Katibu Tawala Mkoa Mtwara wa Awaasa Maafisa Habari Kutekeleza Majukumu Yao Kwa Weledi
Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Bw.
Alfred Luanda akisisitiza jambo kwa Mwakililishi wa Idara ya Habari
MAELEZO Bw. Casmir Ndambalilo wakati wa ziara iliyoandaliwa na Chama cha
Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) kwa kushirikiana na
Idara ya Habari MAELEZO katika Mkoa wa Mtwara leo kuona utendaji wa
Vitengo vya Mawasiliano Serikalini pamoja na changamoto zilizopo ili
kuweka mikakati ya pamoja ya kuzitatua hali itakayoimarisha Mawasiliano
Serikali kwa umma katika mkoa huo.
kurugenzi Mtendaji wa Halmashauri
ya Wilaya ya Mtwara Bw. Omari Kipanga akisisitiza jambo wakati wa ziara
iliyoandaliwa na Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini
(TAGCO) kwa kushirikiana na Idara ya Habari MAELEZO katika Mkoa wa
Mtwara leo kuona utendaji wa Vitengo vya Mawasiliano Serikalini pamoja
na changamoto zilizopo ili kuweka mikakati ya pamoja ya kuziondoa hali
itakayoimarisha Mawasiliano Serikali kwa umma katika Halmashuri hiyo
mapema leo.
fisa Habari wa Mkoa wa Mtwara Bw.
Evaristi Masuha akisisitiza jambo kwa Ujumbe kutoka Chama cha Maafisa
Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari MAELEZO
wakati wa ziara yakutembelea vitengo vya mawasiliano Serikalini katika
Mkoa huo mapema leo.
Mwakilishi wa Idara ya Habari
MAELEZO Bw. Casmir Ndambalilo akisisitiza jambo kwa Afisa Habari wa Mkoa
wa Mtwara Bw. Evaristi Masuha mara baada ya Ziara yakutembelea na kuona
changamoto zinazomkabili katika kutekeleza majukumu yake wakati wa
ziara iliyoandaliwa na Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano
Serikalini (TAGCO) kwa kushirikiana na Idara ya Habari MAELEZO
Katibu Tawala Msaidizi
anayeshughulikia Utawala na Rasilimali watu Mkoa wa Mtwara Bw.Renatus
Mongogwela akisisitiza jambo wakati wa ziara ya Ujumbe kutoka Chama cha
Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari
MAELEZO wakati wa ziara yakutembelea vitengo vya mawasiliano Serikalini
katika Mkoa huo mapema leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri
ya Wilaya ya Mtwara Bw. Omari Kipanga (Katikati) akiwa kwenye picha ya
pamoja na Ujumbe kutoka Chama cha Maafisa Habari na Mawasiliano
Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari MAELEZO wakati wa ziara
yakutembelea vitengo vya mawasiliano Serikalini katika Mkoa huo mapema
leo.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya
Mtwara Mikindani ambaye pia ni Afisa Mipango Mji Bi. Mariam Kimolo
(katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Ujumbe wa kutoka Chama cha
Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari
MAELEZO wakati wa ziara yakutembelea vitengo vya mawasiliano Serikalini
katika Mkoa huo mapema leo.
Mwakilishi wa Idara ya Habari
MAELEZO Bw. Casmir Ndambalilo akisisitiza jambo Kaimu Mkurugenzi wa
Manispaa ya Mtwara Mikindani ambaye pia ni Afisa Mipango Mji Bi. Mariam
Kimolo wakati wa ziara ya Ujumbe kutoka Chama cha Maafisa Habari na
Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari MAELEZO wakati wa
ziara yakutembelea vitengo vya mawasiliano Serikalini katika Mkoa huo
mapema leo.
(Picha zote na Idara ya Habari MAELEZO)
…………….
Frank Mvungi- MAELEZO
Maafisa Habari Katika Mkoa wa
Mtwara wametakiwa kutekeleza majukumu yao kwa weledi ili kuimarisha
mawasiliano ya Serikali kwa umma.
Akizungumza na Ujumbe wa chama cha
Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na Idara ya Habari
MAELEZO uliomtembelea ofisini kwake , Katibu Tawala wa Mkoa huo Bw.
Alfred Luanda amesema kuwa jukumu la Maafisa Habari ni kuhakikisha kuwa
masiliano kati ya Serikali na wananchi yanakuwa yakimkakati na
yanayoendana na kasi ya Serikali katika kuwahudumia wananchi.
“ Baadhi ya Maafisa Habari
wanajiweka nyuma na kusahau kuwa wanalo jukumu kubwa la kuuhabarisha
umma kuhusu miradi ya maendeleo inayoteklezwa katika maeneo yao hasa
kwenye Mikoa na Halmashauri” Alisisitiza Luanda
Akifafanua amesema kuwa umuhimu wa
Afisa habari unatokana na namna anavyotekeleza majukumu yake kwa
weledi hasa katika suala la mawasiliano ya kimkakati.
Aidha, alipongeza kazi
zinazofanywa na Idara ya Habari na chama cha Maafisa Habari na
Mawasiliano Serikalini katika kuimarisha mawasiliano ya Serikali kwa
umma.
Kwa upande wake muwakilishi wa
Idara ya Habari – MAELEZO Bw. Casmir Ndambalilo amesema kuwa kila Afisa
Habari ana jukumu la kuisemea Serikali katika Mkoa au Halmashauri ili
kuwapa wananchi fursa ya kuelewa mikakati ya na miradi ya maendeleo
inayoteklezwa katika maeneo yao na kuachana na kasumba ya kufanya kazi
kwa mazoea.
Naye Kiongozi wa ujumbe huo Bi.
Gaudensia Simwanza amesema kuwa kuna haja kwa maafisa habari kupanua
wigo wa utoaji wa taarifa za miradi ya maendeleo kwa wananchi kwa
kutumia mitandao ya kijamii.
Aliongeza kuwa Lengo la chama cha maafisa habari na mawasiliano Serikalini ni kuwajengea uwezo katika kuisemea Serikali.
Ziara ya ujumbe wa chama cha
Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini (TAGCO) katika Mkoa wa Mtwara ,
Lindi na Ruvuma inalenga kuimarisha mawasiliano ya Serikali kwa umma
kwa kuweka mikakati ya pamoja kati ya ujumbe huo Maafisa Habari, na
Viongozi wa ngazi mbalimbali wakiwemo wakurugenzi wa Halmashuri za Mikoa
hiyo.
Comments
Post a Comment