PICHA ZA AY NA PREZOO ZILIVUNJA NDOA YA DAYNA NYANGE

Dayna
Msanii wa muziki, Dayna Nyange amedai kilichosababisha wakaachana na mzazi mwenzake ni wivu wa mapenzi uliotokana na picha aliyopiga na wasanii wawili wa Kenya, Wahu na Prezzo pamoja na Mtanzania, Ambwene Yessaya ‘AY’.
Muimbaji huyo ambaye ni mama wa mtoto mmoja aitwae Rahma, ameliambia gazeti la Mtanzania, kuwa picha hizo alizipiga na wasanii hao kabla hajawa maarufu wala kujihusisha na muziki kwa kiasi kikubwa hivyo hiyo ilikuwa sehemu ya kutafuta marafiki wa kumsaidia kimuziki.
“Kutokana na picha hiyo mchumba wangu huyo alihisi kwamba mmoja wa wasanii hao labda natoka naye kimapenzi hivyo akawa hataki nipige picha na wasanii na nisijihusishe tena na masuala ya kimuziki,” alisema Dayna.
Aliongeza, “Muziki ni kitu ninachokipenda sana katika maisha yangu hapo nikaona wivu umezidi kwa mwezangu ambaye tumebarikiwa kupata mtoto mmoja wa kike mwenye miaka 10, tukaamua kuachana nami nikaendelea na muziki wangu hadi leo bila mchumba, mpenzi wala nini na maisha yanaenda,” alijieleza mrembo huyo.
Dayna alianza kujulikana katika muziki mwaka 2008 baada ya kuachia wimbo ‘Mafungu ya Nyanya’ ambao alimshirikisha Marlow, kisha akatoa ‘Nivute kwako’ na sasa anatamba na wimbo wa ‘Ungejua’.

CHANZO na Bongo5

Comments

Popular posts from this blog