Posts

Breaking News: Polisi Yakanusa DCI, Mambosasa Kuondolewa

Image
Msemaji wa Jeshi la Polisi, Barnabas Mwakalukwa. MSEMAJI wa Jeshi la Polisi nchini, Barnabas Mwakalukwa, amekanusha taarifa zinazozagaa mitandaoni zinazohusu jeshi la polisi kufanya mabadiliko na kuomba wananchi kuzipuuza. Taarifa ya msemaji hiyo imeeleza kuwa mkuu wa jeshi hilo, IGP Simon Sirro,  amewataka wananchi kuzipuuza taarifa hizo zenye lengo la kupotosha umma na kuwataka kuacha kutumia mitandao ya kijamii na badala yake waitumie kupeana taarifa za kuleta maendeleo. “Serikali na vyombo vyake ina utaratibu maalum wa kutoa taarifa kwa umma,” ilisema taarifa ya Mwakalukwa. Taarifa ambazo si za kweli  zilidai Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Boaz, wamepangiwa majukumu mengine. Ziliongeza kusema kuwa Mambosasa amerejeshwa makao makuu kwenye kamisheni ya ushirikishwaji jamii,  na Charles Kenyela amekuwa DCI mpya huku Mkuu wa Chuo cha Polisi Moshi, SACP Ramadhan

Ajali mbaya yatokea Singida, Watu watano wameripotiwa kupoteza maisha

Image
Watu watano wameripotiwa kupoteza maisha kwenye ajali ya gari iliyotokea eneo la Njirii wilayani Manyoni mkoani Singida leo Oktoba 21. Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, kamishna msaidizi wa polisi Sweetbert Njewike, amesema kuwa ajali hiyo imehusisha magari mawili ikiwemo gari dogo mali ya Wizara ya Kilimo na Chakula iliyokuwa na watu watano pamoja na lori. Kamanda Njewile amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari ndogo iliyokuwa katika mwendokasi ikijaribu kupishana na lori. "Gari ndogo mali ya Wizara ya Kilimo na Chakula ilikuwa ikitokea Dodoma kwenda Shinyanga ikiwa na watumishi wa wizara hiyo, ilikuwa katika mwendokasi na kugongana uso uso na Lori", amesema Kamanda Njewile. Kamanda amewataja waliofariki kuwa ni wanawake wawili na wanaume watatu na wote wamehifadhiwa katika hospitali ya Wilaya ya Manyoni.

Jinsi ya kuruka vihunzi vya mwanume anayekutongoza mara kwa mara

Image
Miongoni mwa kero ambazo huwakumbuka wadada wengi ni pamoja na kutongozwa, jambo hili  huwa halikwepeki kwani lipo tu. Hivyo kama wewe ni msichana ambaye upo  kwenye mahusiano na bado unaendelea kukutana na ushawishi wa kutongozwa kila iitwapo leo pindi ukutapokutana na mtu ambaye anakutongoza unatakiwa kuwa hivi. 1. Usijibu mtu huyo simu wala texts zake.  Kitu cha kwanza cha kufanya ni kuhakikisha kuwa haujibu simu zake wala kumtext hata kama umeboeka. Ukiwa unajibu simu zake basi utakuwa unampa matumaini kuwa uko interested na yeye. Ukimzima baada ya muda flani bila shaka atakuja kuelewa – ama unaweza tu kumpa ile hotuba ya kuwa wewe na yeye hamulingani. 2. Mblock katika mitandao ya kijamii.  Kando na kuwa hujibu sms zake wala simu zake, unapaswa kublock contacts zake zote katika mitandao ya kijamii ambazo unazijua. Kama unahisi kumblock utakuwa umevuka mipaka yakuonekana mbaya, na unaona si t

TFF Yapangua Kikosi Cha Simba

Image
Kikosi cha timu ya Simba SC. KIKOSI cha Simba ambacho kitashuka dimbani kesho kumenyana na Stand United kitakuwa na mabadiliko makubwa kutokana na sababu mbalimbali. Simba, kesho Jumapili itakuwa Uwanja wa Taifa kusaka alama tatu muhimu mbele ya Stand United. Hata hivyo, Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji, Patrick Aussems amelazimika kukifanyia mabadiliko kikosi chake hicho kutokana na baadhi ya wachezaji wake kukumbana na adhabu mbalimbali kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). Mabadiliko hayo ya kikosi cha Simba yanahusika zaidi kwenye safu ya ulinzi ambapo nyota wake wawili James Kotei na Erasto Nyoni wataukosa mchezo huo kutokana na kufungiwa na TFF. Wachezaji hao walibainika walifanya vitendo vya utovu wa nidhamu. Pia Simba itamkosa nahodha wake, John Bocco ambaye naye alikumbwa na adhabu hiyo. Kiungo Jonas Mkude anaweza kukosekana kutokana na kuwa majeruhi. Aussems ameliambia Championi Jumamosi kuwa, kutokana na hali hiyo amelazimika kukifanyia mabad

ADAKWA AKITOA MAHARI NG’OMBE WA WIZI

Image
BUNDA: Dunia ina mambo! Hivyo ndivyo unavyoweza kusema kufuatia tukio la bwana harusi mtarajiwa, James Marwa, mkazi wa Wilaya ya Serengeti mkoani Mara kunaswa akitoa mahari ya ng’ombe 10 wa wizi ili amuoe Prisca Faustine, mkazi wa Kijiji cha Kihumbu wilayani Bunda katika Mkoa wa Mara. Tukio hilo la aina yake limetokea Oktoba 3 mwaka huu, majira ya saa 3:00 katika Kijiji cha Kihumbu, Kata ya Hunyari, wilayani Bunda na kusababisha bwana harusi mtarajiwa huyo kuambulia kipigo na kukosa mke, kabla ya kuangukia mikononi mwa polisi. Tukio hilo la kufedhehesha lilimkumba Marwa baada ya Chacha Nyamahi, mkazi wa Kijiji cha Makundusi, Kata ya Nata wilayani Serengeti kuuarifu uongozi wa Kijiji cha Kihumbu kuwa anatafuta mifugo yake (ng’ombe) 48 ambao waliibwa wakiwa malishoni Oktoba 2, mwaka huu. Nyamahi alisema siku hiyo, akiwa safarini majira ya alfajiri, kijana mmoja alifika nyumbani kwake na kumkuta mkewe pamoja na mchungaji wa ng’ombe zake zipatazo 300 akawaambia

BREAKING NEWS: Bongo Muvi Yapata Pigo, Muigizaji wa Filamu Afariki Dunia

Image
BREAKING NEWS: Aliyewahi kuwa msanii wa maigizo wa Kundi la Sanaa la Kaole, Ramadhani Mrisho Ditopile maarufu kama Mashaka amefariki dunia katika Hospitali ya Amana iliyopo Ilala jijini Dar es Salaam leo Jumamosi, Oktoba 20, 2018 majira ya saa 3, asubuhi.

Ratiba ya kuagwa na kuzikwa Isack Gamba hii hapa

Image
Marehemu Isack Gamba Mwili wa aliyekuwa mtangazaji wa zamani wa IPP media, kupitia Radio One na ITV kabla ya kuhamia Idhaa ya Kiswahili ya Ujerumani, Deutche Well DW, Isack Gamba anatarajiwa kuzikwa Bunda mkoani Mara mapema wiki ijayo. Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo  ya habari jijini Dar es salaam, mwili wa Isack Gamba utawasili nchini jumatatu ya wiki ijayo na shughuli ya kuaga mwili huo zitaanza wiki hiyo. Pia taarifa hiyo imeeleza kuwa kwa upande wa Dar es salaam, msiba upo kwa dada yake, Gongo la Mboto, kituo kipya. Na kwa anayetaka kufika anaweza kuuliza Mongolandege kwa Mandai, Mbuyuni. Aidha kwa mujibu wa taarifa hiyo mara baada ya zoezi la kuuaga mwili wa Isack Gamba mwili huo utasafirishwa kuelekea Bunda Mkoani Mara mahali alipozaliwa kwa ajili ya mazishi ya mwili wake. Oktoba 18 mwaka huu kulisambaa taarifa juu ya kifo cha mtangazaji nguli wa zamani alikutwa akiwa amefariki nyumbani kwake mjini Bonn Ujerumani ambapo ilisadikika kabla

Msigwa Kumburuza Mahakamani RC Hapi

Image
Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa amesema  atamfikisha mahakamani Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi  kufuatia uamuzi wake wa kumuweka ndani diwani wa Viti maalum CHADEMA, Silestina Jonso. Msigwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Iringa jana Octoba 2, alisema Hapi alimdhalilisha diwani huyo. “Alidiriki kumdhalilisha diwani wetu, sheria iko wazi sana, vipengele vyote vile mkuu wa mkoa hakufuata, amekiuka, ametoa amri ya kumpeleka diwani wetu polisi kinyume cha sheria. “Sasa kwa sababu amekiuka taratibu, mimi kama mwenyekiti wa kanda na mbunge ili kukomesha tabia hii ya RC Hapi  tumwambie hatukubaliani naye na hatujalala, anakuja na sheria zake za kutisha watu na kuwatia ndani. "Tumejipanga vizuri tunamfungulia kesi mahakamani kwa sababu anatumia madaraka yake vibaya. Tutakutana naye mahakamani kwa sababu anatumia madaraka vibaya.” Alisema Msigwa

Nafasi za Kazi zilizotangazwa Leo Aug 3

Image
Bonyeza links zifuatazo kusoma zaidi na kuapply 20 Field Marketing Representatives Jobs at MoGo Tanzania Limited 8 Jobs at Tanzania National Roads Agency (TANROADS) 4 Jobs at Zanzibar University Marketing Manager Job at Transsnet Financial Team Leader at KPMG’s International Development Advisory Services (IDAS) Shop Manager at Miniso Tanzania Company Limited Area Manager at at Miniso Tanzania Company Limited Training and Development Officer at Miniso Tanzania Company Limited Nafasi zingine ingia  www.ajirayako.co.tz

KUVISHWA PETE YA UCHUMBA, SIRI 3 KILIO CHA LULU ZAFICHUKA

Image
Elizabeth Michael ‘Lulu’ kuvishwa pete ya uchumba na Francis Shiza ‘Majizo B AADA ya wikiendi iliyopita staa ‘grade one’ wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kuvishwa pete ya uchumba na bosi wa Radio EFM, Francis Shiza ‘Majizo’ na kuangua kilio cha aina yake, siri tatu (3) zimefichuka, Risasi Mchanganyiko linakupa habari kamili. Kwa mujibu wa mtu aliyehudhuria, shughuli hiyo iliyofanyika nyumbani kwa Majizo, Mbezi-Beach jijini Dar ilikuwa ya aina yake kwani watu walifurahi kwa kula na kunywa huku mastaa wa filamu wakionekana kutoalikwa au kutokuwepo. “Unajua ishu ya Lulu kuvishwa pete ya uchumba ilikuwa ni siri sana ndiyo maana hakukuwa hata na mastaa wenzake wa filamu zaidi ya mwigizaji Mahsein Awadhi ‘Dk Cheni’ ambaye alikuwa mshehereshaji lakini ilifana kwani mpaka Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda alikuwepo,” alieleza mtu huyo kwa sharti la kutotajwa gazetini. SHEREHE ILIKUWA HIVI Chanzo kiliendelea kutiririka kwamba sherehe ilianza vizuri

Prince William, Kukutana na Rais Magufuli

Image
Mwanamfalme William wa Uingereza Mwanamfalme  (Prince) William wa Uingereza anapangiwa kukutana na Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli wiki ijayo wakati wa ziara yake ya siku saba Afrika. Anatarajiwa kuzuru pia Kenya na Namibia katika ziara hiyo ambayo si ya kikazi. Ziara hiyo itafanyika kuanzia 24 Septemba hadi 30 Septemba. Lengo kuu litakuwa kufuatilia juhudi za kukabiliana na ujangili na uhifadhi wa wanyama. Atafanya ziara hiyo katika wadhifa wake kama rais wa mashirika yanayotetea uhifadhi wa wanyama ya United for Wildlife na Tusk Trust. Amekuwa pia mlezi wa shirika la Royal African Society linalolenga kukuza uhusiano kati ya Afrika na Uingereza na hushiriki sana juhudi za kukabiliana na ujangili. Akiwa ziarani Tanzania, atafanya mashauriano na Rais Magufuli kuhusu juhudi zinazopigwa na taifa hilo katika kukabiliana na ujangili kwa mujibu wa shirika la habari la Press Association. Kadhalika, atazuru bandari ya Dar es Salaam kujifahamisha zaidi kuhusu juhudi

Tamko la Masoud Djuma kuhusiana na kuzikosa safari mbili

Image
Baada ya kuzikosa safari mbili za Klabu ya Simba kuelekea Mkoani, Kocha Msaidizi wa timu hiyo Masoud Djuma,  amesema kuwa amebakia Dar es Salaam kwa majukumu makubwa mawili. Taarifa imeeleza kuwa Djumma amesema hakuweza kuambatana na Kikosi cha Simba kuelekea Mtwara pamoja na Mwanza kutokana na kupewa majukumu na Kocha Mkuu, Patrick Aussems ya kuwasoma Yanga wakicheza Taifa. Djuma alihudhuria mechi ya Yanga jana dhidi ya Coastal Union ili kujua timu hiyo mbinu inazozitumia kuelekea mechi yao ya watani wa jadi Septemba 30 2018. Mbali na kuwapigia chapuo Yanga, Djuma amesema amesalia Dar es Salaam kuendelea kuwanoa wachezaji ambao hawasafiri na kikosi kwenda Mwanza kucheza na Mbao ili kuwaweka fiti zaidi. Juuko Murushid pamoja na Haruna Niyonzima, ni baadhi ya wachezaji ambao wapo kwenye program hiyo chini ya Djuma wakijifua kurejesha makali yao baada ya kutokuwa na timu kwa muda mrefu.

Dogo Janja, Uwoya wamwagana rasmi? Madee atoa majibu

Image
Kufuatia kusambaa kwa taarifa za kumwagana chini kwa wanandoa mastaa, Dogo Janja na Irene Uwoya, Baba wa muziki wa Janjaro, Madee amekanusha tetesi hizo akiziita ni uvumi na kwamba wawili wao hawana tatizo lolote. Stori za mastaa hao kumwaga zimezidi kuenea zaidi siku za hivi karibuni zikichagizwa na kitendo cha Uwoya kutoonekana Hospitalini alipokuwa amelazwa Janjaro ambaye anaumwa. " Hakuna taarifa kama hizo, Janja na Uwoya wapo kama kawaida hawajatemana kama ambavyo inaenezwa, hizo ni tetesi tu au niite ni uzushi, nachokuambia wale bado ni mtu na mke wake hizo stori za kuachana mnazipika nyie," amesema Madee. Lakini leo Uwoya alizidisha kasi ya watu kuamini kuwa hakuna ndoa baina ya wawili hao baada ya kujibu comment ya shabiki wake kwenye Instagram aliyeandika, " Dogo Janja atakufa Irene" kisha Uwoya kujibu, " hapana, simlisema wenyewe nitafute wa umri wangu yeye bado mdogo? sasa nimefuata ushauri jamani...au kashakua?"  Masta

Mwili wa Dk Misanya Bingi waagwa Dar, kuzikwa Dodoma

Image
MWILI wa aliyekuwa mtangazaji mahiri nchini na Mhadhiri wa Shule ya Habari na Mawasiliano ya Umma (SJMC) iliyo chini ya Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Dkt Misanya Bingi (47) umeagwa leo katika Kanisa Katoliki la Makongo Juu liliopo Dar es Salaam na kusafirishwa kuelekea Mjini Dodoma kwa ajili ya mazishi siku ya kesho. Dkt Misanya Bingi alifariki dunia siku Jumapili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na wakati wa uhai wake alifanya kazi kwenye kituo cha Radio One ambapo alitangaza vipindi mbalimbali kikiwemo kipindi cha Chemsha Bongo siku za Jumanne na Ijuma saa tatu usiku. Hadi umauti unamkuta alikuwa akifundisha SJMC, tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. na kabla ya hapo Misanya Bingi alikuwa mtangazaji kwenye kituo cha Radio One kazi aliyoanza kuifanya mwaka 1996.

Tazama ‘FLYOVER’ Inavyofanya Kazi TAZARA

Image
Septemba 15, 2018 daraja la juu ‘flyover’ lililopo katika makutano ya Tazara lilifunguliwa na magari yakaanza kupita na uzinduzi rasmi unategemea kufanywa na Rais Magufuli mwezi ujao. Mradi huu ambao ni wa thamani ya Sh bilioni 95 unatekelezwa na kampuni ya Oriental Consultans Global na Eight Japan Engineering Consultants, zote za Japan. Rais John Magufuli alizindua ujenzi wa ‘flyover’ hii Aprili, 2016 na kueleza kuwa lengo ni kupunguza kero ya foleni jijini Dar es Salaam pindi itakapomalizika na kuanza kutumika. GLOBAL TV imefunga safari mpaka maeneo ya Tazara jijini Dar es Salaam kushuhudia ile barabara ya juu (FLYOVER) iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na Watanzania ambao hivi sasa imesaidia kupunguza foleni kwa kiasi kikubwa. Baada ya kufika eneo la Tazara na kuona uzuri wa barabara hiyo na jinsi ambavyo magari yanapita, tukaamua kukielekeza kipaza sauti chetu na Wananchi wanaoishi kandokando ya barabara hiyo na kuwasikiliza wanalipi la kusema mara ba

Faida tatu za kusamehe

Image
Katika tafiti ambazo zimewahi kufanywa na wanasaikolojia miaka ya nyuma, waligundua ya kwamba watu wengi hawana maendeleo yao binafsi kwa sababu hawatambui nguvu ya msamahama iliyovyo na nguvu katika safari ya Mafanikio. Tafiti hizo hizo zinaendelea kusema watu wengi wanashindwa kufanikiwa kwa sababu wamebeba mizigo mizito ndani nafsi zao. Mizigo hiyo mizito ambayo inawezekana kuna mtu alisabibisha mtu kuwa katika hali hiyo. Kwa mfano inawekana kuna ndugu,rafiki, mzazi aliwahi kufanya au kukutamkia maneno mazito ambayo yanakufanya Leo, kesho mpaka kesho kutwa usiwe kuyasahau. Maneno au vitendo hivyo vimekusababisha kwa kiasi kikubwa hupunguza hamasa za kiutendaji, magonjwa na mawazo mengi (stress). Hebu tuangalie japo kwa uchache ni kwa kiasi gani madhara ya kutokusamehe yanavyoweza kukuathiri. Msipo msamehe mtu kunakupekea kwa kiwango kikubwa kuweza kupunguza uwezo wa kufikiri vitu vipya, hata hivyo pamoja na kupunguza uwezo wa kufikiri kunakupelekea kuzama kati

MAGAZETI YA LEO 19/9/2018

Image