Breaking News!! MSAFARA WA KAMATI YA BUNGE WAPATA AJALI,WATU WANNE WAFARIKI,6 WAJERUHIWA

 

Watu wanne wamefariki dunia na wengine sita wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha msafara wa kamati ya TAMISEMI baada ya lori kuparamia msafarahuo eneo la Mapinga Bagamoyo mkoani Pwani. 


Ajali hiyo iliyohusisha lori la mchanga, gari dogo yaliyokuwa yanatokea Bagamoyo kuja Dar es Salaam, na magari mawili yaliyokuwa kwenye msafara wa Kamati hiyo, yaliyokuwa yanaenda Bagamoyo kwa shughuli zake za kibunge.


Magari yaliyokuwa katika msafara wa kamati hiyo, ni gari la Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf) na gari la Mkurugenzi wa Wilaya ya Bagamoyo ambayo yaligongwa na lori hilo la mchanga na kusababisha vifo vya watu hao na kuwajeruhi wengine kadhaa. 

 Aidha mingoni mwa waliofariki ni pamoja na DPLO- Hilda, Mwanasheria Kiliba, Mchumi- Pallangyo, na M adereva wawili.
Majeruhi wa ajali hiyo ni Mkurugenzi(DED)-Matovu,Engeneer wa maji-Juliana,Mweka hazina- Mashauri,Afisa maendeleo ya jamii-Mwangata,na Mratibu TASAF-Amedus Mbuta

Ajali hiyo ilitokea baada ya gari dogo lililokuwa linatokea Bagamoyo kupunguza mwendo ghafla na kusababishwa lori lililokuwa nyuma yake kuligonga na kuhama upande wa pili na kuyagonga magari mawili yaliyokuwa katika msafara wa kamati ya Bunge.
Tutawaletea taarifa kamili hivi punde....

Comments

Popular posts from this blog