Posts

RC MAKONDA AKABIDHI ORODHA YA MAJINA 97 YA WAUZA DAWA YA KULEVYA KWA KAMISHNA MKUU WA MAMLAKA YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA JIJINI DAR LEO

Image
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akionyesha majina mengine 97 ya wauza Dawa za Kulevya awamu ya tatu kwa Bw. Rogers William Sianga kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya ili yaanze kushughulikiwa.RC Makonda amesema awamu hii itaitikisa nchi kwani wameanzia toka awamu ya tatu iliyoongozwa na Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, ya nne Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na hii ya Tano inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli, Katika mkutano uliofanyika kwenye ukubi wa Mwalimu Nyerere JNCC Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akikabidhi majina mengine 97 kwa kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa Bw. Rogers William Sianga, kuwa ili yaanze kushughulikiwa.Rc Makond amesema awamu hii itaitikisa nchi kwani wameanzia toka awamu ya tatu iliyoongozwa na Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, ya nne Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na hii ya Tano inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli. Mkuu w

BREAKING NEWZ TID AOMBA RADHI KWA KUTUMIA ‘UNGA’, AWAPA NENO WANAOHOFIA ATAWATAJA

Image
Khaled Mohammed, maarufu kama Top In Dar es Salaam (TID), kwa mara ya kwanza amekiri hadharani kuwa alikuwa anatumia dawa za kulevya na kuwaomba radhi watanzania kwa ujumla. Akizungumza muda mfupi katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam muda mfupi kabla ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutaja orodha ya awamu ya tatu ya wanaotuhumiwa kwa kujihusisha na dawa za kulevya, TID amesema kuwa ameamua kuachana na dawa za kulevya na kwamba sasa anaunga mkono vita dhidi ya dawa hizo. “Nimesimama hapa kama kijana shupavu, mpambanaji na mwenye nguvu mpya. Lakini niko hapa mbele yenu kama mnyama, narudia tena mnyama… na niko tayari kuungana na mapambano dhidi ya madawa ya kulevya,” amesema. “Unapaswa kuwa mnyama kama kaka yangu Makonda ili uweze kuishinda,” ameongeza. Ameongeza kuwa hakuna anayefahamu amepitia mangapi hadi kufikia hapo alipo leo na uamuzi wa kuacha dawa za kulevya akidai kuwa huenda ilihitajika nguvu ya dola kumsukuma

Kajala Afunguka Kutomuona Wema Sepetu Selo

Image
Baada ya Miss Tanzania 2006/07 ambaye ni Mwigizaji wa Bongo Muvi, Wema Isaac Sepetu kusota lupango kwa siku kadhaa kufuatia kutajwa kwenye tuhuma za madawa ya kulevya na Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda, kabla ya kupandishwa mahakamani na kuachiwa kwa dhamana, staa mwenzake, Kajala Masanja ameibuka na kufunguka sababu ya kutokwenda kumuona mahabusu. Kajala, akiwa ni rafiki wa Wema, aliwahi kuokolewa kwenda jela na mrembo huyo baada ya kumlipia faini ya shilingi milioni 13, anadaiwa kutofika lupango katika Kituo Kikuu cha Polisi ‘Central’ jijini Dar alikokuwa ameshikiliwa Wema, jambo ambalo liliwashangaza wengi. Chanzo makini kililieleza Wikienda kuwa, kitendo cha kutokwenda kumuona wala kufika mahakamani siku aliyopandishwa kizimbani, kilimuumiza Wema na ndugu zake kwani hawakutegemea mtu kama Kajala angeshindwa kufika kumuona na kumsapoti shosti wake huyo. Katika mitandao ya kijamii, gumzo lilikuwa ni Kajala kutokwenda selo kumuona Wema hadi akatoka huku watu

HAWA NDIO WALIOTIWA MBARONI KWA TUHUMA ZA KUHUSIKA NA BIASHARA YA DAWA ZA KULEVYA MKOANI KILIMANJARO

Image
Baadhi ya watuhumiwa wa dawa za kulevya waliokamatwa katika msako uliofanyika kwa muda wa siku nne. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi Mwandamizi,Wilbroad Mutafungwa akitaja majina ya watu wanadaiwa kujihusisha na usafirishaji,uuzaji na matumizi ya dawa za kulevya. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini. JESHI la Polisi mkoa wa Kilimanjaro limetaja majina ya watu 47 wanaotuhumiwa kuhusika katika kusafirisha,kuuza na kutumia dawa za kulevya huku likifanikiwa kukamata misokoto 269 na miche 13 ya Bhangi,pamoja na kilogramu 32.9 za mirungi pia ikikamatwa. Kukamatwa kwa watuhumiwa hao pamoja na dawa hizo za kulevya kunatokana na msako mkali uliofanywa na kikosi maalumu cha jeshi hilo kwa muda wa siku nne katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kilimanjaro . Akitangaza majina hayo ofisini kwake ,Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro ,Kamishna Mwanadamizi Msaidizi wa Polisi,Wibroad Mutafungwa alisema watuhumiwa

RAIS JOHN MAGUFULI LEO AMEMTEUA ROGERS W. SIANGA KUWA KAMISHNA MKUU WA MAMLAKA YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA.

Image

MAKAMU WA RAIS AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI MJINI DODOMA LEO

Image
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri katika ukumbi wa TAMISEMI mjini Dodoma leo.   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipitia baadhi ya ajenda wakati  kikao cha Baraza la Mawaziri mjini Dodoma.  Mawaziri wakijadiliana jambo kabla kikao cha Baraza la Mawaziri hakijaanza kutoka kushoto ni Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako, Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage. Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Mwigulu Nchemba(kushoto), Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama (katikati) wakizungumza jambo na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango muda mfupi kabla ya kuanza kikao cha Baraza la Mawaziri mjini Dodoma. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Ma

UPDATES: IDD AZZAN AWASILI KITUO CHA POLISI CHA KATI KWA AJILI YA MAHOJIANO

Image
Mbunge wa zamani wa Kinondoni, Iddy Azzan ameripoti katika kituo cha polisi cha kati kama aliyotakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Azzan amewasili kituoni hapo muda wa saa 09:06 kwaajili ya mahojiano na polisi baada ya kutakiwa kufanya hivyo na mkuu wa mkoa. Azzan ni miongoni mwa watu 65 waliotajwa na mkuu wa mkoa juzi kutakiwa kufika polisi jijini Dar es Salaam. Jana. Askofu wa kanisa la ufufuo uzima Josephat Gwajima na mfanyabiashara maarufu, Yusuf Manji ambao nao wapo katika orodha hiyo ya mkuu wa mkoa waliripoti.Kamanda wa Kanda Maalumu, Simon Sirro amesema ifikikapo saa 7 mchana atazungumza na waandishi wa habari.

FREEMAN MBOWE AGOMA KWENDA KUHOJIWA POLISI ASEMA MAKONDA HANA MAMLAKA HAYO

Image
Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Aikaeli Mbowe amesema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda hana mamlaka ya kumuita kwenda Kituo cha Polisi.  Mbowe ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Mjini Dodoma kufuatia kutajwa katika orodha ya watuhumiwa 65 wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya na kutakiwa kufika Kituo cha Polisi cha Kati jijini Dar es Salaam leo saa tano asubuhi. Mbowe amekanusha vikali tuhuma hizo za kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya na kusema kuwa anachokifanya RC Makonda ni kuwaepusha watuhumiwa wa kweli wa dawa za kulevya na mikononi mwa sheria. Aidha, Mbowe amesema kuwa yupo tayari kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi muda wowote endapo njia sahihi zitakapofuatwa.  Pia amesema atamfungulia mashtaka RC Paul Makonda kwa kumchafulia jina lake kufuatia kumtuhumu kwa biashara ya dawa za kulevya. Kiongozi huyo wa Kambi ya Upinzani Bungeni a

Jeshi la Polisi Dar Lamjibu Mbowe……Lasema Kama Hataripoti Polisi, Basi Litamfuata Popote Alipo.

Image
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema kama Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe hataripoti bila kutoa taarifa yoyote ya udhuru atafuatwa kwa kuwa jeshi hilo linahitaji  kumhoji. Kamanda wa kanda hiyo, Simon Sirro amesema hayo leo muda mfupi baada ya Mbowe kueleza kuwa hataripoti polisi kutokana na wito wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Amesema operesheni dhidi ya mihadarati bado inaendelea na kuanzia sasa hawataruhusu tena mkusanyiko wa watu katika kituo cha polisi kati na wale watakaoonekana watashughulikiwa hivyo asije kulalamika mtu kwani taarifa imeshatolewa. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ametangaza rasmi kutofika kituoni hapo kwa madai kuwa hawezi kwenda polisi kwa wito wa Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda isipokuwa pale tu taratibu za kisheria zitakapofuatwa.

STAA WEMA SEPETU KUONANA USO KWA USO NA ZARI THE BOSS LADY

Image
Akizungumza live kutoka Clouds Fm, Diamond ametamka rasmi kuwa staa Wema Sepetu ni miongoni mwa wageni waalikwa kwenye sherehe hiyo, kwa upande wa Zari Hassan nae amesema hana shida na ujio wa Wema Sepetu Kwenye Arobaini ya Nillan ambaye waliwahi kuingia kwenye bifu kipindi cha nyuma. Kama kweli Wema akifanikiwa kuhudhuria kwenye sherehe hiyo itakua ndo mara ya kwanza kwa mafahari hao wawili kuonana, na itakua sherehe ya aina yake kwa uwepo wa mastaa hao waliowahi kuingia kwenye vita nzito na kurushiana maneno mtandaoni

MUME AMKATA MASIKIO MKE WAKE, SABABU YATAJWA KUWA AMEMCHOKA

Image
Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Zarina mkazi wa mji wa Balkh, Afghanistan amekatwa masikio na mume wake kwa madai kuwa mume wake amemchoka na hataki kuishi nae. Akielezea tukio hilo la kikatili, Zarina alisema amedumu na mwanaume huyo kwa muda wa miaka saba na tukio hilo lilitokea wakati akiwa amelala usiku lakini ghafla aliamka na kukuta akifanyiwa tukio hilo.“Sikuwa nimemfanyia jambo lolote baya, sijui kwanini mme wangu alinifanyia hivi … mahusiano yetu hayakuwa mazuri,” alisema Zarina.Mwanamke huyo mwenye miaka 21 aliongeza kuwa mume wake amekuwa akimfanyia vitendo vya kikatili kwani kuna kipindi alimzuia hata kwenda kuwatembelea wazazi wake.Aidha Zarina alizungumza kuhusu mpango wake wa baadae kama ataendelea kuishi na mwanaume huyo na kusema, “Sihitaji tena kuishi nae.” Zarina kwasasa anapatiwa matibabu katika moja ya hospitali iliyopo Balkh na Polisi mjini humo wamesema mume wake amekimbia na juhudi za kumtafuta zinafanyika ili hatua za kisher

MZEE WA UPAKO NAE AFUNGUA HAYA KUHUSU MADAWA YA KULEVYA

Image
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) Ubungo-Kibangu jijini Dar, Lusekelo Anthony ‘Mzee wa Upako’ amejitaja kuwa ni mmoja kati ya watu mashuhuri ambao wamewahi kutuhumiwa kuhusika na biashara ya dawa za kulevya. Amefunguka na kusema kuwa yeye ni mhanga wa suala hilo jambo ambalo lilimpa wakati mgumu sana katika maisha na kumfanya kunyanyapaliwa na jamii pamoja na watu wake wa karibu wakiwemo wachungaji wenzake. Mchungaji Lusekelo amesema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachofanyika kupitia ukurasa wa facebook wa EATV kila Jumatano. “Mimi ni mhanga wa dawa za kulevya mwaka 1997 nilituhumiwa kuwa nauza madawa, lakini wale askari walikuwa wastaarabu, waliniandikia samasi nikafika kutoa maelezo yangu, lakini baadaye niliwaambia kuwa wao ni polisi wafanye uchunguzi wao, walifanya uchunguzi na kugundua mimi sihusiki, watu walifuatilia na kugundua siyo kweli, na kila mtu akajitoa kwenye, ilionekana kuwa ni wivu tu, ila mbaya zaidi ile

SAKATA LA DAWA ZA KULEVYA ASKOFU GWAJIMA ATEMA CHECE ,ADAI DC MAKONDA ANATUMIKA

Image
Gwajima:   Nakumbuka Kuna siku Makonda alikuwa anahutubia, akamwambia Waziri mkuu eti nlipiga marufuku shisha lakini imerudi, hawa wavuta shisha waliniletea Milion 5 nikakataa akasema lakini naamini kamanda Siro hizi milioni tano tano zimepita kwao. Makonda alidiliki kumtuhumu Waziri MKuu eti Karudisha Shisha!?. DC Makonda ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar, kwanini hakuisemea kwenye Vikao, Kwanini alisubiri Media? Gwajima:   Safari hii kamfikia kiongozi wa Kiroho, huu ni unafiki sana. Huweze kumuita rafiki yako kaka yako namna hii. Gwajima:   Sasa leo nataka niwambie kwanini Makonda anafanya hivi; 1. Nataka niwambie, Rais hajamtuma Makonda atutuhumu sisi 2. System za Serikali zimeparalyse kwa sababu watendaji wa Serikali na Mawaziri wanamuona Makonda ni Mkono wa kiume wa Rais. Wanafikiri labda kwakuwa Makonda ni Msukuma basi atakuwa anatumwa na rais, Rais hawezi kufanya hivyo. Mawaziri wamekosa neno wamekaa Kimya. Gwaji

MANJI AJISALIMISHA POLISI

Image
Mwenyekiti wa klabu ya Yanga ,Yusufu Manji akiwasili katika kituo cha Polisi Kati jijini Dar es Salaam mara baada ya kuamua kujipeleka hapo yeye kwa ajili ya kuhojiwa baada ya kutajwa kwenye watu wanaotuhumiwa na madawa ya kulevya. Yusufu Manji akipokelewa na baadhi ya wanachama wa Yanga katika kituo cha Polisi kati mara baada ya kujipeleka leo badala ya kesho Manji akisalimiana na wanachama wa Yanga katika kituo cha Polisi Kati Mnaji akiwa akiwa ameongozana na mawakili wake na wasaidizi kuingia kituo cha kati jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Yanga Yusufu Manji akisalimiana na Waandishi wa Habari jijini Dar ess Salaam katika kituo cha Polisi Kati