Posts

Uchaguzi Zanzibar; Dk Shein, Balozi Seif wapiga kura zao

Image
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye ni mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk. Ali Mohamed Shein akipiga kura katika uchaguzi wa marudio kituo cha kupiga kura namba 1 Skuli ya msingi Bungi Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja leo, Wananchi wa Zanzibar leo wanapiga kura katika uchanguzi wa marudio baada ya kufutwa kwa uchanguzi uliofanyika Oktoba 25, 2015 kutokana na kasoro zilizojitokeza. Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ally Iddi akiwa katika maandalizi ya kupiga kura katika uchaguzi wa marudio kituo cha Skuli ya Kitope, Wilaya ya Kaskazini B, Mkoa wa Kaskazini. Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ally Iddi akipiga kura katika uchaguzi wa marudio kwenye kituo cha Skuli ya Kitope, Wilaya ya Kaskazini B, Mkoa wa Kaskazini. Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ally Iddi akizungumza na baadhi ya Waandishi wa Habari mara baada ya

Mbunge Vicky Kamata Afunga Ndoa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dk. Likwelile

Image
Mbunge wa Viti Maalamu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Vicky Kamata amefunga ndoa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dk Servacius Likwelile.Dk Likwelile amefunga ndoa hiyo baada ya mkewe wa awali kufariki dunia Mei mwaka 2014.Kwa hatua hiyo, Dk Likwelile amemfuta machozi mbunge huyo kijana baada ya ndoa yake ya awali aliyotarajia kuifunga na Charles Pai kukwama dakika za mwisho wakati wa maandalizi yote ya msingi kukamilika. Dk. Likwelile Habari ambazo Tanzania Daima imezipata, zilieleza kwamba mbunge huyo ambaye ni msanii wa muziki wa kizazi kipya , alifunga ndoa hiyo Septemba mwaka jana katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Geita. Habari zinaeleza kuwa wawili hao baada ya kufunga ndoa, hawakuwa na sherehe kubwa bali walikuwa na ‘pati mchapalo’ iliyofanyika nyumbani kwa Dk Likwelile na kuwashirikisha baadhi ya wana ndugu na marafiki wa pande zote mbili. “Wamefunga ndoa bomani, hakukuwa na sherehe bali kulikuwa na hafla ndogo iliyofanyika nyumbani na wanafamil

Maajabu ya Mungu… Meja Jenerali Afariki, Afufuka!

Image
Meja Jenerali Mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Benjamin Noah Msuya (enzi akiwa kazini). Oscar Ndauka, RISASI JUMAMOSI DAR ES SALAAM: Kweli haya ni maajabu ya Mungu! Meja Jenerali Mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Benjamin Noah Msuya (74), ameanika kwamba, alifariki dunia na mipango ya mazishi ikafanywa lakini siku nne baadaye alifufuka, hapa anasimulia alichokiona baada ya kifo, fuatana na Risasi Jumamosi. Akiwa na famimilia yake wakati akiugua. AZUNGUMZA NA RISASI NYUMBANI KWAKE, DAR Akizungumza na gazeti hili Machi 16, mwaka huu, nyumbani kwake, Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam, Msuya ambaye mwaka 1979 aliongoza majeshi ya Tanzania kuingia Uganda kwa mara ya kwanza, alisema kifo chake hicho kilitokana na ugonjwa wa saratani (kansa). MSIKIE MWENYEWE “Awali ya yote, mimi kwa sasa ni Meja Jenerali Mstaafu. Lakini katika utumishi wangu, ndiye niliyeingiza majeshi nchini Uganda mwaka 1979 na kumwangusha mtawala wa mabavu, Idi Amini

LIVE KUTOKA ZANZIBAR MDA HUU.... VIKOSI VYA 'JESHI' VYAIMARISHA ULINZI KWENYE VITUO VYA KUPIGIA KURA

Image
07:50  Safari zote za meli kati ya bandari ya Dar es Salaam na visiwa vya Zanzibar zimekatizwa. Hapa chini ni tangazo la kuwapasha wateja wa Azam Sealink kwamba hakutakuwa na safari za meli kuanzia tarehe 18 hadi 22 Machi kutokana na uchaguzi unaoendelea Zanzibar. Licha ya kukatizwa kwa safari, badi wapo watu waliojitokeza wakitarajia kusafiri. Wengi wa waliofika ni wageni kutoka Ulaya ambao hawakuwa na habari. 07:44  Usalama umeimarishwa visiwani. Hapa chini ni maafisa wa usalama wakiwa na mbwa wa kunusa kabla ya Dkt Shein kupiga kura yake katika kituo cha Bungi, Unguja. 07:42  Baadhi ya wapiga kura wakitafuta majina yao kituoni Madungu Chake-Chake, kisiwani Pemba. 07:30  Mwanamke akipakwa wino kwenye kidole chake baada ya kupiga kura kituo cha Madungu Chake-Chake, Pemba. Baadaye, atabasamu baada kutoka nje ya ukumbi. 07:20  Hii hapa ni picha nyingine ya Dkt Ali Shein, mgombea urais wa CCM baada yake kupiga kura Unguja. 07:05  Mgo

Paul Makonda Azungumza na Watendaji wa jiji la Dar

Image
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na wenyeviti na maofisa watendaji wa jiji hilo leo kati ka Ukumbi Wa Mwalimu Nyerere asubuhi kuhusu mambo mbalimbali hasu suala la usafi wa mazingira.  Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando akiongoza mkutano huo.  Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akizungumza katika mkutano huo.  Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema akizungumza katika mkutano huo.  Mwakilishi wa Taasisi ya Wakala wa Upimaji Ardhi Tanzania, Linus Kinyondo akizungumzia suala zima la ujenzi wa nyumba kwa kuzingatia mipango miji ili kutunza mazingira.  Wenyeviti na maofisa watendaji wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda (hayupo pichani) Maofisa Watendaji na Wenyeviti wa Manispaa ya Kinondoni wakipiga makofi kwenye mkutano huo. Na Mtandao wa habari za jamii

Jinsi ya Kuangalia kama Simu ni Feki

Image
  Hivi karibuni zilisambaa taarifa kwamba simu feki zote nchini Tanzania zitazimwa ifikapo mwezi Juni mwaka 2016, makala hii itakuonesha jinsi ya kuangalia kama simu yako ni feki ama la. Hatukuweza kuthibisha moja kwa moja kwamba kweli simu zitazimwa mwezi Juni lakini tumejiridhisha kuwa kutakuwa na hatua dhidi ya wanaomiliki simu feki pindi itakapofika tarehe hiyo. Zifuatazo ni hatua unazoweza kuzitumia kuangalia kama simu yako ni fake, hakuna mahitaji makubwa kufanya hili ila tu unahitaji simu yako unayoitumia na unayotaka kuiangalia. Jinsi  ya angalia IMEI namba Andika *#06# kisha bonyeza kitufe cha kupiga Baada ya hapo simu yako itakuletea IMEI namba ambapo kama simu yako au kifaa chako kina laini mbili basi kutakuwa na IMEI namba mbili Namba hii pia unaweza kuipata katika boksi la simu ama nyuma ya ya simu hiyo baada ya kutoa betri, utaijua kwa kuwa huwa ni tarakimu 15. Nakili namba hizo pembeni. Mfano wa IMEI namba iliyopatikana kwa kupiga *#06#

Pichaz za jaliyojiri kwenye usiku wa Birthday ya Linah,

Image
March 17 ni tarehe waliozaliwa watu wengi dunia lakini kutoka kiwanda cha   Bongoflevani mrembo anayemiliki hitsongs nyingi ikiwepo ‘ Malkia wa Nguvu’ ,   Linah   amesherekea siku yake ya kuzaliwa march 17 na kuudhuriwa na mastaa mbalimbali. Linah na Bilnass Neddy Music Queen Darleen na Kajala Queen Darleen, Kajala, Mwijako na Mwasiti Linah na Mdogo wake Linah na Bilnass Linah na Kajala Linah na Director Khalifani Linahna Recho Linah na Perfect Linah na Simple Linah, Mwijako na Mwasiti Linah na G Model Dj Tass, Linah na Bilnass Perfect, Bilnass na Kajala

BAADA YA WAFUASI 42 WA CUF KUKAMATWA ,MSHAURI WA MAALIM SEIF NAYE AKAMATWA NA POLISI ZANZIBAR

Image
Jeshi la Polisi linamshikilia mwanasiasa Mansoor Yussuf Himid kwa mahojiano kuhusiana na kulipuliwa kwa maskani ya CCM, Kisonge Michenzani mjini Unguja. Mansoor, ambaye ni mshauri wa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad alipigiwa simu jana jioni na polisi kwa ajili ya mahojiano katika kituo cha Madema. Kukamatwa kwa Mansoor kumekuja siku chache baada ya Jeshi hilo kuwakamata wafuasi wengine 42 akiwamo Kaimu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mawasiliano ya Umma, Hamad Masoud akituhumiwa kutoa taarifa kwamba kuna watu wamekimbilia porini na wengine wamekwenda Mombasa. Wafuasi hao 42 ambao bado wanashikiliwa ni kutokana na kuhusishwa na tukio la kulipuliwa nyumba ya Kamishina wa Polisi, Hamdan Omar Makame. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam jana alithibitisha kukamatwa kwa Mansoor na kwamba ni kutokana na hali ya matukio ya milipuko na mambo mengine, hivyo wanahitaji kupata maelezo ya kina kabla ya kumwachia. Alis

WAZIRI NAPE NNAUYE KUZINDUA MSIMU MPYA WA MASHINDANO YA UREMBO YA MISS TANZANIA 2016 JIJINI DAR

Image
Pichani kulia ni Mkurugenzi wa Lino International Agency LTD,Hashim Lundenga akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani),katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO),kuhusiana na msimu mpya wa mashindano ya Urembo ya Miss Tanzania kwa mwaka 2016.Lundenga amesema kuwa msimu huo mpya unatarajiwa kuzinduliwa rasmi siku ya jumamosi Machi 19,2016 katika hotel ya Ramada Resort iliyopo eneo la Kunduchi jijini Dar.Katika uzinduzi huo utakaokuwa wa aina yake Mgeni rasmi amepangwa kuwa ni Waziri wa Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo Mh.Nape Moses Nnauye.Kati ni Mshindi wa Miss Tanzania 2014-2015 Liliani Kamazima pamoja na Mkuu wa Itifaki wa kamati ya Miss Tanzania Albert Makoye. Lundega akifafanua jambo kwa umakini mbele ya Wanahabari (hawapo pichani). Lundenga amesema kuwa katika uzinduzi wa msimu huo mpya,utawakutanisha wadau mbalimbali wa tasnia ya Urembo wakiwemo Wabunifu wa Mavazi,Mawakala wanaoandaa mashindano ya Miss Tanzania katika ngazi mbalimbali hapa

ZIARA YAWAZIRI MKUU, CHATO NA KATORO - GEITA.

Image
  Waizri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mtambo wa kukamu mafuta ya alizeti  wanaushirika wa Chato akiwa katika ziara ya mkoa wa Geita Machi 17, 2016. Kushoto ni Mwenyekiti wa  Ushirika huo Elias Kaswahili.     Wasani wa Katoro Geita wakicheza ngoma ya Kisukuma mara baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuhutubia mkutano wa hadhara kijijini hapo  Machi 17, 2016.   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia Mkutano wa hadhara katika mji wa Katoro , Geita Machi 17, 2016.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)