Posts

BREAKING: Wananchi wavamia tena mgodi wa Acacia

Image
Kundi kubwa la wananchi kutoka vijiji vitano vinavyozunguka mgodi wa Acacia North Mara wamevamia mgodi huo. Taarifa kutoka eneo la tukio hivi sasa zinaeleza kuwa wananchi hao wanaendelea kukusanyika katika lango kuu la mgodi huo maarufu Boom Gate huku jeshi la polisi likijaribu kuwatawanya. Hilo ni jaribio la pili kwa wananchi hao kutaka kuingia mgodini humo baada ya lile ya jana ambapo polisi walifanikiwa kulizima. Taarifa zaidi kukujia.

OLE SENDEKA AFUNGUKA HAYA KUHUSU EDWARD LOWASSA,AFICHUA MENGI LIVE

Image
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka amempongeza Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kwa kumpongeza Rais John Magufuli kufuatia uamuzi aliouchukua kuhusu mchanga wa madini yanayochimbwa nchini na kampuni ya Acacia. Ole Sendeka ambaye aliwahi kuwa msemaji wa Chama Cha Mapinduzi, amesema kuwa baada ya kusikia kupitia vyombo vya habari kuwa Lowassa ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema amempongeza Rais, hana budi kumshukuru na kumpongeza pia kwa kufanya hivyo, na kuwaomba wabunge wote bila kujali vyama vyao kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kusimamia kikamilifu rasilimali za nchi. “Nanyi wabunge mkiwa bungeni muungeni mkono Rais wetu Magufuli anavyotetea rasilimali za nchi ili madini yanayochimbwa yaweze kuwanufaisha Watanzania, waweze kupata huduma zao za msingi kupitia madini hayo,” Ole Sendeka anakaririwa na Mwananchi. Mkuu huyo wa Mkoa wa Njombe alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza jana kwenye mazishi ya mama yake mzazi yaliyofanyika

JAJI WARIOBA ASEMA TUMSAIDIE RAIS MAGUFULI KUSHINDA VITA HII YA RASILIMALI ZA NCHI

Image
Hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli alipokea ripoti ya Kamati ya kwanza na ya pili ya uchunguzi wa makontena 277 ya mchanga wa madini (makinikia) yaliyokuwa njiani kusafirishwa nje ya nchi na uchunguzi ulifanyika na kulibaini ndani ya mchanga huo kuna dhahabu na madini mengine kwa asilimia kubwa. Aidha, Mhe Rais amechukua hatua mbalimbali kulingana na ushauri wa kamati husika, pamoja na maamuzi yake kama Rais. Kutokana na sakata la hilo, Idara ya Habari-MAELEZO imepata fursa ya kufanya mahojiano na Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mstaafu Mheshimiwa, Jaji Joseph Sinde Warioba katika ofisi zake zilizopo Osterbay Jijini Dar-es-salaam. SWALI: Ninanukuu maneno ya Baba wa Tafa, Hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere kuhusu raslimali za nchi na hususan madini alisema: “Madini yetu tuliyonayo ni vema kuyaacha mpaka Watanzania watakapokuwa na ufahamu wa kutosha wataamua kuyachimba” mwi

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI AMVAA TUNDU LISSU,AFUNGUKA LIVE

Image
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba ‘amemvaa’ Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu kwamba amejaribu kutengeneza kila aina ya kichaka kukwamisha jitihada za Rais John Magufuli kupambana na usafirishaji holela wa madini nje ya nchi bila mafanikio. Ingawa Mwigulu hakumtaja jina Lissu moja kwa moja alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Zinzirigi kilichopo katika Jimbo lake la Iramba Magharibi pia mkoani Singida juzi, hoja nyingi alizogusia ni zile ambazo Lissu amekuwa akinukuliwa kuzisema. Moja ya hoja hizo ni ile ambayo Mwigulu alisema watu wenye nia mbaya walianza kusema kuwa Serikali itashtakiwa kwa hatua yake ya kuzuia makontena 277 ya mchanga wenye dhahabu. “Baadaye watu haohao walisema tena kwamba mchanga ule ni takataka tu lakini walipoambiwa wasisafirishe mchanga huo wenye madini walisema wanapata hasara ya Sh4 trilioni kwa siku.” Hata hivyo, Acacia walisema wanapata hasara ya dola bilioni moja kila siku. Pia, Mwigulu alise

KIJANA AJINYONGA JUU YA MTI KWA UGUMU WA MAISHA

Image
Matukio ya watu kuchukua maamuzi ya kujiua katika manispaa ya Shinyanga yanazidi kushika kasi ambapo jana Jumapili June 18,2017 majira ya saa 10 alfajiri kijana aitwaye Paulo Ezekiel (17) mkazi wa mtaa wa Mazinge kata ya Ndembezi alifariki dunia kwa kujinyonga kwa kamba juu ya mti jirani na nyumba yao.Inaelezwa kuwa huenda ni ugumu wa maisha ndiyo umechangia kifo cha kijana huyo kwani enzi za uhai wake alikuwa analalamika kuwa maisha ni magumu. Baba mzazi wa marehemu Ezekiel Paulo anasema majira ya saa 10 alisikia mlango wa chumba cha kijana wake ukifunguliwa akadhani pengine ametoka kwenda kujisaidia lakini hakurudi tena ndipo alipoingiwa na wasiwasi na kuanza kumsaka.“Tuliamshana tukaanza kumsaka kila mahali baadaye tukamuona akiwa juu ya mti jirani na nyumba yetu tayari amefariki dunia”, ameeleza Paulo. Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga Jumanne Murilo amethibitisha kutokea kwa tukio. Matukio ya watu kuchukua uamuzi wa kujiua yameanza kukith

Serikali ya China kujenga shule ya usafirishaji nchini

Image
Dar es Salaam. Serikali ya China imesema kuwa ipo kwenye mazungumzo na Serikali ya Tanzania ya kujenga shule ya usafirishaji hapa nchini. Akizungumza leo (Jumamosi) katika hafla ya kutoa ajira kwa wahitimu wa vyuo vikuu hapa nchini iliyoandaliwa na taasisi ya Confucius, Balozi wa China nchini, Dk Lu Youging amesema wakimaliza mazungumzo hayo wataanza ujenzi mara moja. Amesema lengo la ujenzi wa shule hiyo ni kuwaongezea ujuzi wahitimu na wale wasiokuwa wahitimu wa vyuo vikuu. Amesema kwa mujibu wa ripoti ya uwekezaji wa China hapa nchini ni kiasi cha dola bilioni saba huku kampuni zaidi ya 1,000 zikifanya shughuli zake na kutoa ajira 1,200 kwa Watanzania. Kwa upande wake, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan aliyekuwa mgeni rasmi kwenye hafla hiyo amezipongeza kampuni za China kwa kuisaidia Serikali kupambana na changamoto ya ukosefu wa ajira. “Wahitimu wa vyuo vikuu hapa nchini wasiichukulie fursa hii kimzaha bali waifanyie kazi kuhakikisha wanakuwa na weledi

OKWI RASMI SIMBA, KUZIBA NAFASI YA AJIBU.

Image
Wakati mshambuliaji Ibrahim Ajib akiwa anaelekea Jangwani, klabu ya Simba inaonekana kutokuwa na shida juu ya hilo kwasababu tayari ipo njiani kumvalisha Emannuel Okwi Jezi 25 msimu ujao. Okwi ambaye ameshaitumikia Simba kwa vipindi viwili tofauti, ametua Bongo jana usiku na leo mchana nilipata nafasi ya kuzungumza na amethibitisha kwamba yupo katika mazungumzo ya mwisho ya kujiunga na Simba. “Ni kweli nipo kwenye mazungumzo ya mwisho na Simba, naamini tutakubaliana kila jambo na nitasaini kuichezea tena Simba.” – alisema Okwi. Source: Shaffihdauda

MSANII ESTER APANGIWA MJENGO NA MWANAUME

Image
MSANII  wa filamu za Kibongo, Ester Kiama anadaiwa kupangishiwa mjengo na mwanaume ambaye ni mume wa mtu aliyemhamisha ku­toka Kijitonyama alikokuwa anaishi na kumwamishia Mbezi Beach. Chanzo makini kilieleza kuwa kwa sasa Ester anaishi kwenye nyumba nzima yenye hadhi tofauti na alikokuwa akiishi mwanzo ambapo amelipiwa kodi ya mwaka mzima na mwanaume huyo. Risasi Jumamosi  lilimtafuta Ester ili kujibu tuhuma hizo na alipopatikana alikiri kuhamia Mbezi Beach kwenye nyumba ny­ingine nzima lakini ali­pinga suala la kupang­ishiwa na mwanaume. “Ninaishi Mbezi Beach kwa sasa amba­ko nimehamia hivi kari­buni, habari za kwamba nimelipiwa kodi na mwanaume ni uongo, nimejilipia mwenyewe,” alisema Ester.