Nalimi
Mayunga (katikati) akiwa amefurahi hadi akitaka kuanguka baada ya
kutangazwa mshindi kwenye Shindano la Airtel Trace Music Star.
Mayunga (kushoto) akiwa haamini kama jina lake ndio limetajwa ndiye mshindi wa shindano hilo.…
Nalimi
Mayunga (katikati) akiwa amefurahi hadi akitaka kuanguka baada ya
kutangazwa mshindi kwenye Shindano la Airtel Trace Music Star.

Mayunga (kushoto) akiwa haamini kama jina lake ndio limetajwa ndiye mshindi wa shindano hilo.
Mayunga (katikati) akiwa na wadau mbalimbali akiwa ameshikilia tuzo yake.

Mayunga akiimba.
Watanzania wakishangilia baada ya Mayunga kuibuka mshindi.
MTANZANIA Nalimi Mayunga ameshinda mkataba wa
kurekodi muziki na Label ya Universal Music wenye thamani ya dola
500,000 ambayo ni shilingi milioni 900 kwenye Shindano la Africa Airtel
Trace Star lililofanyika nchini Nairobi, Kenya Jumamosi iliyopita.
Mayunga aliwashinda wasanii wengi kutoka nchi mbalimbali za Afrika.
Washiriki wawili walioingia kwenye hatua ya tatu bora sambamba na
Mayunga ni Jitey wa Nigeria na Baz kutoka Congo Brazzaville.
Nchi zilizoshiriki katika shindano hili ni Burkina Faso, Democratic
Republic of Congo (DRC), Chad, Congo Brazzaville, Gabon, Ghana, Kenya,
Madagascar, Malawi, Nigeria, Tanzania, Uganda na Zambia.
Baada ya mchujo zilibaki nchi sita ambazo Uganda, Madagascar, Malawi,
Tanzania, Nigeria na Congo Brazzaville na hatimaye ukafanyika mchujo
mwingine na kubaki nchi tatu, Nigeria, Congo Brazzaville na Tanzania.
Mayunga ni mtoto wa mwisho kwenye familia yao yenye makazi yao mjini Morogoro.
Comments
Post a Comment