NEWZ ALERT: WATU WANNE WAPOTEZA MAISHA NA WENGINE KUJERUHIWA VIBAYA KUFUATIA AJALI YA LORI KUYAGONGA MAGARI MATATU YA MSAFARA WA KAMATI YA TAMISEMI ENEO LA KEREGE, BAGAMOYO.
WATU wanne wanahisia kufariki dunia huku 12 wakiwa wamejeruhiwa vibaya, katika ajali iliyoyahusisha magari manne, mawili yakiwa katika msafara wa Kamati ya Bunge Utawala na TAMISEMI maeneo ya Kerege, Bagamoyo Pwani, anaandika Mwandishi Wetu.
Ajari
hiyo iliyohusisha lori la mchanga, gari dogo yaliyokuwa yanatokea
Bagamoyo kuja Dar es Salaam, na magari mawili yaliyokuwa kwenye msafara
wa Kamati hiyo, yaliyokuwa yanaenda Bagamoyo kwa shughuli zake za
kibunge.Magari
yaliyokuwa katika msafara wa kamati hiyo, ni gari la Mfuko wa Maendeleo
ya Jamii (TASAF) na gari la Mkurugenzi wa Wilaya ya Bagamoyo ambayo
yaligongwa na lori hilo la mchanga na kusababisha vifo vya watu hao na
kuwajeruhi wengine kadhaa.Ajali
hiyo ilitokea baada ya gari dogo lililokuwa linatokea Bagamoyo
kupunguza mwendo ghafla na kusababishwa lori lililokuwa nyuma yake
kuligonga na kuhama upande wa pili na kuyagonga magari mawili yaliyokuwa
katika msafara wa kamati ya Bunge.Taarifa
zaidi zitawajia hivi punde baada ya kupata taarifa kamili (Taarifa ya
awali inaeleza hivyo sijawa na uhakika nayo moja kwa moja)
Hivi ndivyo ionekanavyo moja ya gari lililohusika kwenye ajali hiyo.
Comments
Post a Comment