Mfanyabiashara Afia Hotelini na Kete 30 za Heroin
Mfanyabiashara wa dawa za kulevya, Kervin Mafita (40),mkazi wa Kinondoni, Dar es Salaam, amekutwa amekufa kwenye Hoteli iliyopo jijini Arusha akiwa na shehena ya dawa hizo aina ya heroin tumboni mwake. Meneja wa hoteli hiyo, Bw. Douglas Minja, alisema marehemu alifika hotelini hapo Aprili 12, mwaka huu, akiwa ameongozana na mama yake mzazi, mdogo wake na mtoto wake mwenye umri wa miaka 11 na kukodi vyumba viwili. Alisema Aprili 15, mwaka huu, saa nne asubuhi, mhudumu wa hoteli alienda kugonga chumbani kwa marehemu ili aweze kufanya usafi na baada ya kufunguliwa mlango, ndani kulikuwa na marehemu, mama yake na mgodo wake marehemu. Aliongeza kuwa, ndugu hao walidai muda huo walikuwa na mazungumzo hivyo hawakutaka usumbufu ambapo kutokana na majibu hayo, muhudumu huyo alilazimika kuwapisha ili waendelee na mazungumzo yao. "Baada ya saa moja, ndugu wawili (mama na mdogo wa marehemu), walitoka na kutokomea kusikojulikana ila mtoto wak