Posts

BREAKING NEWS : TUHUMA ZA RUSHWA KAMATI ZA BUNGE: Mbunge Zitto amejiuzulu

Image
Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, ameishtumu Kamati ya Huduma za Jamii anayohudumu kuwa kuna baadhi ya Wajumbe hupokea rushwa. Kutokana na shtuma hizo ameamua kumuandikia spika kumtaka achunguze na kuchukua hatua. Kauli yake ianapatikana hapa chini; "Kuna tuhuma za rushwa dhidi ya Kamati mbalimbali za Bunge ikiwemo kamati ninayohudumu. Nimemwandikia Spika Kuomba Uchunguzi juu Ya tuhuma hizo na kwamba achukue hatua kali dhidi ya yeyote atakayekutwa kuhusika na vitendo vya rushwa. Nimejiuzulu Ujumbe wa Kamati ili Kutoa Nafasi Ya Uchunguzi Husika.

Uchaguzi wa Meya Dar: Isaya C. Mwita(CHADEMA) aibuka mshindi

Image
Huyu ndiye Meya wa Jiji la Dar es salaam. Meya wa jiji la Dar es Salam, Isaya Charles akisaini. eo ndo siku ya uchaguzi wa Meya wa jiji la Dar es salaam. Viongozi wakuu wa UKAWA wameshawasili ukumbini. Viongozi wa UKAWA wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chadema taifa Freeman Mbowe, Katibu Mkuu wa Chadema Dk.Mashinji, Naibu wa katibu wakuu; Salum Mwalimu na John Mnyika, pamoja na aliyekuwa mgombea uraisi na PM mstaafu Mhe. Edward Lowassa wameshawasili ukumbini. Ikumbukwe kuwa ombi la CCM la kuahirisha uchaguzi lilitupiliwa mbali na mahakama hapo jana na kuruhusu Uchaguzi huu ufanyike leo. Muda huu taratibu zinaendelea ukumbini, tutawajuza.. Picha viongozi wa UKAWA wakiwa ukumbini kusubiri taratibu zinaendelea. - Kituko cha mwaka madiwani 5 wa CCM wameingia mitini hawajaonekana ukumbini.

Updates: Uchaguzi wa Meya Jiji la Dar

Image
Mh. Edward Lowassa na Godbless Lema wakiwasili Ukumbi wa Karimjee kunakofanyika uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es salaam leo. Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt Vincent Mashinji (aliyesimama katikati) na Makamu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalim (wa kwanza kutosho) na baadhi ya wajumbe wakiwa nje ya Ukumbi wa Karimjee ambapo wamefika kufuatilia uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es salaam Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt Vincent Mashinji wa kwanza kushoto akijadiliana jambo na baadhi ya wajumbe. Maofisa wanaosimamia uchaguzi huo wakikagua taarifa za wajumbe wanaositahili kuingia ukumbini kwa ajili ya kumchagua Meya wa Jiji la Dar. Hali ilivyo ndani ya Ukumbi wa Karimjee ambapo uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam unafanyika. Baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kuamuru uchaguzi wa Meya na Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam, kufanyika leo kama ilivyopangwa. Baadhi ya wajumbe wanaoshiriki uchaguzi huo wamefika ukumbini Karimjee ambapo uchaguzi huo unaf

KASI YA MAGUFULI YAMPA KIWEWE MKUU WA WILAYA YA IRAMBA,AMEAMUA KUJISALIMISHA KABISA HATAKI TENA UKUU WA WILAYA

Image
Wakati Taifa likisubiri uteuzi wa wakuu wa wilaya huku wanaoshikilia nafasi hizo wakiwa katika chekeche kwa kuzingatia vigezo vitano, Mkuu wa Wilaya Iramba, mkoani Singida, Lucy Mayenga amemuomba Rais John Magufuli asimjumuishe kwenye orodha ya wakuu hao anayotarajia kuitangaza wakati wowote. Rais Magufuli ameweka bayana vigezo atakavyotumia kufanya uteuzi wa wakuu hao wa wilaya ambavyo ni pamoja na suala la migogoro ya ardhi, tatizo la elimu hasa upungufu wa madawati, njaa na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu alivyovitangaza wakati akizungumza na wazee wa Dar es Salaam na katika uteuzi wa wakuu wa mikoa, alizungumzia pia suala la wafanyakazi hewa ambao wamekuwa wakilipwa mishahara bila ya wahusika kuchukua hatua kudhibiti. Akizungumza kwenye kikao cha UWT, Mkoa wa Shinyanga mwishoni mwa wiki, Mayenga ambaye pia ni mbunge wa Viti Maalumu alisema aliwasilisha ombi hilo binafsi kwa Rais Magufuli ili apate fursa ya kusimamia biashara zake alizosema zinazodorora kutokana

Hoteli ya kigogo NSSF yazua gumzo

Image
Meneja wa Miradi Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Injinia John Msemo. Stori: Makongoro Oging’ na Issa Mnally, UWAZI DAR ES SALAAM: Meneja wa Miradi Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Injinia John Msemo anadaiwa kujenga hoteli ya kisasa yenye ghorofa tano, Makumbusho jijini Dar huku baadhi ya watu wakisema kuwa, kama mtumishi wa serikali hatakiwi kumiliki mali hiyo, Uwazi limechimba. Baadhi ya wananchi, wakiwemo majirani wa hoteli hiyo waliliambia gazeti hili kwamba, maadili ya watumishi wa serikali hayataki mtumishi wa umma kumiliki mali zenye thamani kubwa kama hoteli hiyo ambayo wao wanaikadiria kujengwa kwa mabilioni ya shilingi. SHUHUDA “Hii ni hoteli ya Msemo. Inaitwa Safina. Ina ghorofa tano. Huyu jamaa ni bosi pale NSSF, mimi sijui ni bosi wa nini lakini kwa mali kubwa kama hii sidhani kama ni halali yeye kumiliki. Muonekano wa hoteli hiyo inayomilikiwa na   Injinia John Msemo. “Hebu nyie Gazeti la Uwazi jaribuni kuchimbua ukweli au uhalali

MAGAZETI YA LEO JUMANNE TAREHE 22.03.2016

Image

MAGAZETI YA MICHEZO NA BURUDANI

Image

MAGAZETI YA UDAKU LEO TAREHE 22/3/2016

Image

Waziri Mkuu Amwagiza CAG Kukagua Bandari na Benki ya CRDB......Makampuni 150 ya Uwakala Yafunguli

Image
  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali aende Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ili akague taarifa za mapato ambazo zilikuwa zikilipwa na mawakala wa forodha na bandari kupitia benki ya CRDB lakini hazionekani kwenye mifumo ya benki. Ametoa agizo hilo leo jioni (Jumatatu, Machi 17, 2016) wakati akizungumza na mamia ya mawakala wa forodha na bandari waliohudhuria mkutano aliouitisha ili kusikiliza kero zinazowapata katika utendaji kazi wao. Akizungumza na mawakala hao kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu alisema kuna dalili za kutupiana lawama baina TPA na CRDB kuhusu malipo yaliyikuwa yakifanyika benki halafu fedha hazionekana na wakala anaidaiwa kuwa hajalipia mzigo wakati alishaulipia. “Kimsingi bado liko tatizo baina ya Mamlaka ya Bandari pamoja na Benki ya CRDB. Naona kila mmoja hapa anamkana mwenzake. Nitamtuma CAG ili akafanye ukaguzi wa kina ili tujue ni nani kati yao amehusika na upotevu wa fedha

BREAKING NEWSSS ... MKUU WA WILAYA NA MTANGAZAJI MKONGWE SARA DUMBA AFARIKI DUNIA

Image
MKUU WA WILAYA YA NJOMBE BI.SARAH DUMBA AKIWA OFISINI KWAKE ENZI ZA UHAI WAKE. Habari zilizotufikia hivi zinasema Mkuu wa wilaya wa Njombe na Mtangazaji mkongwe wa Radio Tanzania,Bi. Sara Dumba amefariki Dunia.  Taarifa zaidi tutazidi kuwaletea ...

NEWZ ALERT: WATU WANNE WAPOTEZA MAISHA NA WENGINE KUJERUHIWA VIBAYA KUFUATIA AJALI YA LORI KUYAGONGA MAGARI MATATU YA MSAFARA WA KAMATI YA TAMISEMI ENEO LA KEREGE, BAGAMOYO.

Image
WATU wanne wanahisia kufariki dunia huku 12 wakiwa wamejeruhiwa vibaya, katika ajali iliyoyahusisha magari manne, mawili yakiwa katika msafara wa Kamati ya Bunge Utawala na TAMISEMI maeneo ya Kerege, Bagamoyo Pwani, anaandika Mwandishi Wetu. Ajari hiyo iliyohusisha lori la mchanga, gari dogo yaliyokuwa yanatokea Bagamoyo kuja Dar es Salaam, na magari mawili yaliyokuwa kwenye msafara wa Kamati hiyo, yaliyokuwa yanaenda Bagamoyo kwa shughuli zake za kibunge. Magari yaliyokuwa katika msafara wa kamati hiyo, ni gari la Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) na gari la Mkurugenzi wa Wilaya ya Bagamoyo ambayo yaligongwa na lori hilo la mchanga na kusababisha vifo vya watu hao na kuwajeruhi wengine kadhaa. Ajali hiyo ilitokea baada ya gari dogo lililokuwa linatokea Bagamoyo kupunguza mwendo ghafla na kusababishwa lori lililokuwa nyuma yake kuligonga na kuhama upande wa pili na kuyagonga magari mawili yaliyokuwa katika msafara wa kamati ya Bunge. Taarifa zaidi zitawa

RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI ATEKELEZA AGIZO LA MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM PAUL MAKONDA LA KUHAKIKI SILAHA.

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia kwa makini zoezi la uhakiki wa silaha zake lililokuwa likifanywa na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Neema Laizer Ikulu jijini Dar es salaam. Mhe. Rais amekuwa mtu wa kwanza kutekeleza agizo la Mkuu wa Mko wa Dar es Salaam Paul Makonda. Kamanda wa Kanda Maalum ya Mkoa wa Dar es Salaam Kamishna CP Simon Sirro kulia akimkabidhi Silaha aina ya Bastola Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya uhakiki uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. Kamanda wa Kanda Maalum ya Mkoa wa Dar es Salaam Kamishna CP Simon Sirro kulia akimkabidhi silaha aina ya shortgun Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya uhakiki uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiiweka silaha yake vizuri mara baada ya kuhakikiwa Ikulu jijini