TAASISI YA MANJANO FOUNDATION KUENDESHA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI KWA WANAWAKE WA DODOMA
Mradi
wa Kuwawezesha wanawake Kiuchumi Kupitia Tasnia ya urembo ujulikanao
kama Manjano Dream-Makers ulioasisiwa na Taasisi ya Manjano Foundation
utaendesha mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake wa Mkoa wa Dodoma
kuanzia Jumatatu, tarehe 28 March 2016 kwenye ukumbi wa LAPF House
Mkoani Dodoma. Mafunzo hayo yatatolewa kwa jumla ya wanawake
watakaochaguliwa 30 kutoka mkoani Dodoma na mikoa ya jirani.
Baada
ya mafunzo hayo wanaweke hao watakuwa chini ya uangalizi wa Taasisi
hiyo kwa lengo la kuhakikisha wanawake wa Mkoa wa Dodoma wanafikia
malengo yao waliojiwekea. Wanawake wakazi wa Mkoa wa Dodoma waliotuma
maombi na wanaopenda kunufaika na mradi huo wanaombwa kujitokeza kwa
ajili ya usaili siku ya Jumamosi tarehe 26 Machi 2016 kuanzia saa tatu
(9:00AM) asubuhi kwenye ukumbi wa wa LAPF House Mkoani Dodoma.
Mafunzo
yana lengo la kumsaidia mjasiriamali mwanamke kujikwamua na
kujiongezea kipato. Awamu ya kwanza ni kumfundisha maswala ya biashara
namna ya kuibua na kubuni miradi mbalimbali namna ya kuandika mpangilio
wa biashara ikiwemo matumizi sahihi ya rasilimali muda, kutokufuja
fedha, muda na pia namna ya kujitunzia akiba itokanayo na biashara
yake.
Awamu
ya pili itahusu kuwafundisha jinsi ya kupamba ma harusi na matumizi
sahihi ya vipodozi vya LuvTouch Manjano. Baada ya wanawake hawa kuhitimu
mafunzo haya Taasisi ya Manjano Foundation inatoa mikopo bila riba ya
bidhaa za vipodozi kwa ajili ya kuwawezesha kuanzisha biashara wakiwa
chini ya uangalizi maalum wa
Taasisi hiyo kwa lengo la kuhakikisha kila mhitimu wa mafunzo haya anapiga hatua na kuweza kujitegemea.
Wasiliana nasi kwa Simu namba +255 712 646 322 au +255 718 010 10
Comments
Post a Comment