Posts

Wabunge wengine wasimamishwa kuhudhuria vikao leo June 17 2016

Image
Leo June 17 2016 idadi ya wabunge kusimamishwa imeongezeka baada ya Naibu Sika, Tulia Ackson kutangaza kusimamishwa kwa wabunge wawili ambao ni Mbunge wa viti Maalum CHADEMA Suzan Lyimo na Anatropia Theonest. Mbune Suzan Lyimo amesimamishwa na Bunge kuhudhuria vikao vitano vya Bunge baada ya kubainika kusema uongo kwamba Jeshi la polisi nchini limenunua magari 777 ya washawasha wakati ukweli ni kwamba hiyo ni Idadi ya magari inayopangwa kuingizwa na jeshi hilo kwa ajili ya matumizi mbalimbali. Licha ya Mbunge kuonesha ushirikiano kwa kamati ya maadili, haki na madaraka ya bunge, kamati imemwona Mbunge ni mzoefu wa shughuli za bunge hivyo anapaswa kusimamishwa vikao hivyo kuanzia June 17 hadi 24 mwaka huu. Aidha Mbunge Anatropia Theonest amesimamishwa kuhudhuria vikao vitatu vya bunge kwa kosa la kulidanganya Bunge kuwa waziri wa ardhi na nyumba William Lukuvi alichukua ardhi ya wananchi akiwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam.

Unawafanyia nini wazazi wako kipindi hiki wakiwa hai?

Image
Amrani Kaima A ssalam aleikum mpenzi msomaji wangu. Uhali gani wewe uliyepata bahati ya kunisoma tena wiki kupitia ukurasa huu? Ni matumaini yangu kwamba kwa rehema zake Mwenyezi Mungu umzima na unaendelea vyema na mishemishe zako za kimaisha. Mimi nitakuwa mchoyo wa shukurani kama sitatumia fursa hii kumshukuru Mungu kwa kila ambalo amekuwa akinitendea katika kila siku ya maisha yangu. Niseme tu kwamba Mungu ni mwema sana kwangu. Mpenzi msomaji wangu, najua Waislam wako katika mfungo wa Mwenzi Mtukufu wa Ramadhani na wale wanaofuatilia safu hii watakumbuka niliwahi kuzungumzia suala la kila mmoja kuiheshimu imani ya mwenzake. Asitokee hata mmoja wa kujiona yeye ni bora zaidi ya mwingine au kwamba yeye ndiye ambaye yuko kwenye mstari ulionyooka. Wote  tuko sawa na sote ni ndugu, tofauti zetu za kiimani, kikabila na kirangi zisitufanye tukafarakana. Baada ya kusema hayo nirudi sasa kwenye mada yangu ambayo nimedhamiria kukuletea kwa wiki hii. Nawazungumzia

WATANZANIA WATAKIWA KUTUMIA FURSA ZA SOKO LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

Image
Na. Immaculate Makilika- MAELEZO, Tarehe 16.06.2016 WAFANYABIASHARA wa Tanzania wametakiwa kutumia fursa za biashara zinazopatikana katika soko la nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kuuza bidhaa zao ndani ya Jumuiya hiyo.Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari. “Wafanyabiashara wanatakiwa kuchangamkia fursa ya biashara katika soko la pamoja kwa kuwa ni haki yao na ni utekelezaji wa malengo ya Mkataba wa uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kifungu cha tano ambapo ilianzishwa itifaki ya umoja wa forodha ” ,alisema Bi. Mindi Wafanyabiashara hao pamoja na wasafirishaji wanaotaka kufanya biashara katika soko la Jumuiya hiyo watatakiwa kuonesha cheti cha uasilia wa bidhaa wakati wakiingia nchi wananchama wa Jumuiya hasa kwa wafanyabiashara wadogo wenye bidhaa zisizozidi dola za kima

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ALIPOKUWA AKIJIBU MASWALI BUNGENI LEO MJINI DODOMA

Image
Wabunge wa Upinzani wakitoka Bungeni baada ya dua kusomwa na Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson Juni 16, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu maswali bungeni mjini Dodoma Juni 16, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri .kuu) Wageni waliofika Bungeni mjini Dodoma kujionea shughuli  mbalimbali za bunge wakifuatilia kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu  Juni 16, 2016. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiteta na Mbunge wa Nkansi Kaskazini, Ally Kessy bungeni mjini Dodoma Juni16, 2016. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa zamani wa Singida mjini , Mohammed Dewji kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni 16, 2016.

Amfumania mume, achoma nyumba!

Image
  Monika akiwa amezimia. Waandishi wetu, Amani Dar es Salaam: Mapenzi uchizi! Hii ndiyo kauli pekee unayoweza kuitumia baada ya mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Monika, mkazi wa Tabata-Senene jijini Dar, kudaiwa kumfumania mumewe na mchepuko ndani kwake kisha kuchoma moto nyumba kabla ya kuzimia. Nyumba ilivyochomwa moto. Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo lililojaza umati, sekeseke hilo lilijiri wiki iliyopita, mishale ya saa 5:00 asubuhi nyumbani kwa wanandoa hao maeneo hayo ambapo mwanamke huyo hakuwepo nyumbani hivyo aliporudi ndipo akaanzisha timbwili, akidai kumkuta mumewe ndani na mchepuko. “Unaambiwa baada ya Monika kurudi nyumbani na kumfuma mumewe ‘akimalizana’ na mchepuko, palikuwa hapatoshi. “Monika aliangusha timbwili la aina yake lakini yule mchepuko alifanikiwa kutoka nduki. “Kutokana na hasira, Monika alijifungia ndani, akamwagia nyumba mafuta ya taa, akawasha moto akitaka kujitoa uhai. “Tunashukuru Mungu, askari wa zima moto walifika na kufan

Huzuni…Familia ya Hoyce yanusa kifo ajalini

Image
Mama mzazi wa Hoyce Temu IMELDA MTEMA, Amani Dar es Salaam: Familia ya Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu akiwemo mama yake mzazi, dada zake watatu na mdogo wake, wamenusurika kupoteza maisha baada ya gari walilokuwa wakisafiria, kupata ajali mbaya kwenye makutano ya Barabara za Ali Hassan Mwinyi na ile ielekeayo kwenye Ufukwe wa Coco, Amani linakujuza. Ajali ilivyotokea Akizungumza kwa masikitiko, Hoyce alisema ajali hiyo ilitokea mchana wa Jumapili iliyopita wakati wanafamilia hao wakielekea Ufukwe wa Coco kwa ajili ya kupata chakula cha mchana ambapo ghafla, gari jingine aina ya Range Rover Vogue, lililigonga gari walilokuwemo ndugu zake na kuwasababishia madhara makubwa. Hoyce aliongeza kuwa alipata taarifa za kupata ajali ndugu zake hao wakati akiwa Bagamoyo, Pwani kwenye kambi ya watoto wenye ulemavu wa ngozi. Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu Mrembo huyo alisema kuwa alipigiwa simu na dada yake mkubwa aitwaye Edith aliyekuwa kwenye ajali hiyo na kumtaarifu kwamba wamep

Manji apiga hodi kwa JPM

Image
Dar es Salaam. Kama ulidhani lile sakata la ufukwe wa Coco Beach uliopo kandokando mwa Bahari ya Hindi jijini Dar es Salaam linalomhusisha Mwenyekiti wa Kampuni za Quality Group Limited (QGL), Yusuf Manji limemalizika, elewa kwamba bado. Manji amezungumza mambo mengi na gazeti la Mwananchi, lakini akasema bado anasubiria majibu yake kutoka kwa Rais John Magufuli baada ya kumwandikia barua Desemba, mwaka jana. Mfanyabiashara huyo ambaye anatarajiwa kustaafu uongozi katika kampuni hiyo mwezi ujao, amesema anatamani kuona suala hilo linamalizika haraka.

Kutoka Arusha: Mbaroni kwa kutupa mapacha

Image
Mtuhumiwa Happiness Joel JOSEPH NGILISHO, Amani ARUSHA: AMENASWA! Msako uliofanywa na wananchi wa Kitongoji cha Namayana, Kata ya Kiranyi wilayani Arumeru mkoani hapa, kufuatia tukio la mwanamke kudaiwa kutupa vichanga mapacha, umefanikiwa kumnasa mtuhumiwa Happiness Joel (29), tembea na Amani. Mwenyekiti wa kitongoji hicho, Elias Naigisa akizungumza na gazeti hili mwanzoni mwa wiki hii, alisema June 7, mwaka huu alipata taarifa ya kutupwa kwa vichanga viwili katika chemba ya choo kinachomilikiwa na mkazi wa kitongoji hicho, Elibariki Loti. Alisema baada ya taarifa hiyo, yeye na wananchi walikwenda kushuhudia na kukuta vichanga hao  wamefariki dunia na kutoa taarifa kwa jeshi la polisi huku yeye na wananchi wake wakianzisha msako mkali kumbaini mwanamke aliyekuwa na ujauzito. “Polisi walifika na kuchukua miili ya vichanga hao na kwenda kuihifadhi katika chumba cha maiti katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru kusubiri uchunguzi,” alisema mwenyekiti huyo. Akipandishwa k

MANENO MUME ALIYOMWAMBIA MKE WAKE USIKU BAADA YA SHEREHE YA HARUSI YAO.

Image
   "Mke wangu, watu wote wameenda nyumbani kwao , mziki umezimwa, shamrashamra zimeisha. Harusi yetu ilikua nzuri mno ila sasa imepita. Tumemaliza harusi sasa ni muda wa kujenga familia yetu. Tuliobaki baada ya harusi hii ni mimi na wewe tu peke yetu. Hatma ya kesho huanza leo. Maisha yetu sasa sio kama ya nyuma ... . Nakumbuka kuna kipindi ulivaa gauni jekundu, lilikupendeza sana, siku ile nlitaman kukugusa, tulikua kwenye maonyesho ya sinema nilikua na shauku kubwa sana kwako. Nilitamani japo kukusogeza upande wa chooni ili nikakubusu tu ila haikuwezekana. Niliumia sana moyoni. Ila sasa wajua nini siri ya furaha yangu? Jibu la siri ya furaha yangu ni kuwa sasa nimekupata, niko na wewe pamoja milele, naweza sasa kukubusu kila siku. Kabla sijakuvua nguo na kufanya mapenzi na wewe kwanza ngoja nikuambie vitu vichache vya muhimu mno......... Sina cha kukuficha, kuanzia leo simu yangu waeza kuitumia kama yako pia waeza tumia account na profile zangu Facebook, whatsapp na ins

NJIA RAHISI KUSOMA QUR-AN YOTE KATIKA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI

Image
  Qur’an ina juzuu thelathini sawa na siku thelathini za mwezi, hivyo kwa kusoma juzuu moja kila siku inatosha kutimiza Qur’an yote kwa mwezi, ikumbukwe pia Qur’an (mas’haf) ina kurasa kati ya 604–612. Inahitaji kusoma kurasa ishirini kwa siku kwa muda wa siku thelathini kumaliza msahafu mzima. Siku moja ina swala tano, zikigawiwa kurasa ishirini kwa swala tano zinapatikanaka kurasa nne katika kila swala. zikigawiwa kurasa nne kwa mbili, yaani itakuwa kurasa mbili kabla ya swala na mbili baada ya swala, ni kiasi chepesi kwa mtu kuisoma Qur’an nzima ndani ya mwezi. Kwa wale ambao hawana muda wa kusoma kurasa nne kila swala, hebu tujaribu hii. Tusome kurasa saba baada ya swala ya sub’hi (alfajir), saba baada ya swala ya laasiri na saba baada ya taraweeh (swala ya Isha). Hivyo itakuwa saba mara tatu ambayo ni sawa na 21. 21 mara siku thelathini ni 630 yaani msahafu na zaidi. Ikumbukwe tabia hujenga mazoea, hebu chagua hesabu moja na uanze nayo mazoezi katika maisha, Mwisho wa s

Usome Hapa Waraka wa Edward Lowassa kwa IGP Mangu

Image
Mhe. Edward Ngoyai Lowassa. Kwako Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Salaam, Kwanza niwie radhi kwamba nimelazimika kwa nafasi yako na yangu, kukiuka taratibu za kiitifaki hata nikalazimika kuandika waraka huu kwako. Ninafanya hivyo si kwa sababu yoyote, bali kwa sababu tu jambo au mambo yaliyonisukuma kukukifikishia ujumbe huu, yana uzito mkubwana kimsingi yanaweza kuathiri mustakabali mwema wa kitaifa. Msingi wa waraka wangu huu ni agizo ulilotoa wewe, Inspekta Jeneraliwa Polisi la kupiga marufuku mikutano ya hadhara ya kisiasa namaandamano ya vyama vya upinzani. Ni bahati mbaya kwamba wakati ukitoa maagizo hayo, nilikuwa niko njeya nchi, ingawa kwa bahati njema, Watanzania wenye mapenzi mema nataifa lao waliopo hapa nchini na nje, walinifikishia taarifa juu ya agizolako hilo. IGP, siyo desturi yangu kuandika waraka wa namna hii mtandaoni au kupitia vyombo vya habari, ingawa safari hii nimelazimika kufanyahivyo ili kuweka rekodi sahihi, sambamba na kukosoa sababu ulizotoakuwa

Mbunge wa Ukonga Ashinda Kesi ya Uchaguzi

Image
    Mbunge wa Jimbo la Ukonga (Chadema), Mwita Waitara (kulia) akitoka mahakamani. (Picha na Maktaba). Mbunge wa Jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mwita Waitara leo ameshinda kesi ya uchaguzi iliyokuwa imefunguliwa na mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jerry Silaa. Hukumu hiyo imetolewa leo muda mfupi uliopita na Jaji Fatma Msengi wa Mahakama Kuu ya Dar es Salaam.

Wolper nusura apigwe risasi ‘sheli’

Image
Jacqueline Wolper. NA MUSA MATEJA, RISASI MCHANGANYIKO DAR ES SALAAM: Chupuchupu! Mwanadada anayeng’ara kunako tasnia ya filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper, juzikati almanusra apigwe risasi kwenye kituo kimoja cha mafuta kilichopo Tegeta (jina linahifadhiwa) jijini Dar es Salaam, baada ya kuibuka kwa timbwili zito eneo hilo, Risasi Mchanganyiko linakupa mkasa mzima. Tukio hilo la aina yake, lilijiri mishale ya saa tano usiku wa Juni 12, mwaka huu ambapo kwa mujibu wa chanzo chetu cha kuaminika, Wolper alinusurika kupigwa risasi na mlinzi wa kituo hicho cha mafuta baada ya kutokea hali ya sintofahamu kati yake na mfanyakazi mmoja kwenye kituo hicho. “Ishu yenyewe ni kwamba, kuna muda Wolper alifika pale sheli (Sheli ni neno lililozoeleka likimaanisha kituo cha mafuta, lakini ukweli ni kuwa jina hilo ni la kampuni ya mafuta yenye makao makuu yake Nchini Marekani) akiwa ndani ya gari aina ya Toyota Mark X, lile linalodaiwa kuwa ni la mpenzi wake wa sasa, Harmonize (Rajab

ANGALIA RATIBA YA LIGI KUU ENGLAND MSIMU 2016/2017

Image
  Kama wewe ni shabiki la Ligi Kuu England ratiba ya Ligi kwa ajili ya msimu wa 2016/2017 imetoka, rasmi sasa Ligi Kuu England msimu wa 2016/2017 itaanza kuchezwa rasmi Jumamosi ya August 13 2016, bingwa mtetezi wa Leicester City ataanza kwa kucheza na Hull City. Unaweza bonyeza  HAPA  kupata ratiba yote. A

Ukweli afya ya Spika Job Ndugai

Image
Spika wa Bunge, Job Ndugai. KUFUATIA uvumi wa mara kwa mara kwenye mitandao ya kijamii juu ya kufariki dunia kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai, Risasi Mchanganyiko limetafuta na kufanikiwa kupata ukweli juu ya afya ya kiongozi huyo mkuu wa wabunge Tanzania. Awali, kulikuwa na taarifa katika mitandao ya kijamii, ikitoa madai hayo, hasa kutokana na kutoonekana kwa muda mrefu kwa Spika akiongoza vikao vya Bunge vinavyoendelea kujadili bajeti kuu ya serikali mjini Dodoma. Kutotolewa kwa maendeleo ya afya yake ndilo jambo linalowafanya wengi kuziamini taarifa hizo za mitandaoni na hivyo kupiga simu chumba cha habari kutaka kujua uhakika wake hasa kwa kuwa hii siyo mara ya kwanza kwa Spika kwenda nchini humo kuangaliwa afya yake. Gazeti hili lilimtafuta Katibu wa Bunge, Thomas Kashililah ili kupata ufafanuzi wa taarifa za mitandao zilizokuwa zikitembea juzi (Jumatatu) kuwa mbunge huyo wa jimbo la Kongwa mkoani Dodoma amefariki, lakini simu yake haikupo-kelewa. Lakini Kaimu Katibu wa

Pichaz 15: CRDB wamemkabidhi Paul Makonda milioni 100

Image
  Baada ya Rais Magufuli kutangaza elimu bure kuanzia elimu ya msingi mpaka kufikia kidato cha nne, kumekuwa na changamoto kubwa ya uhaba wa madawati ambapo Serikali ilianzisha kampeni ya uchangiaji wa madawati, leo June 14 2016 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam   Paul Makonda  amepokea milioni 100 kutoka Bank ya CRDB kwa ajili ya manunuzi ya madawati katika Mkoa wa Dar es Salaam , ‘ Nimeshaongea na wakuu wangu wote wa Wilaya popote pale ambapo upo waje na mimi kama Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam nitapokea chochote kile hata kama liwe ni dawati moja nitalipokea ‘ >>> Paul Makonda

Aina mbalimbali ya maumivu ya tumbo

Image
Kuna hali nyingi zinazoweza kusababisha maumivu ya tumbo. Chanzo cha maumivu hutegemea na sehemu maumivu yalipo. Maumivu chini ya mbavu: Kulia yanaweza kusababishwa na mawe kwenye mfuko wa nyongo, maambukizi kwenye mfuko wa nyongo Cholecystitis , uvimbe wa ini, jipu kwenye ini, saratani ya kongosho na kifuko cha nyongo. Maumivu chini ya chembe ya moyo: Husababishwa na vidonda vya tumbo, kiungulia, saratani ya tumbo na saratani ya kongosho. Maumivu pembeni mwa kitovu: husababishwa na mawe ya figo Kidney Stones, maambukizi ya figo, Pyelonephritis na  maambukizi kidoletumbo Acute Appendicitis Maumivu chini ya kitovu: huweza kusababishwa na maambukizi ya mfumo wa mkojo, magonjwa ya zinaa kama klamidia, PID, vivimbe vya mji wa uzazi, mimba kuharibika na saratani ya kibofu cha mkojo. Maumivu ya tumbo: Ni utumbo kujiziba Intestinal Obstruction,  utumbo kujisokota Volvulus, kula sumu na  mzio wa chakula fulani au ugonjwa wa Crohn Crohn’s Disease,  Ngiri Hernia au homa ya tum

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AGAWA FUTARI KWA WATU WENYE MAHITAJI MAALUM NA KUJIONEA MABASI YA MWENDO KASI

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiteremka kwenye basi la mwendo kasi baada ya kupanda na kujionea ubora na uzuri wa mabasi hayo ambayo yamerahisisha usafiri kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam.( Picna na OMR) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa shughuli ya kukabidhi Futari na Chakula kwa watu wenye mahitaji maalum katika ofisi za UDA-RT Jangwani jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki dua maalumu wakati wa shughuli ya kukabidhi Futari na Chakula kwa watu wenye mahitaji maalum katika ofisi za UDA-RT Jangwani jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akiongoza dua hiyo Mussa Salum . Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Futari Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa Baraza la Waislam mkoa wa Dar es Salaam Bibi Pili Abdala Mwale wakati wa shu