HIZI NDIO TAARIFA ZENYE UHAKIKA KUHUSU ALIYEKUWA MPENZI WAKE LULU MICHAEL
Mitandao ya kijamii kuanzia kwenye Whatsapp mpaka twitter, Facebook
na Instagram siku hizi imekua na nguvu kubwa na ndio maana hata taarifa
zinaenea kwa kiasi kikubwa sana siku hizi bila kungoja Magazeti, Radio
au TV.
Secky alikua rafiki wa watu wote wakiwemo wasanii wengi wa bongofleva na hata bongomovie pia ndio maana msiba huu umewagusa kutokana na ukarimu wake kwao akiwemo Wema Sepetu ambae amesema >>> ‘Ulikua
mtu wa watu, sanaaaaa…… najua utaliliwa na wengi…. they say vizuri
havidumu, pumzika kwa amani baba…. It’s jus too hard to sink in….‘
Najua kama unafatilia habari zinazoendelea
mjini utakua umekutana na voicenote au taarifa ya kifo cha huyu ndugu
yetu inaweza kuwa imekufikia lakini sio kwa usahihi, au chanzo cha kifo
kinaweza kuwa kimepotoshwa.
Sasa familia ya Marehemu Lusekelo Samson Mwandenga (Secky)
imekanusha taarifa zinazoendelea kusambazwa kupitia voice note na
kwenye mitandao kuhusu chanzo cha kifo chake na kwamba alikwenda kwenye
birthday,
"ukweli ni kwamba aliumizwa na kiti cha kioo akiwa kambeba
mtoto wake nyumbani kwake, akapelekwa hospitali na baadae akafariki
akiwa Hospitali, hakuna kingine zaidi ya hapo".
Diamond Platnumz ameandika ‘Gone too soon my Brother… i still don’t wanna believe that you are realy Gone….dah si jana tu tumezungumza’
R.I.P Secky.
Comments
Post a Comment