wanne.
Hawara
aliyechomwa kisu.”Mwaka 2003 tulihamia hapa Dar kutafuta maisha zaidi ya
Lindi, mwenzangu kazi yake ikiwa ni kuuza kahawa pale karibu na huyo
hawara yake aliyemchoma visu. Mimi ni mama wa nyumbani tu.
“Sijui
walihitilafiana kitu gani na huyo hawara yake maana leo ndiyo nimejua
kumbe mume wangu alikuwa na hawara. Lakini hebu soma meseji hii kwenye
simu yangu, alinitumia mume wangu mwanzoni mwa mwezi huu (Februari) bila
kuhofia kuwa mimi ni mke wake.”
ILIVYOSOMEKA MESEJI
“MAMA
NEEMA NAKUOMBA MESEJI HIYO ISOME PEKE YAKO NA USIMWAMBIE MTU YEYOTE.
MIMI NAJIUA KWA SABABU ESTER HANITAKI. WEWE BAKI NA WATOTO, NIMEVUMILIA
KUKUFICHA NIMESHINDWA. KWA HIYO MIMI NAJINYONGA, WEWE BAKI NA WATOTO.”
Baada ya
Uwazi kuzungumza na mwanamke huyo, lilibahatika kuzungumza na dalali
mmoja wa magari anayefanyia shughuli zake eneo hilo lakini aliomba jina
lake lisiandikwe gazetini.
“Hussein
alikuwa akimtuhumu dereva taksi mmoja kwamba anaingilia penzi lake na
mwanamke huyo aliyemjeruhi na amekuwa akiahidi kulipa kisasi.
Mke wa
ndoa.“Yaani leo kama jamaa angekuwepo hapa basi ndiye angekuwa wa kwanza
kuchomwa visu, pengine huyu mwanamke angefuatia,” alisema dalali huyo
aliyeshuhudia tukio hilo.
MGANGA MKUU
Akizungumzia
tukio hilo, Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana, Dk. Shaany Mwaruka
alikiri kuwapokea majeruhi hao na kusema: “Kwa sasa hali za majeruhi
zinaendelea vizuri ingawa awali hali ilikuwa mbaya na kusababisha
wakimbizwe chumba cha upasuaji kutokana na kisu kilichotumika kuingia
sana ndani ya miili.”
Comments
Post a Comment