CCM kuweka utaratibu mpya wa kuwapokea Wanachama waliokihama Chama hicho na Kukimbilia Vyama vya Upinzani


Siku kadhaa baada ya mwanachama wa siku nyingi wa Chama cha Mapinduzi,balozi Juma Mwapachu, kurejea katika chama hicho baada ya kukihama wakati wa harakati za Uchaguzi mkuu wa mwaka jana, kimekiri kuwa kuna haja ya kusikiliza hisia za wanachama wake na kuangalia upya namna gani wanachama wa Chama hicho walioondoka na kwenda kujiunga na vyama vingine wanapokelewa kufutia mazingira ya siasa yalivyo sasa.

Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana , ametoa kauli hiyo jijini Dar Es Salaam,wakati wa mkutano na waandishi wa habari, uliolenga kumtambulisha Mjumbe wa Halmashauri kuu Ya Taifa ya Chama hicho Christopher Ole Sendeka, kuwa msemaji wake, kuchukua nafasi ya Nape Nauye, ambaye sasa ni waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Bwana Kinana, amekiri kuwa ni vyema sasa CCM ikae na kutengeneza namna ya watu fulani kurudi ama kutorudi kabisa katika chama hicho kwa kuwa kwa sasa utaratibu unatambua mchakato kumrejesha mwanachama bila kuangalia alitoka kwa mtindo upi.

Katibu Mkuu huyo wa CCM, ameenda mbali zaidi na kusema kuwa lazima chama hicho kiheshimu hisia za wanachama wake.

Akizungumza baada ya kutambulishwa, Ole Sendeka amesema CCM kinampongeza Rais John Magufuli kwa utendaji wake na kwamba huo ndio msimamo wa Chama na kukanusha maeneo yanayoelezwa kwamba huo ni udikteta na uonevu

Comments

Popular posts from this blog